spika
JF-Expert Member
- Dec 7, 2014
- 458
- 426
By Mwananchi
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema sababu za washirika wa maendeleo kutotoa fedha ni nyingi na kwamba yako masharti waliyotoa ambayo Serikali haiyakubali.
Amesema yapo masharti ambayo Serikali haikubaliani nayo akitoa mfano wa waliotaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ijiondoe kuiendesha aje mtu binafsi na kusema imekataa kwa masilahi ya Taifa. Mbali ya sharti hilo, Dk Mpango alisema masharti mengine ni kinyume cha mila na desturi zetu.
Tatizo jingine alisema ni kitendo cha wafadhili hao kutaka kufadhili miradi moja kwa moja akisema hiyo itafanya wachague baadhi ya miradi jambo ambalo alisema si sahihi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Bunge ya Bajeti kwa kipindi cha Januari 2016 hadi Januari mwaka huu, iliyosomwa bungeni jana na mwenyekiti wake, Josephat Kandege mwaka wa fedha 2016/17 washirika wa maendeleo waliahidi kutoa Sh3,600.8 bilioni lakini takwimu zinaonyesha kuwa hadi kufikia Septemba mwaka jana, kiasi kilichopokewa ni Sh285 bilioni sawa na asilimia 16 ya lengo la robo mwaka.
Maelezo ya Waziri Mpango aliyotoa bungeni jana, yalikuja baada ya Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia (CUF), ambaye kusema kwamba huenda Tanzania imenyimwa misaada na wafadhili kutokana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 huko Zanzibar.
Mtulia alisisitiza kuwa Zanzibar haijakaa vizuri ndiyo maana Tanzania haikupata misaada ya kibajeti maelezo ambayo yalijibiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba ambaye alisema Zanzibar ni ya Umoja wa Kitaifa na inajumuisha vyama vingine vinne.
Suala la misaada ya maendeleo kutoendana na bajeti limekuwa likijirudia mwaka hadi mwaka na hata pale ambako hakuna matukio makubwa kama hilo la uchaguzi, bado kilio cha kwamba kile kilichoahidiwa hakikupatikana chote kimeendelea kusikika.
Mathalani, katika hotuba ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2002/03 iliyosomwa bungeni na Waziri wa Fedha wakati huo, Basil Mramba ilisema, “Ingawa baadhi ya fedha za misaada na mikopo nafuu ya wahisani hazikufika kama zilivyoahidiwa, bajeti ya Serikali haikuathirika. Kwa kiwango fulani hali hii ya kutotetereka kwa bajeti kutokana na kuchelewa kupatikana kwa fedha za misaada, ni kipimo kizuri cha uwezo wetu wa kujitegemea.”
Hata katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2010/11, iliyosomwa na Waziri wa Fedha wakati huo, Mustafa Mkulo, wizara ilipanga kukusanya mapato kutokana na misaada na mikopo kutoka nje yenye thamani ya Sh 3,274.6bilioni na kufikia Juni, 2011 misaada na mikopo iliyopokewa ilikuwa Sh2,701 bilioni sawa na asilimia 82 ya makadirio ya mwaka.
Tunadhani hiki ndicho ambacho kimeendelea kujitokeza mara kwa mara hivyo wito wetu kwa Serikali ni kupambana kujitoa katika utegemezi kwa kuendelea na jitihada zilizoanza za kukusanya mapato, kubuni vyanzo vipya vya mapato na kujielekeza katika nidhamu ya matumizi.
Tukifanya hivyo, tutakuwa na nafasi nzuri ya kufanya tathmini ya misaada ambayo wahisani wanataka kutupatia ambayo baadhi imekuwa na masharti siyo tu magumu, bali ambayo yanadhalilisha utamaduni wetu.
Tunawashajiisha Watanzania kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza uzalishaji ambao utachangia kipato ambacho ndani yake Serikali itapata kodi yake na kuiwezesha kujiendesha ili hatimaye ipunguze kama siyo kuachana kabisa na utegemezi wa wahisani katika bajeti yake.
Inawezekana kila mtu akitimiza wajibu wake.
Maswali ninayojiuliza:
Rais Kikwete aliwahi kulipinga hadharani swala la ushoga, je ni tofauti gani iliyojitokeza sasa?
Hivi haiwezekani kwamba serikali yetu ndio inayojaribu kuwawekea masharti wahisani?, maana tumeoshaona na kusikia mengi awamu hii
Kama serikali haina uwezo wa kuendesha bajeti kwa mapato ya ndani nini hatma ya nchi yetu kama wataendelea kutunishiana misuli na hao wenye pesa zao?