Karume avirushia madongo CUF, NCCR-Mageuzi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,241
33,002
Karume(42).jpg

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Amani Abeid Karume



Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Amani Abeid Karume, amesema chama hicho hakina utamaduni wa kuwafukuza viongozi wake waliopewa dhamana kuwaongoza wananchi kwa vile kinaheshimu misingi ya demokrasia na utawala bora.

Tamko hilo amelitoa wakati wa uzinduzi wa kampeni za kuwania nafasi ya Uwakilishi, katika uchaguzi mdogo katika jimbo la Uzini unaotarajiwa kufanyika Febuari 12 mwaka huu.

Karume alisema kwamba demokrasia ndani ya CCM tofauti na vyama vingine hasa katika kuheshimu maamuzi ya wanachama kupitia kura za maoni, na ndio maana kikamteua kada wake, Mohamed Raza ambaye alichaguliwa na wanachama wengi kati ya wagombea 14 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.

Alisema kwamba CCM siku zote imekuwa ikiheshimu maamuzi ya wanachama na wananchi, na ndio maana Chama hicho hakina utamaduni wa kufukuza watu bila ya kuzingatia maamuzi ya waliyo wengi, na kumrudisha mgombea aliyechaguliwa kwa kura ndogo na kumwacha aliyechaguliwa kwa kura nyingi.

“Vyama vingine hawana utaratibu huu, wanapeleka watu waende kugombea, halafu wanasema ooh mambo yameharibika, sasa yakiharibika mambo tena yule aliyechaguliwa na aliyependekezwa na wananchi, anawekwa mwisho na yule wa mwisho ndio anawekwa mwanzo, sisi CCM mnayemchagua ndiye tunayewarejeshea,” alisema Karume.

Aidha Karume alisema sio mwafaka kubeza maendeleo katika jimbo la uzini, kwa vile Serikali ya CCm imefanya kazi kubwa ya kujenga barabara katika jimbo hilo, na kuwasogezea huduma muhimu.

Kauli ya Karume imekuja siku chache tangu vyama vya NCCR- Mageuzi na CUF kuwavua uanachama wabunge wao, kwa madai ya kwenda kinyume na katiba na maadili ya vyama hivyo, ambao ni Hamad Rashid mohamed (CUF) na David Kafulila (NCCR-Mageuzi).

Naye Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa alisema mrithi wa jimbo hilo lazima atoke CCM, ili aweze kuyaendeleza malengo na mafanikio ya chama katika jimbo hilo kupitia Ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2010/15.

“Ukoo unapofiwa, mrithi wake atatoka katika ukoo ule ule, na mrithi wa jimbo hili lazima atoke CCM,” alisema Msekwa.
Aliwakumbusha wanachama wa CCM kujiandaa na uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaofanyika mwaka huu, sambamba na kujipanga na zoezi la kura za maoni kuhusu mabadiliko ya katiba mpya ya Tanzania.

Naye mgombea wa Chama hicho, Mohamed Raza Dharamsi, aliwahakikishia wananchi wote wa Uzini kuwa atatekeleza vyema ilani ya chama hicho, na kusaidiana na Serikali katika kwasogezea wananchi wake maendeleo, pamoja na huduma za kijamii.

“Nawaomba ndugu zangu wa uzini, kwanza nyinyi ndio mulionifikisha hapa, bila ya nyinyi Raza asingejulikana wala kupata nafasi hii, hivyo nawaomba nyote munipe kura zeni za ndio ili niwaletee maendeleo,” alisema Raza.
Raza aliwataka wananchi wa jimbo kuondoa wasiwasi na wapinzania aliowafafanisha na kelele za mlango, ambazo hazimkoseshi usingizi mwenye nyumba.




CHANZO: NIPASHE
 
Hii kauli ni very controversial. Tafsiri yake ni kwamba, moja, kitendo cha Rostam kuondoka kwa kushinikizwa kilivunja misingi ya demokrasia. Na pili, ni kuhusu hekaheka za kuvuana magamba CCM ambapo, kwa kauli hii ya karume kama Makamu Mwenyekiti wa CCM (Visiwani), ametoa jibu kwa umma kwamba suala la kuvuana magamba halipo. Whether alimaanisha kutoa ujumbe huu au umemponyoka kwa bahati mbaya, kwa maneno hayo, mjadala wa gamba umefungwa rasmi.
 
mbona huo mjadala wa kuvuana magamba ulishafungwa siku nyingi. Hakuna wa kumvua gamba mwenzake hapo maana sisiem yoote imegeuka gamba. Tena lililokwisha kauka
 
Hii kauli ni very controversial. Tafsiri yake ni kwamba, moja, kitendo cha Rostam kuondoka kwa kushinikizwa kilivunja misingi ya demokrasia. Na pili, ni kuhusu hekaheka za kuvuana magamba CCM ambapo, kwa kauli hii ya karume kama Makamu Mwenyekiti wa CCM (Visiwani), ametoa jibu kwa umma kwamba suala la kuvuana magamba halipo. Whether alimaanisha kutoa ujumbe huu au umemponyoka kwa bahati mbaya, kwa maneno hayo, mjadala wa gamba umefungwa rasmi.

Nadhani hoja iko local zaidi-hajawaza huko mbali, na hii ndio siasa hasa! unatumia udhaifu wa wenzenu kuwa kejeli dhidi yao! amenifurahisha mtu mzima!
 
Siasa za Zanzibar hazijawahi kuhusisha vijembe kwa vyama zaidi ya CCM na CUF. Huyo muandishi aliyeitaja NCCR itakuwa simzoefu labda
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom