Kashfa ya ESCROW yakwamisha ujenzi wa Maabara

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,223
1,673
Kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow, imesababisha baadhi ya vyama vya siasa mkoani hapa kuwahamasisha wananchi kuacha kuchangia miradi ya maendeleo na kukwamisha ujenzi za maabara kutokamilika.

Akizungumza na NIPASHE mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Festo Kang'ombe, alisema kuwa sakata hilo limekuwa kikwazo kikubwa cha kufanikisha ujenzi wa maabara kama walivyopanga kutokana na kuwapo kwa uitikiwaji mdogo wananchi.

Kang'ombe alisema katika kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa na Kashifa ya Escrow, baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakishawishi wananchi kutochangia jenzi za maabara kwa madai kuwa viongozi wanakula fedha za walipa kodi , mabilioni ya fedha, fedha ambazo zingeweza kujenga maabara hizo na hivyo wananchi kugoma kutoa mchango wowote.

"Ujenzi wa maabara katika shule zote za sekondari ni agizo la Rais, na halmashauli hazikupewa fedha zozote kutoka serikali kuu ili kukamilisha ujenzi huu,tunajisimamia wenyewe kwa kushirikiana na wananchi, ili kukamilisha agizo hili la Mheshimiwa Rais," alisema Kang'ombe na kuongeza kuwa.

"kuna baadhi ya fedha za miradi ya maendeleo, Sh. milioni 133 tulizibadirishia matumizi na kuzipeleka kwenye jenzi hizi za maabara, lakini nazo hazitoshi, huku mwitikiao nao kwa jamii bado ni mdogo kutokana wanasiasa kulivalianjuga na kukwamisha utekelezaji huu usikamilike kwawakati."

Kang'ombe alifafanua kuwa, maabara zinazaoendelea kujengwa katika manispaa ya Shinyanga ni 43, na hakuna hata moja iliyokamilika, na kabla ya zoezi la ujenzi huo wa maabara shule zilizokuwa na maabara tangia awali ni saba tu, kati ya shule za sekondari 10 za serikali zilizopo mjini humo.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Annarose Nyamubi, alilaani baadhi ya wanasiasa kuchanganya masuala ya maendeleo na siasa, vitendo ambavyo vimekuwa vikikwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.

"Kila mtu anajua umuhimu wa maabara na siku zote ninasisitiza juu ya suala hili,shule bila kuwa na maabara bado haijakamilika, naiomba jamii ibadilike ipuuze maneno ya wanasiasa na ione umuhimu wa kuchangia elimu ili kuwawezesha watoto wasome katika mazingira mazuri ya kujifunza kwa vitendo" alisema Nyamubi.


CHANZO:
NIPASHE
 
Maabara Zijengwe Cha Ajabu Yanakuwa Magofu Ya Kucheza Komborea
Serikali Haitanunua Vifaa Vya Maabara
Ahsante JIGO
 
Hata mimi ningegoma kuchangia. Sio haki kidogo. Mhe. Ndugai ametumia 13m first class ticket pesa ya walipakodi. Serikali ina matumizi mabovu sana matokeo yake ndio haya.
 
Back
Top Bottom