Karibu UtuExchange!

UtuExchange

Member
Oct 15, 2008
12
0
Karibu UtuExchange

Napenda kukukaribisha UtuEchange.
UtuExchange: Trading on the future!

UtuExchange ni mchezo ambao washiriki mnashindana katika kubashiri matukio ya baadaye. Jinsi ambavyo unabashiri sawasawa ndivyo jinsi unavyoshinda zaidi.

UtuExchange inaendeshwa kwa mfumo wa masoko ya mitaji. Madai ya matukio ya baadaye ni kama makampuni ambayo washiriki wanaweza kuwekeza kwa kununua hisa za matukio hayo.

Mfano wa Dai:
Ndio, kufungiwa kwa MwanaHALISI kutatanguliwa
Will the ban on MwanaHALISI be reversed?

Kama umenunua hisa za dai hilo na MwanaHALISI likafunguliwa kabla ya kifungo chake kuisha, unatengeneza faida, na lisipofunguliwa unakuwa umepata hasara.

Changamoto ni kukusanya faida nyingi zaidi kuliko wengine kwa kubashiri matukio kwa usahihi zaidi kuliko wengine.

Nnapata wapi fedha za kununulia?
Kwenye UtuExchange U ndio fedha yetu. Siyo fedha rasmi ya nchi yako.

Unapojiunga tu unapewa kama 2,000U kama mtaji wako. Unaweza ukatumia mtaji huu kununulia hisa kwenye matukio yajayo.

Na wakati ambapo faida ulizotengeneza hazifikii 25,000U, utakuwa unaongezewa mtaji kidogo kidogo ili uweze kujikwamua. Asiyenacho anaongezewa ... UtuExchange tunapenda haki ... :)

Thamani ya Hisa
Thamani ya hisa katika dai lolote ni kati ya 0U na 100U. Kabla matokeo ya dai hayajajulikana, thamani ya hisa inategemea na walionazo wakotayari kuuza kiasi gani, na wanaotaka kununua wako tayari kununua kwa kiasi gani. Utafanikiwa kununua hisa kama kuna mtu yuko tayari kuuza katika bei unayotaka. Na utafanikiwa kuuza hisa kama kuna mtu yupo tayari kununua hisa katika bei unayotaka.

Lakini baada ya matokeo ya dai kujulikana, thamin ya hisa ni kama hivi:
-Tukio la dai hilo likitokea, thamani ya hisa katika dai hilo inapanda kufikia 100U.
-Tukio lisipotokea, thamani ya hisa inashuka mpaka 0U.

Hisa zinatolewa vipi kwa mara ya kwanza?
Hisa za mdai mapya zinatolewa kwa mara ya kwanza kwa mnada (IPO).

Katika mnada huu, kila mshiriki anasema anataka hisa ngapi na yupo tayari kulipa kiasi gani kwa kila hisa. Huwezi kuona madau ya wengine kwenye mnada huu.

Baada ya mnada kufungwa, nusu ya washiriki watauziwa hisa. Na hawa ni wale walio weka madau ya juu zaidi. Lakini bei watakayouziwa ni bei ya yule aliyeweka bei ya chini kabisa.

Kwa mfano: kama kuna washiriki wanne waliweka madau ya 70U, 60U, 50U na 40U, hisa zitauzwa kwa aliyeweka 70U na 60U, lakini wote watauziwa kwa bei ya 60U.

Ninanunuaje/Ninauzaje hisa?
Baada ya IPO, na baada ya hisa kugawiwa, hisa zaweza kununuliwa na kuuzwa.

Mtindo wa kuuza na kununua hisa unafanana na unaotumika katika masoko ya mitaji.

Kununua hisa, unaweka oda yako ya kununua na kusema namba ya hisa unazotaka , na bei unayotaka kununulia. Kama kuna mtu ambaye yupo tayari kuuza katika bei hiyo, biashara itafanyika na utapata hisa na yeye atapat U zake. Kama hayupo, basi oda yako itasubiri mpaka atakapotokea mtu aliye tayari kuuza katika bei hiyo. Au mpaka utakapo amua kuifuta hiyo oda.

Vivyo hivyo, kuuza hisa, unaweka oda yako ya kuuza. Na oda yako itasubiri mtu aliyetayari kununua katika bei hiyo.

