Kashfa ya Kagoda yatibua siku ya sheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa ya Kagoda yatibua siku ya sheria

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Feb 4, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete akiangalia kalenda aliyozawadiwa na Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande baada ya kuhutubia Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini jijini Dar es salaam jana.(PICHA:IKULU)


  Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili (TLS) Tawi la Arusha, Duncan Oola, amehoji iwapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ameshindwa kumjua mmiliki wa Kampuni ya Kagoda, inayotuhumiwa kukwapua zaidi ya Sh. bilioni 40 katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) iliyoko katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
  Oola alihoji hayo mjini hapa, mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Aisha Nyerere, majaji, mahakimu, mawakili na watumishi wa mahakama na viongozi wa dini katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini.
  Mada ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ilikuwa ni “Adhabu mbadala katika kesi za jinai-faida zake katika jamii.”
  “Dhana ya ufisadi iliyoongelewa kwa nguvu nyingi tangu 2005/2006 harakati zilizoibua wizi mkubwa wa EPA, je, ndugu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ni kweli mmeshindwa kumjua Kagoda kampuni iliyoiba zaidi ya Sh. bilioni 40 kati ya Sh. bilioni 133 zinazosemekana ziliibwa?
  “Je zisingesaidia kulipa madaktari leo?....Lakini unaweza kukuta mwizi wa kuku au vitu vidogo kama hivyo, anachukuliwa hatua haraka na kufungwa jela,” alisema.
  Akizungumzia makosa yanayostahili adhabu mbadala, Oola alisema yapo makosa ambayo ni madogo na ambayo kwa namna moja au nyingine mkosaji akipewa adhabu mbadala anaweza akaelimika na kufikia kubadilika kitabia na katika hali hiyo ikawa ni kwa faida ya jamii na yeye binafsi.
  Alisema tofauti na vifungo magerezani, halmashauri za wilaya, miji na manispaa zinaweza kuanzisha vitengo vya kusimamia huduma za jamii ambapo mtu akiadhibiwa na mahakama atazimika kwenda kupangiwa kazi na kitengo kinachohusika cha halmashauri.
  Akizungumzia sababu za kuwa na adhabu mbadala, Jaji Nyerere alisema ni bayana kuwa magereza 126 yaliyopo nchini yamekuwa na mrundikano wa wafaungwa na mahabusu.
  Kwa Mkoa wa Arusha, takwimu zinaonyesha wafungwa waliopata fursa ya kutumikia adhabu zao chini ya sheria hiyo kutoka mahakama mbalimbali kuwa ni 153 tu, wanaume wakiwa ni 119 na wanawake wakiwa ni 34.  JK AKUBALI ADHABU MBADALA

  Rais Jakaya Kikwete ameunga mkono matumizi ya mfumo wa adhabu mbadala kwa wahalifu wa makosa madogo, kwamba badala ya kufungwa jela wahukumiwe kufanya kazi za kijamii badala ya kufungwa jela.
  Kikwete alisema matumizi ya adhabu mbadala, mbali na kuweza kumrekebisha mhalifu wa makosa ya aina hiyo, yatasaidia pia kupunguza mrundikano wa wafungwa na kuondoa msongamano uliokithiri magerezani ambao alisema umekuwa ukimsumbua.


  Aliyasema hayo jana wakati akitoa salamu katika maadhimisho ya “Siku ya Sheria nchini kwa mwaka huu”, jijini Dar es Salaam, yaliyoongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman.


  Hata hivyo, Rais Kikwete alisema wanakabiliwa na changamoto ya kujipanga namna ya kufanya kazi za kijamii ili badala ya kazi hizo kuwa za kukwaza, ziwe za kumsaidia mhalifu kujirekebisha kimwenendo na kitabia na kuwa raia mwema katika maisha yake ya kila siku katika jamii.
  Alisema kuna kazi kubwa ya kuelimisha jamii kuhusu adhabu mbadala na kwa hiyo, akataka wakuu wa mikoa na wilaya kuhusishwa kikamilifu katika elimu juu ya utekelezaji wa adhabu hiyo.
  Awali, Jaji Chande alisema adhabu ya kifungo gerezani, kinachangia matumizi ya gharama yasiyokuwa na tija na kwamba, hakirekibishi bali kinakomaza.
  Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Francis Stola, alisema mrundikano wa wafungwa na mahabusu magerezani limekuwa ni tatizo kubwa linalosababisha uvunjifu wa sheria za msingi, maradhi ya kuambukiza na ukosefu wa huduma nyingine, hivyo, akashauri matumizi ya adhabu mbadala ili kupunguza tatizo hilo.
  Naye Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, alisema adhabu zote mbili ni muhimu kulingana na aina ya makosa, hivyo akapendekeza zote ziendelee kutumika, hasa kwa vile haujapatikana mwafaka kati ya makundi yanayovutana kuhusu ama kuruhusiwa kwa matumizi ya adhabu mbadala au la.

  MGAWO WA FEDHA KWA MAHAKAMA
  Rais Kikwete pia alisema tatizo la kifedha lililokuwa likiikabili serikali, lilisababishwa na ulipaji wa malimbikizo ya madeni ya zamani, ambayo alisema muda wa kuyalipa ulifika.
  Hata hivyo, alisema kiasi kikubwa cha madeni hayo kimekwisha kulipwa na kwamba limebaki deni la kati ya Sh. bilioni 40 au Sh. bilioni 30.
  Alisema wakati wowote kuanzia sasa mgawo wa fedha kwa Mahakama ya Tanzania, utarudi kama kawaida.
  Alisema katika kutekeleza hilo, serikali itabana bajeti za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mihimili mingine ya dola kuhakikisha Mahakama ya Tanzania inatengewa bajeti ya kutosha ili kuiwezesha kuendesha shughuli zake bila vikwazo.
  Pia aliahidi kulipatia ufumbuzi tatizo la upungufu wa majaji na mahakimu kwa kurekebisha urasimu uliopo serikalini katika uteuzi wao.
  Mapema Jaji Chande alisema ufanisi umekuwa ukikosekana katika utendaji wa Mahakama ya Tanzania kutokana na bajeti finyu inayotengwa na isiyokuwa na uhakika.
  Alisema kwa mfano, katika mwaka huu wa fedha, waliomba Sh. bilioni 13.7, lakini zilizopokelewa ni Sh. bilioni 8.5 na kwamba, jambo hilo limekuwa likijirudia mwaka hadi mwaka, hali ambayo imekuwa ikisababisha washindwe kuendesha mahakama.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #2
  Feb 4, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kagoda unknown to this momemt?!!! Muulize Msemakweli
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Si kagoda hata meremeta,tangold na dowans hawawajui wamiliki wake!!!hata...ingawa wanatumiana email tu
   
Loading...