Hayo mambo makubwa aliyoyafanya ambayo hayajawahi kufanywa, wameyataja?
1. Ndege tulikuwa nazo, tena nyingi zaidi awamu ya kwanza
2. Umeme - tulijenga Mtera, Kihansi, Kidatu na vinu vya gas
3. Barabara - awamu ya 4 kulijengwa zaidi ya km 2,500. Safari hii, ngwe ya kwanza inaisha bila kufikia hata km 1,000
4. Treni - Kulijengwa reli ya Uhuru toka Dar mpaka Kaprimposhi, Zambia. Umbali karibu wa km 2,000. Ya sasa inaishia Makutupora, haifiki hata km 400.
5. Hospitali - ilijengwa Muhimbili, Rufaa Mbeya, Dodoma, Mloganzila. Safari hii hakuna hata moja ya rufaa iliyojengwa. Hospitali za mikoa zilijengwa kila mkoa, safari hii zinapandishwa madaraja lakini siyo kujengwa
6. Elimu - zilijengwa sekondari, vyuo vikuu UDSM, Sokoine, Mbeya, UDOM, n.k. Safari hii hakuna kipya hata kimoja
7. Vituo vya utafiti - zilijengwa research centres za kilimo, ufugaji, uvuvi, magonjwa ya binadamu, n.k. Awamu hii hakuna hata kimoja kilichojengwa.
Serikali awamu hii, kama awamu ziluzopita, inajitahidi kutimiza wajibu wake LAKINI kusema inafanya cha pekee ni UWONGO.