Karibuni Songea mji wa giza na adha ya maji

Karibuni Songea mji wa giza na adha ya maji

Crispin Nyoni

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
413
Reaction score
90
Wakuu,kuna ratiba ambayo inakera sana siku hz Songea na haya ndio maisha bora na big result now kwa kila Mwanasongea.Angalia ratiba ya umeme ilivyo na mchanganyo:
1.Kuwaka saa nne usiku kuzima saa 3:20 asubuhi.
2.Kuwaka saa 3:20 asubuhi kuzima saa moja moja kamili usiku.
3.Wakizima saa moja usiku kuwasha saa sita usiku na kuzima saa 3:20 asubuhi.
Mgao hapo haujasahaulika pia. Kabla sijasahau,maji yanaweza kukatwa siku 3 hadi 4 na wakiyaleta basi ni usiku wa manane.
Haya ndio maisha bora kwa watanzania. CCM safiiiiiiii....
 
Da! #Nyoni umenikumbusha ki2 mana kuanzia tareh 13 hata ratiba sijaielewa maana wakikata ni mpaka sa 6 sasa leo soka je?
 
da hiyo ni kweli nilikuepo huko songea mjini pale lizaboni nimekaa siku saba niliuona umeme siku mbili tu nao wa kubahatisha.du ila kunamradi wakuleta umeme wa maji huko kutoka makambako vumilia tu si nyumbani ni nyumbani?
 
Nyie aliyewaambia mchague mbunge anayekaa Dar nani? Nchimbi yeye hizo adha wala hazimuhusu anakula maisha tu.
 
kweli wajina hakai kule kabisa usumbufu wa umeme ni wa mda mrefu na halijatatuliwa mpaka atatoka madarakani
 
Da mwenyewe nipo msamala da hata raha ya umeme siioni simu ndo inataka kuzima da kweli majanga!
 
hapa nilipo umekatika asubuhi kurudi saa 6 usiku. Yaani huyu nchimbi bure kabisa. Cha kushangaza hapa songea mjini umeme hamna huko mbinga, namtumbo upo. Mimi niliwaambia tusichague ccm mnaona sasa
 
Aaa kwenye kuchagua nani na nani mi hiyo simooooooooooooooo da tanesco wananikatili nisitumie azskyg6 yangu.
 
karibia mtaunganishwa na umeme mkubwa utokanao na gesi toka mtwara,by the way niliupenda sana mji wenu nilipofika hapo wiki mbili zilizopita kupitia tunduru nikitokea lindi
 
#Binamu kumbe ndo umeingia leo! karibu ktk mgao wa umeme naona unataka kufanana na ule mgawo wa mkoa wa kagera da!
 
Nyie aliyewaambia mchague mbunge anayekaa Dar nani? Nchimbi yeye hizo adha wala hazimuhusu anakula maisha tu.

Mkuu,sidhani kama kuna mwananchi mwenye akili timamu akachagua ccm kwa hiari yake. Yawezekana waliponzwa na kofia,kanga,fulana,mashati,wali na hela. Hata hivyo kila anayetaka kuchomoza kichwa kugombea ubunge linapita fyekeo la chuma shingoni wasiendelee. Cha msingi na cha chuo kikuu nguvu ya umma haishindwi na chochote kwani ni nguvu ya MUNGU. Mpe pole mkuu Binamu.
 
umewaka usiku huu nikiamka najua utakuwa umekatika. Ngoja nicharge ka simu kangu
 
miaka zaidi ya 50 ya uhuru bado tupo kwenye utumwa wa maji na umeme....

yahitaji ukomboz wa fikra na madiliko ya ukweli
 
kwahali ya songea umeme umekuwa kelo kubwa.mchimbi hana jipya.nazani nimda mwafaka wanasongea tukailazimisha tanesco kutupa huduma inayo stahiri.
 
Aaa lkn wametangaza wanafanya marekebisho wa mashine ndo mana mgawo wa kuanzia 13 septemb ni #nouoma ni zaid ya masaa 18
 
Endelea kuchagua wabunge wasio na mchango wowote! Mnamkumbuka MAREHEMU GAMA, bila yeye songea ingekuwa na lami ya udongo wa mwekundu! Hata hvy hyo uraniamu inafanya nini huko namtumbo?
 
Jana niliandamana mpaka tanesco songea.. ... Nkacharge smu pale mahenge,nikaingia jamiiforums kupitia my laptop... Waliisoma namba. Wakikata tena leo naenda kufanya kazi zangu pale ofisini kwao
 
Back
Top Bottom