Kashfa ya Chenge yamtoa jasho Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa ya Chenge yamtoa jasho Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mutu, Apr 24, 2010.

 1. M

  Mutu JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Na Muhibu Said
  23rd April 2010
  Mbunge ambana aeleze chenji ya rada
  Ni mabilioni yanayotakiwa kurejeshwa
  Spika Sitta aingilia kati kuokoa jahazi


  Mjadala unaohusisha kashfa ya ufisadi wa rada iliyonunuliwa kwa bei ya juu zaidi kinyume na bei yake halisi, uliibuka tena bungeni, baada ya Kambi ya Upinzani kuhoji sababu za msingi za Serikali ya Uingereza kuamua kuirudishia Tanzania ‘chenji’ katika ununuzi wa rada hiyo, wakati ipo Sheria ya Manunuzi ya Umma inayoiongoza serikali namna bora ya kufanya manunuzi yake.

  Mjadala huo uliibuliwa tena na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed, katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

  Katika swali lake la msingi kwa Waziri Mkuu, Hamad, ambaye ni Mbunge wa Wawi (CUF), alisema baada ya kuibuka kwa kashfa kwenye ununuzi wa rada hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alikaririwa akisema serikali ya Tanzania imerudishiwa ‘chenji’ na serikali ya Uingereza baada ya kuonekana kwamba manunuzi yale hayakufanyika kwa bei halisi.

  “Sasa nasema kwa nini serikali mpaka inafikia pahala inarudishiwa chenji wakati ipo Sheria ya Manunuzi ya Umma inatuongoza namna bora ya kufanya manunuzi ya serikali kama vile, ambavyo tulivyofanya kwenye Richmond, hivyo hivyo, na kila pahala manunuzi yanaelezwa vizuri katika Sheria ya Manunuzi ya Umma, lakini bado serikali inanunua vitu kwa bei ya juu zaidi mpaka inafikia pahala inarudishiwa chenji. Ni sababu zipi za msingi?” alihoji Hamad.

  Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema hajui kama kuna suala la kurudishiwa chenji katika ununuzi wa rada hiyo na kumshauri Hamad kulenga jambo mahsusi katika swali lake.

  “Mheshimiwa Spika, labda nikiri kwamba, mimi silijui hilo la kurudishiwa chenji. Lakini kama serikali inaendelea kuheshimu sana utaratibu wa kisheria uliopo, na mara zote tumeutumia kwa kadiri tulivyoweza. Lakini kama ulikuwa na jambo mahsusi, mimi nafikiri kwamba ningefurahi sana kupata jambo mahsusi katika swali lako,” alisema Pinda. Majibu hayo ya Pinda yalimfanya Hamad kusimama na kuuliza swali la nyongeza ambapo alimweleza Waziri Mkuu kwamba aliyesema Tanzania imerudishiwa chenji ni Waziri Membe, ambaye ni waziri wa serikali ambayo Pinda ni msimamizi wake.

  “Lakini labda niseme tu kwamba, juzi katika kipindi kilichopita, tulipitisha sheria hapa ya kuongeza nyongeza ya matumizi ya fedha Sh. trilioni 1.7 kwa ajili ya kufidia watu waliopata matatizo katika kilimo na kutokana na matatizo ya uchumi. Katika fedha hizo, mpaka sasa ni kama Sh. bilioni 2.3 zilizotumika.

  Lakini bado vile vile serikali imekuja bungeni kuomba Sh. bilioni 1.7, lakini fedha halisi zilizotumika sizo zile ambazo zimeombwa na Bunge. Ni dhahiri kwamba kuna chenji nyingine imebaki, ambayo Bunge hili halikuweza kuidhinisha.

  Lakini kwa nini utaratibu huu wa makisio halisi ya serikali ya kununua au kutoa fedha kulipa hayawi halisi kila siku, Mheshimiwa Waziri Mkuu?” alihoji Hamad. Hata hivyo, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, alisimama na kuzuia swali hilo kujibiwa na Waziri Mkuu kwa maelezo kwamba, lilikuwa ni jipya na sio la msingi lililoulizwa na Hamad, ambalo halikupaswa kuulizwa wakati huo kwa vile kufanya hivyo ni kukiuka kanuni za Bunge.

  “Kwa mujibu wa nyongeza ya sita ya kanuni zetu, swali linalofuata lazima liwe la nyongeza. Lisiwe jipya kabisa. Sasa suala la fedha tuliyopitisha ya kulipia athari za kiuchumi, halihusiani hata kidogo na chenji. Kwa hiyo tunaendelea waheshimiwa,” alisema Spika Sitta na kumruhusu Mbunge wa Dimani, Hafidh Ali Tahir (CCM) kumuuliza Waziri Mkuu swali jipya.

