Karibu UtuExchange!

Nimejiunga mzee ... kazi imetualia.

Lakini kiasi cha kuanzia (2000U) ni kidogo sana baba mkubwa. Kwa mfano nikikuta share za 30U nnapata kama 60 tu. Sasa kwa kuanzia kidogo haimpi mtu munkari wakuinvest.

Ingeanzia kama 15000U ingekuwa mwake baba ake.
 
Nimekupata bwana Fisadi.

Ninaiingiza kwenye mchakato wa maboresho. Tuaifanya vizuri zaidi. Baada tu ya kuingia mtu atakuwa anapewa 25,000U kama mtaji.

Hiyo itakuwa tayari kwenye next update, ambayo itakuwa ndani ya wiki moja tu hivi.

Lakini kwa sababu hiyo itawasaidia watu wapya tu, ningekushauri uwe mvumilivu. Akaunti yako itakuwa inaongezewa U kidogo kidogo mara kwa mara, na nadhani ndani ya kama masaa 30 hivi itakuwa imefikia 25,000U.

Kama unaswali lingine usisite kulimwaga hapa-hapa JF. Lakini ikitokea una wazo kama hilo la kuboresha UtuExchange, tafadhali limwage hapa:

Feature Requests | UtuExchange Community

Nadhani tupo pamoja.
 
Back
Top Bottom