Karume na Seif waanza pandisha jeki

Unajua, hili kaburi liko hivi kwa ajili ya Muungano. Ni Watanganyika wamefanya hadi jamaa washindwe kuondoa vipande vya bati na kusafisha nyasi sehemu ambapo Vigogo wa Zenji wanakuja kusali. Sijui ni kaburi la nani. Ila anaonekana alikuwa mtu maarufu na walishindwa kabisa kulisafisha kabla ya MISA. Hii ilifanyika ili kuonyesha uonevu wa Wabara kwa Wazenji, Saafi sana.


Safi sana ... yaani unamaanisha hapo ilikuwa inamiminwa misa... hayaga weeeee mi simo

.................................
Amani yetu inatumiwa vibaya.
 
1. Sasa ndugu, udini utakuwepo vipi Zenj wakati nyote ni Waislamu?
2. Ubaguzi wa kati ya mzanzibar na Mtanganyika utatoka wapi wakati wafanyakazi wote wa Zenj ni Wazenj?

Wewe huoni jinsi mnavyo nyonya bila kulisha? Nyie ni wazanzibar na pia ni watanganyika! Watanganyika ni watanganyika na sio wazenj. Unaweza kuishi kokote na kufanya kazi kokote wakati mtanganyika hawezi hivyo, HUO UBAGUZI huuoni? Serikali ya muungano ni yetu sote ila ya Zenj ni yenu peke yenu. Tanzania ni yetu sote ila Zenj ni yenu peke yenu! Ebo, wabaguzi ni kina nani?

ETI? Serikali ya Muungano ni yetu sote? Umelala kijana huku ukitamka hayo?
Anza na Rais wa Muungano na uangalie mangapi anayoifanyia Zanzibar? Hotuba zake za mwisho wa miezi anazungumza mangapi kuhusu Zanzibar? Zanzibar ilikosa umeme kwa kipindi cha miezi 3 jee Rais na Makamo wake walisema chochote kwa Wazanzibari au hilo halikuwa jambo kubwa? Hotuba maarufu ya Rais wa Muungano aliyotowa baada ya tatuizo la Zanzibar ni nchi au la, nini alisema Rais wenu ? akitumia lugha ya "WAO" alipoiadress Zanzibar katika dakika tano tu alizozungumzia Zanzibar kwenye hotuba iliyochukuwa masaa matatu na nusu. Unataka uthibitisho gani tena kuwa Serikali ya Muungano ni ya Tangamyika? OF COURSE katika masuala ya kuikandamiza Zanzibar Serikali ya Muungano inakuwa mbele .
Nenda kwenye Bunge na Baraza la Mawaziri na unieleze issue gani ya Zanzibar zaidi ya kusema Zanzibar si nchi imewahi kushughulikiwa na chombo hicho? Wacha kuzuga akili yako kwa kufikiri kuwa tuna umoja wa umoja bali tuna umoja wa mmoja kumuonea mwengine basi.
 
Kila mtu na sukani yake sawa.lakini ukiacha jazba na kutuliza kichwa ukawaza na kuwazua ni upande upi ulotegemezi kwa mwenzie? Angalia temeke tu wapemba walivyojazana na frem zao nini namanga kkoo masaki hadi ubungo. Nie ni wafadhilaka mmezoea KUUTIA KASI BORAYEISHE ALAAAA tugawane fito uchuguzi ukifika wake zenu wabara mwawatimua Mpaka mmalize chaguzi zenu ndo ubinadam gani huooo ati ammy.MBONA KULALA AAG .........endeleeni kuramba sijui mwaramba nini

Usiwe na shaka Ngala.

Wapemba unaosema wamejazana Kkoo, Masaki hadi ubungo watabadilisha status na kuwa wawekezaji wa kigeni halafu wataomba wapatiwe likizo ya kodi (tax holiday) kama walivyo wawekezaji wa nje wa kwenye migodi na mahoteli makubwa. Si unajua tena watanganyika bado wamelala usingizi wa pono.

Faida itakayopatikana kutokana na biashara na taxi holiday itatumika kuijenga Zanzibar Mpya.
 
dhambi ya dhuluma itawapata watanganyika kwa kuitawala zanzibar kimabavu...
asilimia 99% ya wazanzibari hawataki muungano . kwanini tanganyika ilazimishe huu muungano...kuhusu hawa wapemba, sio temeke wala ilala au tandale . wapemba wako karibuni kila nchi duniani. kuwepo kwa wapemba temeke haina maana kama wanaukubali muungano...kuna wapemba mombasa, kampala ,maputo,,durban na hizi sio sehemu za tanzania. madai ya wanzanzibari kuwa serikali ya smz iongozwe na wazanzibari wenyewe na sio kuchukua amri ya ccm dodoma au amri ya Pinda au ya watanganyika...maendeleo ya zanzibar yanazuiliwa na muungano, hili halina shaka. na muungano ukivunjika zanzibar itakuwa kama zamani...wakati ina sarafu yake na hakiba ya fedha za kigeni za kutosha... hawa watanganyika wanoa lazimisha huu muungano wanafaidika nini?
kwanini hamufungui macho au bado mnaamini nyerere yuko hai?
Zanzibar haina hela yoyote hiyo BOT Zanzibar ni kama sehemu ya kutolea hela ya matumizi ya nyumbani tu mkiishiwa mnarudi tena huku bara kuhemea
 
