Kashfa nchini Kenya: Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Seneti kuhusu Covid-19 ajiuzulu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Seneta wa mji wa Nairobi na mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Seneti kuhusu COVID-19, Johnson Sakaja, ameamua kujiuzulu baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka sheria za kutotoka nje, zilizowekwa kwa kupambana dhidi ya janga la COVID-19. Alikamatwa Ijumaa jioni Julai 17 katika baa saa saba usiku.

Seneta Johnson Sakaja amesikilizwa leo Jumanne asubuhi na Mahakama moja ya mji mkuu wa Kenya.

Kulingana na mwandishi wetu nchini Kenya, Sébastien Németh, Jaji alipata taarifa ya kujiuzulu kwa Johnson Sakaja. Jaji huyo alikuwa amemhukumu kifungo cha miezi mitatu au faini ya Dola 150. Baada ya kupatikana na hatia, Johnson Sakaja ameepuka kufungwa jela kwa muda wa miezi mitatu na hivyo kuamua kulipa faini ya Dola 150.

"Nimelipa faini na ninajikubalisha mbele ya Wakenya kufuata sheria na hatua zingine. Ninawashukuru wale ambao waliniunga mkono kwa kuwa wenye uelewa. Sisi sote ni wanadamu, " Johnson Sakaja amesema.

Kuanzia mwanzo, Johnson Sakaja alijizuia kuzungumza chochote kwa mtu yeyote au kwa vyombo vya habari na kukubali kujishusha. Seneta Johnson Sakaja amekiri makosa mbele ya Mahakama leo Jumanne. Jumatatu wiki hii alifika kituo cha polisi na kuweza kujisalimisha: "Sije kuomba msamaha. Ninashutumiwa kwa kukiuka sheria za kutotoka nje ambazo ziliwekwa na serikali katika kupambana dhidi ya COVID-19, na ni kweli. Nilikosa na ninasikitika. Ninajutia kitendo nilichofanya. Sheria inatumika kwangu kama inavyotumika kwa Wakenya wote. "

Kwa kushangaza, Johnson Sakaja alikuwa akisimamia Kamati ya Baraza la Seneti iliyopewa jukumu la kujadili na kutathmini vikwazo vilivyowekwa dhidi ya COVID-19. Sheria ambazo yeye mwenyewe alivunja.

Hata hivyo, Johnson Sakaja amekosoa kitendo ch apolisi cha kutumia uwezo kupita kiasi. Amesema karibu maafisa 50 waliojihami kwa bunduki walifika nyumbani kwake Jumamosi na Jumapili, na kutishia familia yake. "Mimi sio muuaji, wala katili. Watoto wangu hawajafanya uhalifu wowote, kwanini kuwanyanyasa na bunduki? Seneta Johnson Sakaja amesema.
 
Back
Top Bottom