  Mjadala kuhusu rada hiyo umeibuka upya bungeni ikiwa imepita miezi michache baada ya kampuni ya kutengeneza zana za kijeshi ya Uingereza, BAE Systems, kukubali kulipa faini ya Dola za Marekani milioni 45 ili kumaliza kesi mbalimbali zilizokuwa inaikabili kutokana na udanganyifu wa kuuza zana za kijeshi kwa nchi kadhaa duniani, Tanzania ikiwamo.

  Suala hilo bado linamweka njia panda aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge, kutokana na kuhusishwa kwake kwenye kashfa hiyo kurejeshwa mikononi mwa serikali.

  BAE Systems imeamua kulipa kiasi hicho cha fedha ili kumaliza kesi zilizofunguliwa dhidi yake na Ofisi ya Makosa Makubwa ya Jinai ya Uingereza (SFO) pamoja na Wizara ya Sheria ya Marekani.

  Katika fedha hizo, Wizara ya Sheria ya Marekani, italipwa Dola milioni 400, wakati SFO watalipwa Dola milioni 47.

  Fedha za SFO zitakwenda kwa nchi, ambazo zilikuwa zikiendesha uchunguzi kuhusu biashara zilizofanywa na BAE System, ikiwamo Tanzania, Jamhuri ya Czech, Romania na Afrika Kusini.

  Wakati BAE wanakiri kuboronga mambo kwa kuwasilisha taarifa za uongo kwa serikali ya Marekani kuhusu biashara ya zana za kijeshi na jinsi ya kuepukana na rushwa, kwa Tanzania inakiri kushindwa kuweka kumbukumbu sahihi kuhusu biashara ya kuiuzia Tanzania rada mwaka 1999. BAE Systems inakiri kwamba, kwa kuboronga mambo katika uuzaji wa rada kwa Tanzania, inaridhia kulipa fidia ya Pauni milioni 30, sehemu ya kiasi hicho kikiwa ni msaada kwa ajili ya Tanzania.

  Wakati Pinda anadai kutolijiua suala la chenji ya rada, Aprili 12, mwaka huu, Waziri Membe, alikaririwa akisema kuwa serikali itatuma ujumbe wa wataalamu na maofisa waandamizi wakati wowote kwenda London, Uingereza kujadiliana na Uingereza kuhusiana na taratibu za Tanzania kurejeshewa Dola za Marekani milioni 45 (Sh. bilioni 62).

  Membe alisema kuwa fedha hizo ni sehemu ya faini iliyolipwa na BAE Systems baada ya kampuni hiyo kukiri kuhusika katika rushwa wakati wa mchakato wa kuiuzia Tanzania rada mwaka 1999.

  Membe alisema ujumbe huo utawajumuisha maofisa kutoka wizara yake, Takukuru, na Hazina.

  Hatua hiyo imefuatia taarifa kuwa serikali ya Uingereza inataka fedha zitakazorejeshwa zitolewe kwa mashirika ya kujitolea yaliyoko nchini.

  Rada hiyo ilinunuliwa kwa bei ya juu ya Dola milioni 40 (Sh. bilioni 54), hatua iliyopingwa na wengi pamoja na taasisi mbalimbali ikiwemo Benki ya Dunia (WB).


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wapiganaji hatuna mtu tena! Huyu 6 tayari kesha rududi kundini.
   
 3. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2010
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 518
  Trophy Points: 280
  Watanzania tuna akili lakini hatuzitumii, tuna macho lakini hatuoni, tuna masikio lakini hatusikii, tuna pua lakini hatuepuki harufu mbaya, tuna ngozi lakini hatuhisi hata kama kuna moto wa kuunguza!
  TUWATOSE MAFISADI NA VIBARAKA WAO, HAKUNA TUTAKACHOPOTEZA!
   
 4. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,993
  Trophy Points: 280
  Kama kweli Six ana nia nzuri basi asingethubutu kutuona wajinga na kudai eti swali la pili ni jipya na wala si la nyongeza.....Wameulizwa ni kwanini tunarudishiwa chenji,hapo ni issue ya umakini moja kwa moja,umakini kwenye utendaji wa serikali,swali la pili ni wazi kabisa kwamba ni la nyongeza,ama kweli kuishi kwingi ni kuona mengi...Duh!
  Hao wanaojiita wapiganaji kama wakituingiza mjini basi wajue they will one day pay for it!
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Wasiomjua Sitta ndio wanadhani ni mpambanaji dhidi ya mafisadi; huyu kama wanaCCM wenzie anatafuta ULAJI TU!!
   
 6. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #6
  Apr 25, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kupigana na fisadi ukiwa na njaa ni sawa na jaribio la kuvua samaki bila chambo MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
Loading...