Karibuni mitaani

Karibuni mitaani

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
19,147
Reaction score
43,079
Karibuni mitaani muone Vijana wamezika ndoto zao kwa sababu ya umaskini...

Karibuni mitaani muone vipaji vilivyofeli kwa kukosa support...

Karibuni mitaani muone Degree zilivyojaa Kwenye vijiwe vya Bodaboda...

Karibuni mitaani muone wenye uwezo wamekosa kazi kwa sababu ya kukosa Connection...

Karibuni mitaani muone mchongo shape kubwa sio una elimu gani kubwa...

Karibuni mitaani muone betting ilivyo ajira kwa Vijana, karibuni mitaani...

Karibuni mitaani muone idadi ya vijana walioambiwa tutakupigia simu baada ya kupeleka barua ya kuomba kazi...

Kwa kifupi karibu mitaani uje uone maisha ya mpiga kura...
 
Karibu mtaani uone vijana walioishia kidato cha nne ambo ni asilimi 60% kulinganisha na wanaoendelea elimu ya juu, asilimia kubwa ya hawa vijana wameharibika wanabaki kulaumiwa na familia na jamii ikiwaadhibu kwa kuwatenga ilihali jamii na mfumo ndio umewaharibu
 
Karibu mtaani uone vijana walivyoharibika kwa madawa ya kulevya, huku waingizaji na wasambazaji wakuu ndio viongozi na marafiki wa utawala ulipo madarakani
 
Karibu mtaani uone vijana wanavyolipwa ujira mdogo kwa kazi ngumu na hakuna sheria za kuwalinda, watunga sheria wameamua kutuita ngedere
 
Karibuni mitaani muone Vijana wamezika ndoto zao kwa sababu ya umaskini...

Karibuni mitaani muone vipaji vilivyofeli kwa kukosa support...

Karibuni mitaani muone Degree zilivyojaa Kwenye vijiwe vya Bodaboda...

Karibuni mitaani muone wenye uwezo wamekosa kazi kwa sababu ya kukosa Connection...

Karibuni mitaani muone mchongo shape kubwa sio una elimu gani kubwa...

Karibuni mitaani muone betting ilivyo ajira kwa Vijana, karibuni mitaani...

Karibuni mitaani muone idadi ya vijana walioambiwa tutakupigia simu baada ya kupeleka barua ya kuomba kazi...

Kwa kifupi karibu mitaani uje uone maisha ya mpiga kura...
Karibu mtaani uwaone watu waliofeli shule wamefaulu maisha.
 
Karibu mtaani uone wapambanaji wanavyowekewa kodi lukuki kwenye biashara na miradi wanayoanzisha ilihali anayeweka kodi ndio amekataa kuwaajiri anawatafuta huko walipojiajiri
 
Kama wamezika Ushauri wa Sasa wafanye nini ili kesho yao iwe Bora. Au nawe huna ushauri nini kifanyike
 
Ukiwa unakuja usisahau akili zako maana ukiziacha utaishia kusema MAMA ANAUPIGA MWINGI kwa furaha na bashasha
 
Kabisa, wakaribie sana waje waseme 'no election no reform' kwa maringo kama kule Dodoma walikomvimbia Msigwa. Tena waseme kwa sauti na kujimwambafai haswaaaa kama watu waliofanikiwa sana.
 
Oyaaaa Hii Africa hasa hii Tanzania kuna mambo ya ajabu sana.
Hebu fikiria Serikali inawekeza kwa kusomesha Wanafunzi vyuo vikuu halafu wakitoka vyuo vikuu wanakuwa madereva bodaboda.

Na ule uwekezaji uliofanywa na Serikali unakuwa umepotea bure 😥
 
Jay z aliwahi kuimba kitu Kama hiki I think na akasema kuna mitaa ukizaliwa Kama Brooklyn unakuta mambo ya kukutoa katika mfumo yabakusubiri. Like sex, drug , n.k na wachache ambao huenda kinyume either watakuwa gunned or watakuwa jailed or katika ladar za Askari.

And people do this shit because had no better option in life .

Street is watching you.
 
Back
Top Bottom