Kashfa nzito Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa nzito Polisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanza Madaso, Aug 9, 2009.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kashfa nzito Polisi
  • DCI Manumba: Aahidi polisi watakaobainika kukiona

  na Kulwa Karedia


  [​IMG]
  JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limekumbwa na kashfa nzito, baada ya askari wake kumkamata mfanyabiashara, George Mwaipungu na kumpora sh milioni 60.
  Tukio hilo la aina yake lilitokea Novemba 11 mwaka jana katika eneo la Kiluvya, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, baada ya polisi kuvamia na kumkamata mfanyabiashara huyo mwenye kumiliki maduka kadhaa ya kuuza magari nchini Zambia.
  Kwa mujibu wa barua ya mfanyabiashara huyo kutoka Gereza Kuu la Mahabusu Segerea, yenye kumb 78/DAR/5/V/300 ya Juni 20, 2009 kwenda kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, polisi wanatuhumiwa kumfungulia kesi ya mauaji.
  "Walikuja askari ambao walijitambulisha kuwa wanatoka Task Force, walinikamata kisha kuchukua kila kitu nilichokutwa nacho, walichukua fedha, paspoti za kusafiria, simu za mkononi na fedha za Zambia Kwacha 6,700," ilisema sehemu ya barua hiyo.
  Barua hiyo ambayo imesainiwa na Mkuu wa Gereza hilo, ACP G. S Nyamwangi na nakala zake kusambazwa Ofisi ya Rais Ikulu, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Waziri wa Sheria na Katiba, Wizara ya Mambo ya Ndani na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, inataka polisi wote waliohusika katika tukio hilo wakamatwe.
  Kwa mujibu wa barua hiyo, baada ya mfanyabiashara huyo kukamatwa, alipigwa na kusababishiwa maumivu makali na ni ukiukwaji wa haki za binadamu.
  "Polisi hawa baada ya kunipiga, walianza kunihoji ili niwaambie gari aina ya Mercedes Benz iliyoibwa na watu wasiojulikana imefichwa wapi, walinikuta na leseni ya nchi za Maziwa Makuu, wakasema lazima nitakuwa naelewa vizuri mtandao wa wizi wa magari… jambo ambalo halina ukweli wowote," ilisema barua hiyo.
  Barua hiyo iliendelea kusomeka kuwa baada ya kukamatwa na kusachiwa, mfanyabiashara huyo alichukuliwa dola 29,860 kwenye koti lake, ambazo hadi sasa polisi wamegoma kuzirudisha.
  "Baada ya kunitesa kwa kila aina ya mateso, walinichukua hadi Kituo Kikuu cha Polisi (Central) na kupelekwa kwa Ofisa Upelelezi wa Kanda (ZCO), Charles Mkumbo, ambaye aliamuru nishughulikiwe," ilisema barua hiyo.
  "Huyu afisa aliamuru wanitese ili niseme wanipe fedha zangu, nilipogoma walinibambikizia kesi ya mauaji… hata sikujua mauaji nimeyafanyia wapi," barua hiyo ilisema.
  Alisema baada ya kukaa Central alipelekwa Kituo cha Polisi Urafiki, ambako alipatiwa kesi nne ambazo ziko Mahakama ya Kinondoni.
  Kesi hizo ni C.C 1808/08, CC 1811/08, CC18/12/08 na PI 21/08.
  Kwa mujibu wa barua hiyo, mfanyabiashara huyo anasema aliombwa kiasi cha sh milioni nne na polisi hao kama rushwa, lakini alikataa kutoa na walimwambia atakiona cha moto.
  "Niligoma kutoa kiasi hicho cha fedha kwa sababu hakuna tukio lolote baya ambalo nimelifanya," ilisema sehemu ya barua hiyo.
  Jambo jingine linalolalamikiwa na mfanyabiashara huyo ni hatua ya upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika tangu mwaka jana huku akiendelea kusota mahabusu.
  "Nakuomba DPP fuatilia suala hili ili unisaidie kutatua tatizo hilo kwa misingi ya sheria, maana kuna watu tuliowapa dhamana ya kulinda jamii lakini badala yake wamekuwa wakiitesa," ilisema barua hiyo.
  Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili ofisini kwake, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba, alionekana kushtushwa na tuhuma hizo na kusema ofisi yake haijapokea malalamiko hayo.
  "Nakuhakikishia kwamba suala hili halijanifikia mezani, limenishtua, nakuahidi kulifanyia kazi kuanzia sasa ili kujua ukweli kati ya polisi na mfanyabiashara huyu," alisema Manumba. Alisema polisi kama chombo cha kulinda amani, kitaanza uchunguzi huo mara moja ili kubaini mtandao uliopo kati ya pande zote mbili.
  "Tutafanya uchunguzi ili tujue ukweli wa tukio hili, kama kuna yeyote aliyehusika atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria," alisema DCI Manumba.
  Alisema licha ya uchunguzi huo, polisi watamchunguza mfanyabiashara huyo ili kubaini kama aliwahi kuhusika na matukio ya wizi.

  Source:Tanzania Daima
  My question: Je hii inawezekana? na huyu jamaa sh milioni 60 alikuwa kazibeba vipi, hali ni mbaya hapa kwetu je huyu jamaa hakujua hili
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Huenda kweli ni mhalifu hata wa unga..60m cash home pesa nyingi sana!
   
 3. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Ni dhambi kuwaza hivyo wakati Polisi wamepewa kazi ya kufanya hiyo kazi ya kufanya uchunguzi ili kubaini uhalali wa hiyo fedha. Na wamekuwa na muda wa kutosha tangu Nov. 08?
  Mfanyabiashara kuhodhi fedha hiyo nyumbani kwake inawezekana. Wengi wanakuwa nazo kwa sababu moja au nyingine. Mimi nisingeshauri mtu kuweka kiasi kikubwa hivyo nyumbani maana kinaweza kuwachanganya akili makamanda wetu eti!
   
Loading...