Karibuni tujadili hali ya kimaisha katika Nchi mbalimbali Duniani

Mr.panya

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
248
274
Wakuu habari,

Kuna wenzetu humu angalau washapata kutembelea au kuishi nchi mbalimbali na wengineo hadi sasa bado wapo huko ughaibuni, basi kwa faida ya wengi ambao hawajawahi kufika huko naomba uchangie chochote kutokana na experience yako kwenye nchi hizo katika nyanja yoyote ile ya kimaisha kama lifestyle, fursa za biashara, starehe na burudani, vyakula, ustaarabu wa watu wa huko, gharama za maisha, usalama hasa kwa raia wa kigeni, upatikanaji wa kazi na ajira, mazingira na hali ya hewa, miji mikubwa, sheria na taratibu, gharama za safari hadi kufika huko, hali ya kisiasa n.k

Hii itasidia sana kwa watu wanaosaka maisha popote kung'amua fursa za kiuchumi katika nchi mbalimbali na kwa wale wanaotafuta makazi nje ya Tanzania, pia itatupa mwanga ni nini kinaendelea huko duniani au hata hapa kwetu Afrika.

Binafsi bado sijawahi kutoka nje ya Tanzania lakini nimepata kusikia mawili matatu kutoka kwa mtu aliofika nchini Korea kusini, kwa hiyo haya ndio machache ninayojua kuhusu South Korea.

Hii nchi ipo huko Far East katika bara la Asia, hawa watu wa far East (S. Korea, Japan, China, N.Korea, Taiwan) ni race ya watu wenye IQ kubwa sana.

Mji mkuu na muhimu nchini humo Korea kusini unaitwa Seoul.

Wakorea wanapenda sana urembo yani huko mpaka mwanaume kujipaka poda na kujichubuachubua uso na vipodozi vya aina mbalimbali ni kitu cha kawaida sana kwao yani wanapenda sana kuonekana wazuri muda wote hata kama tayari umri umeenda lakini wanalazimisha tu kuonekana wazuri na hii ndio huwapelekea mpaka kufanya plastic surgery na had sasa hii ndio nchi inayoongoza watu wake kufanya plastic surgery dunia nzima, pia wanapenda sana kujikinga na jua lisiwapige mana wanaogopa litaharaibu ngozi zao.

Hawa jamaa wanapenda san kuishi kwa lifestyle ya kimarekani yani mpka ikulu yao wameipa jina "Blue house"
Jamaa ni wajuvi sana kwenye maswala ya kieletroniki na makampuni makubw kama Samsung na LG yanatokea huko.

Hawa jamaa kwa miaka mingi sasa wapo kwenye misuguano na ndugu zao wa North Korea kwa akina mapanki lakin uzuri wao huwa hawadundani kama tulivyo sisi huku Afrika bali wao wanapeana tu vitisho na mikwala ya hapa na pale.

Upande wa fursa, hii ni nchi ya viwanda kwahiyo ni wewe tu utavyojichanganya na wenyeji unaweza ukapata hata nafasi ya kubeba boksi sio mbaya kwa nchi kama hii mana ni First wolrd country.

Kwa upande wa vyakula, watu wa Far East naweza kusema vyakula vyao vinafananafana kiasi fulani yani unavyoona Wachina wanayokula hawatofautiani san na Wakorea.

Wakuu mimi naishia hapa wengine watakuja kujazia nyama.


Karibuni!
 
Uchumi wa Tanzania unakua kwa wastani wa 7%, maisha ya wananchi yameboreka. Idadi ya maskini imepungua kwa kiwango kikubwa sana.
 
Back
Top Bottom