Kaseja atetewa

Kaseja atetewa

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,687
"Wadau wengi wanataka Simba ibadilishe uamuzi wa kumtema Juma Kaseja kwa vile bado ana uwezo mkubwa na ndiyo maana ninahodha wa Taifa Stars."

Dar es Salaam.Baadhi ya wadau wa soka, wamekosoa uamuzi wa klabu ya Simba kutangaza kumtema kipa wake namba moja, Juma Kaseja na kusema hatua hiyo imechangiwa na siasa za chuki dhidi ya kipa huyo.
Kwa wiki nzima sasa, suala la Kaseje kutemwa limekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari, huku ikielezwa kuwa uamuzi huo umewagawa viongozi wa klabu, kwani baadhi yao wanataka aendelee kubaki.
Rafiki wa karibu wa Kaseje amelitonya gazeti hili jana kuwa, kipa huyo kwa sasa yuko nje ya jiji na kwamba anatarajia kuzungumzakwa mara ya kwanza kuhusu hatima yake Simba Jumapili wiki hii.
Mwenyekiti wa Simba na hata kocha Abdallah Kibadeni walikaririwa wakisema, kipa huyo aliyesajiliwa mwaka 2003 kutoka Moro United hatakuwamo kwenye kikosi hicho msimu ujao.
Kipa wa zamani wa klabu hiyo, Moses Mkandawile ameshutumu uamuzi wa Simba kumtema Kaseja kwani, yeye binafsi anaamini Kasejandiye kipa bora kwa sasa Tanzania.
“Huyu ni nahodha wa timu ya Taifa, ikiwa na maana kwamba kiwango chake bado kiko juu. Sasa iweje Simba wamteme kwa madai ya kushuka kiwango? Kweli uamuzi huu unashangaza sana,” alisema Mkandawile.
“Nadhani kuna chuki binafsi kati yake na baadhi ya viongozi ndiyo maana wengine wanapinga Kaseja kutemwa,” alisema zaidi kipa huyo wa zamani.
Aidha, Katibu Mkuu wa zamani TFF, Fred Mwakalebela naye alishangazwa na uamuzi wa Simba kumtema kipa huyo na kusema haukuzingatia uwezo wake, bali chuki kutoka kwa baadhi ya viongozi wake.
Mwakalebela alisema, anaamini Kaseja bado ni kipa mwenye uwezo wa kucheza timu yoyote kwa vile kiwango chake bado kinadai tofautina mawazo ya watu wengine.
Kwa upande wake, mchezaji wa zamani Yanga Kitwana Manara alisema walichokifanya kwa Kaseja siyo sahihi hata kama mpira umekwisha anatakiwa apewe heshima yake kama mchezaji aliyeitumikia klabu muda mrefu.
“Huyu ni alama ya mafanikio Simba, alipaswa kupewa heshima kubwa. Kama hawataki kumsajili, basi wangemweka kwenye benchi la ufundi,” alisema Manara.
Kwa upande wake, nyota wa zamani Taifa Stars, Peter Tino alisema masuala ya usajili waachiwe viongozi na benchi la ufundi na kwamba wasisikilize kelele za mashabiki.
“Kaseja ni kipa mzuri mpaka sasa, ana uwezo wa kucheza zaidi tofautina wengine wanavyodhani. Apewe nafasi nyingine aonyeshe uwezo wake,” alisema Tino.
Kocha Kennedy Mwaisabula ameishauri Simba kufuta mpango wake wa kumtema kipa huyo, kwani bado ana uwezo mkubwa.
Wakati huohuo, klabu ya Yanga imekana taarifa kuwa ina mpango wa kumsajili Juma Kaseja.
Katibu wa Yanga Laurance Mwalusako alisema, wanatambua kuwa Kaseja bado ana uwezo mkubwa langoni, lakini hayuko kwenye mpango wa kumsajili kwa vile wana makipa wazuri. Kaseja aliwahi kucheza Yanga msimu mmoja, mwaka 2009.

Chanzo: MCL
 
Aaaah...jamani! Kwani wachezaji wenye uwezo mkubwa hawatemwi! Kama hawana nidhamu au hawafit kwenye mpango wa mwalimu waachwe tu..na mishahara yao mikubwa alipe nani!? Klabu ngapi duniani zimeuza wachezaji wakubwa wakiwa kwenye peak kwa sababu za kinidhamu au kutofautiana na kocha!?
 
''KASEJA bado anaitajika kwa sana tu ndani ya MSIMBAZI''
........that is what only i can say.
 
Timu ziko nyingi sana..kama yeye bado ni kipa mzuri atapata timu. Kulalamikia uamuzi wa watu ambao wanamlipa mshahara si haki. Simba SC wana haki ya kuamua kumtema mchezaji yeyote. Kama kweli jamaa ana uwezo mkubwa kama tunavyosema tusubiri tuone! Mpira hauchezwi mdomoni.
 
Mwl. Nyerere ni mwasisi wa CCM, kipindi cha uhai wake aliwahi kusema 'CCM siyo baba wala mama', falsafa hii anaweza kuitumia Kaseja, aseme Simba siyo baba yake wala mama yake asajiliwe timu nyingine aendelee na maisha yake, over all hakuanzia mpira Simba hivyo ataendelea kucheza mpira nje ya Simba.
 
Kutemwa ni sawa tu,unaweza kufanya kazi ktk kampuni kwa miangi ila professonal,technical/logy, yanaweza kukondoa kazini.
 
Jana Kaseja akihojiwa na mmoja wa waandishi wa habari huko mkoani Kigoma, alisema kwa sasa hawezi kuzungumza chochote hadi hapo baadaye.
 
klabu ya Yanga imekana taarifa kuwa ina mpango wa kumsajili Juma Kaseja. Katibu wa Yanga Laurance Mwalusako alisema, wanatambua kuwa Kaseja bado ana uwezo mkubwa langoni, lakini hayuko kwenye mpango wa kumsajili kwa vile wana makipa wazuri.

Chanzo: MCL

Simba na Yanga ni taasisi, na sio timu ya mtu kusema akilala akiamka anamfukuza mchezaji anavyotaka.

Hapo juu ni maoni ya Club Yanga kuhusu Juma K Juma.

Binafsi naheshimu maoni ya club ya Yanga na hivyo hivyo nyie waandishi habari na jamii kwa ujumla muheshimu maamuzi ya Simba kuhusu kumuacha Juma K. Juma. Case Closed
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom