Kasi ya kufungua matawi CHADEMA iongezwe

Kasi ya kufungua matawi CHADEMA iongezwe

Wa Busiya

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
326
Reaction score
67
Nimesoma taarifa kutoka Tabora jinsi Zitto alivyofungua matawi 19 katika kata 19 za tabaora mjini nikafurahi sana. Naamini pia mtu yeyote anayeelewa maana ya neno 'DEMEOKRASI' atafurahia ukuaji huu wa demokrasia nchini mwetu.

Maana yake ni kwamba kama CDM kitakuwa na kujitanua hadi vijijini na hasa ngazi ya kijiji na mtaa au shina, ushindani utakuwa wa haki na unaompa nafasi mpiga kura kufanya maamuzi bila hofu. Hii inatokana na kweli kwamba hapo awali CCM kilidhibiti maeneo hasa ya vijijini kiasi cha kuwaamuru wananchi kukipigia kura.

Mf. wazee na watu wengine wasiojua kusoma huelekezwa kwa mtu ambaye atawasaidia na kuwaelekeza namna na mtu gani wampigie kura. Haya hufanyika hadharani na sisi watu wa vijijini huyaona tusijue la kufanya maana vinginevyo utakutana na mkono wa jeshi la ulinzi la jadi kwa ukarabati.

Kwa hiyo CDM zidisheni juhudi ili taifa hili lifike mahali ambapo hapatakuwa na fikra zilizopo sasa hivi za wanasiasa hasa wa vyama vinavyotawala kutetea maslahi yao na vyama vyao badala ya maslahi ya taifa. Tunataka tuwe na vyama kama ilivyo nchi nyingine zisizohitaji mtu kuhamia chama kingine bali mtu kupembua sera za mgombea yeyote ili kama anafaa ampigie huyo huku akiendelea kuwa mwanachama kwenye chama chake.

Ifike mahali tuacha ujinga wa kushabikia tu hata kama unaumizwa na hupati faida yoyote kutakana na chama unachoshabikia. Kwa hatua ambayo CDM kimefikia, ni vizuri wananchi wengi wakjiunga ili kiwe na wanachama wengi kama na au zaidi ya CCM ili kuleta ushindani wa kweli kidemokrasia.

HEBU FIKIRIA KAMA TIMU ZOTE ZINGEKUWA TOTO AFRICAN halafu kuwe na timu moja tu kubwa ambayo inajihakikishia ushindi siku zote? Lakini kama kuna timu kubwa maarufu kama Simba na Yanga

zinapokutana
hata mashabiki mnajisikia vizuri baada ya kupata ushindi. HONGERENI CHADEMA KWA KUTAFUTA KULETA DEMOKRASIA YA KWELI NCHINI MWETU.
 
Umenena vema mkuu, ushindani wa kweli, uleta maendeleo, siku hizi yapo mambo mengi yalikuwa yanaendeshwa kiolela na bila mwanchi kujuwa ila kuwepo kwa vyama vya upinzani na hasa hasa CDM wameleta mapinduzi makubwa nchini, watu wanajuwa na kufuatilia yanayotokea.
 
Back
Top Bottom