Niliwahi kusoma habari toka katika media moja ya kitanzania miaka ya tisini kuwa Yanga walinunua kiwanja kile toka kwa mama mmoja wa kizaramo lakini mama wa watu hakulipwa kama makubaliano yalivyokuwa... Kuna mtu ana ufahamu juu ya hili?
Mkuu hapa nakusudia kuweka kumbukumbu sawa kama ni kweli rais Abeid A. Karume licha ya kutoa mchango wa pesa Yanga je hakutoa kwa klabu ya Simba pia?Niliwahi kusoma habari toka katika media moja ya kitanzania miaka ya tisini kuwa Yanga walinunua kiwanja kile toka kwa mama mmoja wa kizaramo lakini mama wa watu hakulipwa kama makubaliano yalivyokuwa... Kuna mtu ana ufahamu juu ya hili?
binafsi sina hakika lakini kwa jinsi mke wake anavyoipenda Yanga yawezekana hata mme wake pia alikuwa mdau wa Yanga na kama alikuwa mdau wa Yanga kweli isingekuwa rahisi kuchangia maendeleo ya Simba.Mkuu hapa nakusudia kuweka kumbukumbu sawa kama ni kweli rais Abeid A. Karume licha ya kutoa mchango wa pesa Yanga je hakutoa kwa klabu ya Simba pia?
Mkuu, palikuwa na tetesi kuwa hata klabu ya Simba alichangia ndio maana nimeona kumbukumbu tuiweke sawa hapa JF. Sipendi kuhisi kama pesa aliyoichangia klabu ya Yanga aliitoa mfukoni mwake (kama hakuchangia Simba lakini) ila alifanya hivo kama rais wa Zanzibar.binafsi sina hakika lakini kwa jinsi mke wake anavyoipenda Yanga yawezekana hata mme wake pia alikuwa mdau wa Yanga na kama alikuwa mdau wa Yanga kweli isingekuwa rahisi kuchangia maendeleo ya Simba.
Mkuu Jacobus kumbukumbu zinaonyesha kuwa hadi miaka ya mwisho ya sitini marehemu Mzee Kondo Kipwata alikuwa ndiye mwenyekiti wa Yanga,makamu akiwa marehemu Mzee mangara na katibu akiwa mzee katundu (yuko hai anaishi Ilala). Huyu mzee katundu ndo aliandika katiba ya Yanga ya mwaka 1968. Ikumbukwe wanaYanga walikuwa na ushirikiano wa karibu na African Association ya Zanzibar na ukaribu huu uliingia mpaka kwenye siasa za kutafuta uhurui wa bara na wa Zanzibar (hadi leo kuna mialiko ya Zanzibar/bara kutembeleana March/april) kila mwaka. Ni kutokana na historia hii Mzee karume aliamua kuitunuku Yanga eneo ambapo lipo jengo la Yanga na uwanja wa Kaunda,wakati huo Mwenyekiti alikuwa ni marehemu Mzee Mangara.Licha ya kutoa eneo (ambalo alilipima kwa miguu) lakini pia alitoa sh milioni mbili laki saba (pesa nyingi mwaka 1971) kwa ajiri ya ujenzi uliosimamiwa na Mzee Mangara (RIP).Kabla ya hapo makao makuu ya Yanga yalikuwa mtaa wa mafia katika kiwanja ambacho Yanga walipewa na mpenzi/mwanachama na Yanga walihamia hapo wakitokea eneo la Fire.Rais wa kwanza wa Zanzibar na mmoja wa waasisi wa Tanzania marehemu Abeid Aman Karume (Mungu amrehemu) alipenda michezo na katika kudhihirisha hilo yasemekana ndio muwezeshaji wa jengo la klabu ya Yanga ya Dar.
Sasa naomba tuweke kumbukumbu yake vizuri kama aliishia hapo tu au hata klabu ya Simba alichangia ujenzi wa jengo lake.
Aksanteni sana wakuu, Jamal Malinzi na Makoye Matale, kwa ufafanuzi japo kidogo. Historia inakuwa marehemu Abeid Aman Karume alichangia na klabu ya Simba pia pesa za ujenzi wa jengo sawa na klabu ya Yanga. Kwa hiyo si halali klabu ya Yanga kumkumbatia na klabu ya Simba kumyamazia.
Pana mwanachama wa Yanga mmoja hapa anasahihisha kuwa mzee Karume alitoa milioni mbili kwa Simba na kuwashauri wabadili jina.Jambo ambalo halina shaka ni kuwa Marehemu Mzee Karume alikuwa Yanga damu,ila kiukweli Marehemu Mwalimu Nyerere sijui alikuwa mnazi wa timu gani ila kwenye ugomvi wa Yanga wa mwaka 1975-1976 bila shaka alichukua upande kati ya Yanga raizoni na Yanga kandambili ( neno 'yanga kandambili' lilibuniwa na Juma Pondamali kipa wa Yanga na mwalimu wa makipa Taifa stars kwa sasa).
Pana mwanachama wa Yanga mmoja hapa anasahihisha kuwa mzee Karume alitoa milioni mbili kwa Simba na kuwashauri wabadili jina.
Sawa mkuu anakushukuru kwa taarifa.Hahahaha hayo muulize mtu kama mzee Omar Gumbo (0719552393) kipindi hicho cha ujenzi alikuwa winga hatari wa simba au half beki four wao Aden Rage enzi hizo.Halafu ukiongea nao wambie wakupe kumbukumbu ya mechi ya Yanga vs Simba ya mwaka 1968 (yanga 5 simba nunge) uwanja wa Karume,watakupa stori ya mchezaji wa simba aliyeibukia kwenye uzi wa yanga siku ya mechi ( miaka hiyo hakuna usajili formal).
By the way Mwenyekiti wa Yanga wakati huo Mzee Kondo Kipwata alisema simba hawatakaa wamfunge kwa miaka mitano na kweli Yanga iliitandika simba kwa kipindi chote kuanzia 1968 hadi walipokuja kufungwa na simba bao moja bila mwaka 1973 kama sikosei mfungaji akiwa Abbas Dilunga,enzi kuna kitu kilikuwa kinaitwa 'kubeba ubao' na kuupeleka nyumbani kwa kiongozi iwapo kasusa uongozi wakati wanachama bado wanamtaka.