Kasi ya kuleta maendeleo ya Rais Magufuli yawafurahisha waislamu, wamuombea dua njema kwenye baraza la Eid

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,746
139,528
Waislamu kwa umoja wao wamesema wanaridhishwa na kasi ya maendeleo inayoongozwa na Rais Magufuli.

Viongozi wa bakwata wamesema serikali ya awamu ya tano imefanya mambo makubwa ambayo hayajawahi kuonekana huko miaka ya nyuma
Hayo yamesemwa katika baraza la Eid el hajj huko Chanika nje kidogo ya jiji la Dsm.
Pia dua maalum ya kumuombea Rais Magufuli ilisomwa na sheikh kiongozi

Source channel ten
 
Asante sana serikali ya ccm kwa malezi bora ya taasisi hii ya Bakwata.
 
1. Waislamu kwa umoja wao wamesema wanaridhishwa na kasi ya maendeleo inayoongozwa na Rais Magufuli.

2. Viongozi wa bakwata wamesema serikali ya awamu ya tano imefanya mambo makubwa ambayo hayajawahi kuonekana huko miaka ya nyuma
Kama kweli wewe unajua kiswahili vizuri, angalia kama kauli zako namba moja na namba mbili zinaendana
 
Hayo mambo makubwa aliyoyafanya ambayo hayajawahi kufanywa, wameyataja?

1. Ndege tulikuwa nazo, tena nyingi zaidi awamu ya kwanza

2. Umeme - tulijenga Mtera, Kihansi, Kidatu na vinu vya gas

3. Barabara - awamu ya 4 kulijengwa zaidi ya km 2,500. Safari hii, ngwe ya kwanza inaisha bila kufikia hata km 1,000

4. Treni - Kulijengwa reli ya Uhuru toka Dar mpaka Kaprimposhi, Zambia. Umbali karibu wa km 2,000. Ya sasa inaishia Makutupora, haifiki hata km 400.

5. Hospitali - ilijengwa Muhimbili, Rufaa Mbeya, Dodoma, Mloganzila. Safari hii hakuna hata moja ya rufaa iliyojengwa. Hospitali za mikoa zilijengwa kila mkoa, safari hii zinapandishwa madaraja lakini siyo kujengwa

6. Elimu - zilijengwa sekondari, vyuo vikuu UDSM, Sokoine, Mbeya, UDOM, n.k. Safari hii hakuna kipya hata kimoja

7. Vituo vya utafiti - zilijengwa research centres za kilimo, ufugaji, uvuvi, magonjwa ya binadamu, n.k. Awamu hii hakuna hata kimoja kilichojengwa.

Serikali awamu hii, kama awamu ziluzopita, inajitahidi kutimiza wajibu wake LAKINI kusema inafanya cha pekee ni UWONGO.
 
Serikali kuhamia Dodoma!
 
Kuomba dua ni jambo moja na dua kukubaliwa ni jambo lingne

Kama una makandokando ya siri, ya kuumiza watu, kufanya hila, ghilba, hizo dua zinaweza zisikufae
 
Nilazima waseme, kwani mufti anahudumiwa na serikali kwa kila kitu, nyumba, ulinzi, mishahara ya warumushi wa Ofsini ,maji, umeme, mafuta mavazi, chakula, na mengineyo hawezi kuenda kinyume na anayemlipia , waswahili wanamsemo '' anayemlipa mpiga zumari ndiye anayechagua wimbo.
 
Hayo hayakuwa maombi ila alikuwa anasifiwa kwa vigezo vyao.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom