Noncommited
JF-Expert Member
- Jun 22, 2012
- 1,125
- 369
Shule ya St. Patrick Arusha imepandisha tena ada kwa mwaka 2016. Hata hivyo, ada ambayo ilikuwa inalipwa mwaka huu wa 2015 bado ilikuwa juu. Kila mwaka shule hii inapandisha ada za shule. Na cha ajabu watoto waliyomaliza darasa la saba mwaka huu walilipa ada temu tatu badala ya temu mbili kwani watoto walikaa shule temu mbili tu na wiki ya kwanza ya temu ya tatu wakamaliza shule.
Malipo ya mtoto wa darasa la saba kwa mwaka huu yalilipwa kama ifuatavyo;
temu ya kwanza laki tisa,
temu ya pili laki nane na
temu ya tatu laki nane.
Ada hii ni kubwa sana na inazidi hata baadhi ya ada za shule za binafsi za sekondari. Kimsingi hizi shule hazitoi huduma bali zinafanya biashara. Tunaomba sana serikali na mamlaka husika ifuatilie hizi shule binafsi kwani zinaumiza sana Watanzania. Pia tunaomba serikali itoe bei elekezi kwa hizi shule.
Nina imani na serikali ya rais ​Magufuli kuwa itashulikia swala hili mapema iwezekanavyo kabla ya mwaka huu kuisha.
Acheni Ujinga hizo JPM aboreshe shule za UMMA ndio muarobaini wa shule binafsi na si kuziingilia kidikteta. shule za binafsi hazitaweza kutoza ADA bei kubwa kama serikali itaboresha shule zake. Kudhibiti ADA kwenye shule binafsi kutaathiri watanzania wengi wanao fanya kazi huko kama walimu, walinzi, wafagizi, wapishi, madereva na wengineo. Wafanyakazi wengi watapunguzwa kazini na kupunguziwa mishahara. Serikali iboreshe na kusimamia shule zake na si kukimbia majukumu yake na kwenye kumdhibiti mshindani wake.