Ile picha ya kaburi imesummarize kila kitu kuhusu mstakabali wa Zanzibar.....Uvivu ni adui mbaya sana
 
Islamic State of Zanzibar " ndio kihoro"kwa wabara...maana itakuwa Iran ndogo
 
Islamic State of Zanzibar " ndio kihoro"kwa wabara...maana itakuwa Iran ndogo
Never will it be, karibu tena naona ulipotea nikaona nilete ile thread ya waraka wa Tafakari nilijua tu utatokea but for this case keep on dreaming
 
Mkuu yale si maneno yangu, nakumbukia tu aliyosema Mwalimu. Thibitisha hapa kuwa Wazanzibari hawafaidiki na Muungano. Pia kumbuka kwetu sisi Wabara kuvunjika kwa pakacha ni nafuu ya mchukuzi.
Siyo maneno yako lakini unayaamini bila ya kujuwa kuwa msemaji wa maneno hayo(Nyerere) alikuwa mnafiki mnafiki,mzugajizugaji...kikubwa alichofikiri kuwaletea watu wake siasa za kuwatia njaa na umasikini hadi leo(ujamaa na kujitegemea), ubaguzi aliouwongea hapo hatuujuwi kwa mantiki ipi,na kama ni kwa ajili ya muungano wa Tanganyika na zanzibar, ndiyo kabisa alijitaftia kundi lake la wanafiki, kwani si ndo yeye aliyeshabikia muungano wa Afrika na akajidai ikibidi hata tuanze kwa kuunganisha nchi moja moja(kama Tanganyika na zanzibar) wakati huo huo anarudi kuunga mkono uasi wa kujitenga kwa jimbo la Biafra kutoka Nigeria. Zanzibar haijawahi kufaidika kiuchumi na serikali ya muungano uthibitisho ni hali ya uchumi ya zanzibar ilivyokuwa kabla na baada ya muungano, hatua za zanzibar kutaka kujikwamuwa kutoka hali mbaya kiuchumi zinarejeshwa nyuma na SMT, hatua za zanzibar kujitaftia washirika wa kimaendeleo wanaofanana na utamaduni wao zinakwamishwa kwa makusudi na SMT (mfano hapa OIC saga), matatizo ya ndani ya kisisa na machafuko yanasababishwa na SMT kuwalazisha wazanzibari lazima wabaki chini ya utawala wa CCM,inayolinda maslahi ya muungano kandamizi visiwani, haya yote na mengine yanachangia hali ya kukosekana kwa utulivu na umoja wa wazanzibari walionyang'anywa tokea tarehe 12 Januari,1964 mpaka leo.
 
Msiwe na kiherehere ,nasema kubwa lijalo ,narudia kuwa Muungano hauguswi ila kila mtu na sukani yake ,nikimaanishaa Tanganyika ipo on the horizon...!Ningewamegea lakini naona hamjui mtokako au hamjui kwenu ni wapi au mnakudharau kule ambako ni haki yenu kuwa nako ,kukutetea,kukulinda ,where are they .......& what was their aim..and what stops them .....? Kikwete na kundi lake G ? Hivyo kwa WaZanzibari hawatakuwa kama akina Kikwete kutishwa wakatishika ,they will prevail !!! Believe me !!
 
Zanzibar haina hela yoyote hiyo BOT Zanzibar ni kama sehemu ya kutolea hela ya matumizi ya nyumbani tu mkiishiwa mnarudi tena huku bara kuhemea
muulize nyerere mara ngapi alikopeshwa pesa na zanzibar za kuwaliwapa wafanyakazi ...unajua ilipo anzishwa BoT zanzibar walitoa kiasi gani?
 
Zanzibar haina hela yoyote hiyo BOT Zanzibar ni kama sehemu ya kutolea hela ya matumizi ya nyumbani tu mkiishiwa mnarudi tena huku bara kuhemea

Muungwana kama umetizama thread zangu za nyuma wakati zinaunganishwa sarafu za Tanganyika na zanzibar. Zanzibar riyal moja ilikuwa sawa na East African shilings 3.4 sasa wewe kwa akili yangu nani alikuwa na msuli mkubwa wa kipesa. Na mbona BOT tukiomba data za BOT ilianza na mtaji gani baina ya Zanzibar na Tanganyika tunanyimwa kunani!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom