Kasi ya ndoa kuvunjika imezidi jamani

Kasi ya ndoa kuvunjika imezidi jamani

The only

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2011
Posts
11,088
Reaction score
14,576
Hasa hizi ndoa za kuanzia 2005 kuja mbele sababu ikielezwa ni:
-Urahisi wa kufuatiliana haususani mitandao ya kijamii
-Usugu tabia wa wanawake wengi wanaendesha ndoa kwa tamthilia za ki Indonesia
 
Kwahiyo dhumuni la mada yako ni nini sasa?
Mbona nashindwa kuelewa ,umetoa kama wazo ,ushauri ,tangazo ,rai ,mbiu au nini ?,Hebu jazia maneno acha uswahili!
 
Kuoana katika umri mdogo siku izi imekuwa fashion (Hasa wanawake kuolewa ktk umri mdg) akili zinakuwa bado hazijapevuka kuhimili mikikimikiki ya kifamilia
Mitandao ya kijamii ndo Source kubwa ya haya majanga
Finally, Watu hawafuati misingi ya kiimani katika Ndoa
 
Hasa hizi ndoa za kuanzia 2005 kuja mbele sababu ikielezwa ni:
-Urahisi wa kufuatiliana haususan mitandao ya kijamii
-Usugu tabia wa wanawake wengi wanaendesha ndoa kwa tamthilia za ki indonesia
Usiombe mchokane ndani ya nyumba
 
Ndoa ni taasisi moja pana sana..ubinafsi na kukosa tafakuri ndio chanzo
Nakaaga nawazaga sipati majibu hili eneo, walioa wanataka kutoka nje ya ndoa sijui nje kuna nn, walio olewa nao wanasema angejua mapema angesubiri, walioa kama ni christian anatamani din ingeruhusu aoe mke wa pil ili asogeze X au mwingine.
Huu mtihani
 
Chini ya jua hakuna mkamilifu la hata mmoja.. Ila hao wanaosema hivyo ni wale wa uchumba wa miezi 9 na mbaya zaidi wakikutana wanandoa wawili ambao kati yao hakuna hata mmoja aliye tayari kutoa bali kila mmoja ana matarajio ya kupokea tu... matatizo huanzia hapo
 
Chini ya jua hakuna mkamilifu la hata mmoja..Ila hao wanaosema hivyo ni wale wa uchumba wa miezi 9...na mbaya zaidi wakikutana wanandoa wawili ambao kati yao hakuna hata mmoja aliye tayari kutoa bali kila mmoja anamatarajio ya kupokea tu ...matatizo huanzia hapo
Its true bro
 
Ndoa ni taasisi moja pana sana..ubinafsi na kukosa tafakuri ndio chanzo

Mwanamke amesahau sehemu yake/nafasi yake katika ndoa. Wengi wanadhani kuambiwa kuwa "Nakupenda" maana yake ni kwenda kuvuliwa pichu baasi. Hata watoto kwao sio kitu muhimu, muhimu kwao kumtimizia Mr haja zake.

Hapana. Ndoa kwa mwanamke ni zaidi ya kutumiwa kama burdani. Neno "Wote sawa" kwa mwanamke lisipate nafasi. Ndio maana anaacha/anaondoka kwao na kuhamia kwa Mr. Akiishaingia kwake tiyari anamkabidhi mikononi mwake Mr uhuru na utashi wake wote. Anabadilika sasa anakuwa Mrs. Yaani Mr's. Mali ya mtu.

Wanapoanza kutafuta haki zao, si ina maana anataka kumnyang'anya Mr mali zake?? Wanawake washuke tu ka zamani ndipo tutapata wake zetu tena. Ndoa za sasa ni kama jirani alichelewa kwenda kwao akaomba kuukata usiku kwako tu
 
Chini ya jua hakuna mkamilifu la hata mmoja..Ila hao wanaosema hivyo ni wale wa uchumba wa miezi 9...na mbaya zaidi wakikutana wanandoa wawili ambao kati yao hakuna hata mmoja aliye tayari kutoa bali kila mmoja anamatarajio ya kupokea tu ...matatizo huanzia hapo

Moja ya chanzo ni kuwa wanawake wengi walipoolewa waliwapendea wanaume zao pesa, so ikitokea mikiki mikiki kidogo, ndoa inaisha Mshana Jr
 
Kuoana katika umri mdogo siku izi imekuwa fashion (Hasa wanawake kuolewa ktk umri mdg) akili zinakuwa bado hazijapevuka kuhimili mikikimikiki ya kifamilia
Mitandao ya kijamii ndo Source kubwa ya haya majanga
Finally, Watu hawafuati misingi ya kiimani katika Ndoa
nadhani umemaliza mkuu
 
Mitindo ya maisha ya vijana wengi, kutoheshimiana ndani ya ndoa, kupuuzia majukumu, kuendekeza masuala yasio na msingi. Umalaya na unywaji pombe kupita kiasi
 
Taifa imara ni intergration ya familia imara na ili uweze kuwa na familia imara basi lazima kuwe na ndoa imara ambayo imejengwa katika misingi halisi ya upendo na ndoa iliyojengwa ktk misingi ya upendo siku zote huwa ya furaha na amani.Ndoa nyingi zipo hoi au zishakufa ,ndio maana siku hizi masingo maza kibao,watoto wamitaani,mitototo yenye tabia mbovu ni output ya ndoa zilizokosa upendo hatimaye kuvunjika.

Ujue wakati mnaingia kwenye ndoa kuna maneno ya viapo wakati wa ndoa ambayo kabla ya kutaka kufunga ndoa lazima ujipime utayaweza kuyashika na kuyaishi "kwa ugonjwa na uzima,utajiri na umasikini",kama huwezi usingie kwenye ndoa kwani utakuwa msalaba ambao utamkosesha mwenzako furaha na amani(utamfanya ahisi yupo kuzimu)..

Tatizo ndoa nyingi zinavunjika sababu wanandoa wenyewe ni wabinafsi na ubinafsi wao wanaingia nao mpaka kwenye ndoa zao mwisho wa siku ndoa chali.Ndoa ni kushare amani,furaha,ufukara,uzima,kipato nk ila kuna watu hao changu changu ,chako changu na kuna wengine wanaingia kwenye ndoa basi ili mradi lkn zipu zao mbovu.

Kitu chengine kinachovunja ndoa hii 50/50 hasa kwa wanawake wenye vipato na elimu kubwa ,hela zao huwapa kiburi.Fanya ufanyavyo huwezi kuenda against na mungu,kwani yeye ndio muasisi wa ndoa, kwa hiyo ili ndoa idumu lazima kila mtu atimize mahukumu yake ya asili aliyopewa na mungu.

Na asikudanganye mtu hakuna maisha magumu kama ya upweke(siku zote wawili ni wawili tu),japo kuna baadhi ya ndugu zangu wana maeno yao ya kishujaa "kwani lazima kuolewa au kuoa".Kuoa au kuolewa si lazima lkn je utaweza kuishi kadri ya mungu alivyotuagiza au utaweza kuzishinda tamaa za kimwili.Usiombee ktk maisha yako ukamkosa mtu wakukushauri,kukufariji,kukuliwaza,kufukurahisha,kukutia nguvu wakati umekata tamaa na kushare nae maumivu ya ndani kotoka katika moyo wako basi utakuwa na msongo wa mawazo na kudondokea kwa wanaume au wanawake mbali mbali mwisho wa siku utu na thamani yako itashuka na utakuwa mtu mwenye maisha ya kutanga tanga.
 
Kukosa nia ya dhati ya kuoana
 
Back
Top Bottom