Kashfa ya Ufisadi Bandari ya Dar

Tatizo la nchi hii ni kwamba kila sehemu kuna mkono wa mafisadi.

Tukubali au tukatae huo ndo ukweli. Kuna watu walishageuza sehemu hizo kama biashara zao binafsi! Napenda kumpongeza Mhe. Mwakyembe kwa juhudi anazofanya kusafisha wizara hiyo. Kazi hiyo inasitahili pongezi za dhati ingawa tunajua kuna upinzani mkubwa kutoka nje na ndani ya Mashirika/Kampuni hizo.
 
Hence proved,Tanzania would never become a strong nation under ccm!
 
Teh teh teh teh teh eeeee uuuuwiiiii, yaani Tanzania zaidi ya kichekesho.
 
Nadhani kuna haja ya kujua ni kwa kiasi gani bandari inaweza changia uchumi wa nchi hii.
 
lakini ziko wapi bandari za mtwara na tanga kama bandari ya dar es salaam imezidiwa?au ndio zitolewa kama offer kwa wawekezaji.
 
mimi nimetoa magari bandarini ndani ya siku mbili tu,kwa kweli bandari hivi sasa wanajitahidi sana
 
Hebu tujaribu kufikiri nje ya box.

Kwanini tusiendeleze bandari ya Tanga? umbali toka Tanga ni Km 360 tu mpaka Dar.

Ukiangalia gharama za meli kupaki kusubiri na storage cost za bandarini it worths kupeleka mzigo Tanga.

Tatizo wote tumejikita ndani ya BOX la Dar esalaam tu.
 
Liwalo na Liwe mwenye uwezo wake wa kukwiba kwiba nji hii shamba la bibi
 
Nadhani kuna haja ya kujua ni kwa kiasi gani bandari inaweza changia uchumi wa nchi hii.

Mkuu, Mh.Dr akijifunga kibwebwe akamshauri JK kwamba Wakurugezi karibu wote pale Wizarani wahamishiwe Wizara nyingine kabisa; bila kufanya hivyo watamkwamisha TU. Mkuu si rahisi Wizara hii ikawa inakuwa na matatizo miaka nenda rudi alafu mtu ukategemea miujiza kutoka kwa jamaa hao hao waliopewa dhamana ya kuiongoza, tunasahau kwamba Waziri ni Kiongozi wa muda kwenye Wizara lakini Wakurugenzi/watendaji niwa kudumu mpaka wastaafu, na mtu akikaa kwenye nafasi moja muda mrefu anajisahau sana na kufikili Wizara ni mali yake au ya ukoo.

Wakurugenzi wakuu wanao teuliwa kuongoza Agencies za Wizara hiyo wanakuwa vetted na Wizara yenyewe wakati mwingine watu wenye uwezo wanatupiliwa mbali badala yake wanateuliwa maswahiba wao tu - mifano tunayo; nikiona wanalalamika kwamba mashirika yao tanzu mambo hayaendi vizuri huwa nawashangaa sana.

Mkuu Bandari yetu ni HUB kwa nchi zinazo izunguka Tanzania, kwa kujibu swali lako bandari hii ina uwezo mkubwa kuchangia mapato makubwa kuliko sector nyingine hapa nchini, we sema tatizo letu ni ukosefu wa ubunifu na kutojali - wenzetu Wakenya ni mahili sana katika nyanja za bihashara, uwezi kuona wana-mix bihashara na starehe, alafu wana mbinu nyingi ya kushawishi wateja na kujitangaza, kwao mteja ni mfalme hiwe Bandarini, Mahotelini na katika nyanja za kitalii -sisi hilo hatuna! Hutujuhi jinsi ya ku-handle wateja, tunawajibu ovyo ovyo tu, njoo kesho njoo kesho-pale longroom ndio usiseme yaani hata mantiki ya kutumia komputa pale ni kama utani vile, wizi uliyo kubuhu pale bandarini siyo kwa magari tu hata makontena yanapotea kabisa au unakuta yamebomolewa na mali imekwisha chukuliwa na wezi - yaani wizi Tanzania umekithili.

Siku moja niliwahi kusafiri na Wacongo wanakwenda Zambia, mambo walio nieleza kuhusu Bandari yetu na usafirishaji wa mizigo kutumia TRAIN ulinifanya nilishikwe aibu sana kuhusu Taifa letu. Mwisho walisema kwa nini Bandari na TRAIN msiwape WAZUNGU au Wachina mkawapa mshahara mkubwa wakaendesha/kuongoza mashirika hayo kwa niaba ya Serikali yenu!!!! We sikiliza wageni mapendekezo wanayo toa - unafikili mimi kama Mtanzania nilijisikiaje?
 
Mitanzania bwana kila mtu anawaza mambo yake binafsi.kuna wakati huwa nawaza MUNGU kama anaipenda nchi hii awachukue watu wote 45 years of age and above aende nao mbinguni ,waliobaki wakae chini wakubaliane namna ya kuendesha Nchi.MIJITU NI MIFISADI MPAKA INAKERA.
 
Nilishasema kwenye thread nyingine na naomba TAKUKURU wanisikie. Funga Suggestion Box kubwa hapo bandarini la kuingiza majina ya wanaodai rushwa halafu funguo kaeni nayo nyie wenyewe mkija kila friday mnafungua box mnasoma jina mnaondoka na mtu anaenda kujieleza mbele ya safari, uchunguzi unafanyika kama ahusiki anaachwa.
 
Nadhani kuna haja ya kujua ni kwa kiasi gani bandari inaweza changia uchumi wa nchi hii.

Nasikia nchi kama Singapore wenyewe hawana madini, hawana kilimo, hawana mafuta hawana chochote wanaishi kutegemea bandari yao tu! sisi hapa tunazungukwa na landlocked countries bado tuna mbwela mbwela watu jirani zetu wa Rwanda na Uganda wanatushangaa sana wanalaani sana wana wish mungu angewaweka wao hapa tulipo sisi!!
 

Pamoja na jitihada za Mwakyembe bila kumuondoa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Omar Chambo I assure you nothing will ever be done! jamaa ni tatizo kubwa!
 
Pamoja na jitihada za Mwakyembe bila kumuondoa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Omar Chambo I assure you nothing will ever be done! jamaa ni tatizo kubwa!

Tupe info zaidi tujue jamaa anahusika vipi kukwamisha jitihada za waziri.
 
sijui kama kumfukuza mkurugenzi kutasaidia!mie nadhani mwakyembe anatakiwa kuwafukuza watu wengi kweli pale, kama kufukuza haiwezekani awahamishie nikoani huko kusiko na bandari kabisa kama dodoma,singida, tabora,shy etc wakakalie madawati tu kuliko kukwamisha watu walio bize huku wakilamba mishahara na posho nono!
 
Bidhaa nyingi zilizopaswa kupitishwa bandari ya dar hata mwagizaji yuko dar sasa wanatumia bandari ya mombasa na pale hakuna bureaucracy unalipa na kuondoka na ulichoagiza kikiwa safe, on time. No wonder wanajenga international airport pale mpakani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…