GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,043
- 119,616
Akizungumza kwa masikitiko makubwa Mwenyekiti wa Klabu ya Zanaco FC ya nchini Zambia Bwana Edward Materu amesema kuwa wanafikiria kuishtaki Klabu ya Yanga CAF na FIFA kwa kitendo chake ambacho amekiita ni cha Kimauaji kabisa cha kuwapulizia dawa ( Watu wa mpira tunaiita 4-4-2 ) katika Chumba cha kubadilishia Nguo cha Timu yake.
Bwana Edward Materu akaenda mbele na kusema kuwa walipoingia tu katika hicho Chumba wakakuta hewa ni nzito sana kiasi kwamba baadhi yao walipiga Chafya nyingi ndipo wakaamua kumuita Daktari wao ambapo alifanya experiment yake ya Kitaalam kabisa na akagundua kuwa kila Chumba kilikuwa kina Kemikali ya kuwadhoofisha Wachezaji hali iliyowafanya wawalazimishe Wachezaji wao wa Zanaco FC waende kuvalia ndani ya Basi lao.
Ikumbukwe hii ni mara ya nne ( 4 ) Klabu ya Yanga inalaumiwa na Wapinzani wao kwa kuwafanyia hiki Kitendo Vyumbani na kama haitoshi hata Klabu kadhaa za Ligi Kuu hapa Tanzania VPL na zenyewe zimekuwa zikilalamika sana hii tabia ya Yanga ila hakuna kinachofanyika kutoka kwa wenye Mamlaka na Soka.
Inasemekana kuwa mechi nyingi ambazo Yanga imekuwa ikishinda magoli mengi sababu kubwa ni matumizi ya hii dawa ya Kemikali ambayo hupenda kuipulizia katika Vyumba vya Wachezaji wa Timu pinzani ili kuwadhoofisha Wachezaji wao.
Kwa wale mtakaotaka mzigo kamili wa huyo Mwenyekiti wa Klabu ya Zanaco FC sikilizeni au angalieni marudio leo Saa 9 alasiri ya Kipindi cha Sports Bar cha Clouds tv ambapo Bwana Edward Materu alitema cheche zote alipokuwa akihojiwa na Mtangazaji wa Michezo wa Clouds tv Jacob Mbuya.
Yanga FC badilikeni kwani mnatutia aibu mno Watanzania na endapo hawa Zanaco FC wakiamua kwenda huko CAF na FIFA basi mtakuwa hatarini kufurumushwa kabisa Mashindanoni kwa bahati nzuri kwa mujibu wa huyo Mwenyeiti Edward Materu amesema kuwa ushahidi wote Daktari wao anao na tayari wameshaanza taratibu za awali za kuashitaki Yanga.
Nawasilisha.