Ninatengenezaje faida?
Unatengeneza faida kwa kununua kwa bei ndogo na kuuza kwa bei ya juu zaidi.

Kuna jinsi mbili.

1. Unaweza kununua hisa na kusubiri mpaka dai litakapofungwa ili likitokea upate 100U. Kama ulinunua hisa kwa 60U, utatengeneza faida ya 40U.

2. Unaweza kununua hisa kwa bei ndogo pale unapodhani bei yake baadaye itaenda juu watu watakapogundua kwamba uwezekano wa tukio hilo kutokea umeongezeka. Bei itakapoenda juu, unaziuza na kutengeneza faida.

Mbona madai yanakuja "dabodabo"?
Kila dai linakuwa na dai lingine moja au zaidi yanayokinzana.

Kwa mfano: kwa swala la MwanaHALISI kuna dai linalosema: "Ndio, kufungiwa kwa MwanaHALISI kutatanguliwa". Lakini pia kuna dai kinzani linalosema "Hapana, kufungiwa kwa MwanaHALISI hakutatanguliwa".

Hii inamruhusu mtu asiyeamini kwenye dai la kwanza kuwekeza kwenye dai linigine ambalo yeye anadhani lina tija zaidi.

Na ni ruksa kufanya biashara kwenye madai yote mawili.

Tuzo
Ukishatengeneza U nyingi, unaweza kuzitumia kujinyakulia zawadi.

Zawadi zitakuwa zinwekwa kwenye orodha ya zawadi mara kwa mara. Na zitakuwa zinatolewa kwa mnada. Anayeweka dau la juu, ndiye anajichukulia. Kwa hiyo jinsi unavyobashiri kwa usahihi zaidi, ndio jinsi unakuwa na U nyingi, na ndivyo unavyojiweka katika nafasi nzuri ya kujinyakulia zawadi.

Na sasa ...
Karibu UtuExchange sasa, na utuonyeshe busara yako katika kubashiri yajayo!

UtuExchange: Trading on the future!
 
Last edited by a moderator:
Afadhali umetoa maelezo ya wazi kabisa. Nilikuwa naulizwa inakuwaje? Sasa wenye maswali bananeni na jamaa hapo!
 
UtuExchange,

Kwanza ahsante sana kwa ufafanuzi.

Umesema huu ni mchezo wa ubashiri katika matukio ya baadaye.

Je huu ni mchezo wa kujifurahisha tu au unalenga kufaidisha watu in real life? Kama ni the latter, mbona sijaona popote exchange rate baina ya UtuEchange currency(U) na Tshs. I mean, kama mshiriki akihamua ku-cash out hizo hisa kwenda kwenye real currency, atawezaje kufanya hivyo?

Kwa kifupi, ni nini hasa lengo la huu mchezo katika jamii yetu?
 
UtuExchange,

Kwanza ahsante sana kwa ufafanuzi.

Umesema huu ni mchezo wa ubashiri katika matukio ya baadaye.

Je huu ni mchezo wa kujifurahisha tu au unalenga kufaidisha watu in real life? Kama ni latter, mbona sijaona popote exchange rate baina ya UtuEchange currency(U) na Tshs. I mean, kama mshiriki akihamua ku-cash out hizo hisa kwenda kwenye real currency, atawezaje kufanya hivyo?

Kwa kifupi, ni nini hasa lengo la huu mchezo katika jamii yetu?

Swali zuri, lazima niseme!

Background
Kwanza naomba nikupe picha kubwa kuhusu huu mchezo maana unaonekana kwamba ni mdadisi na mfuatiliaji mzuri.

Mchezo kama huu uko katika kundi la michezo inayojulikana kama "Prediction Markets". ( Prediction market - Wikipedia, the free encyclopedia - http://en.wikipedia.org/wiki/Prediction_market )

Tunaiita michezo lakini, lakini sio katika dhana ya mzaha. Ni aina fulani ya kukusanya maoni ya watu kuhusu future ya mambo fulani-fulani ya muhimu katika jamii yetu.

Lengo la msingi
Lengo la msingi kabisa ni kujaribu kwa pamoja kubashiri yajayo; au kupata picha ya matukio ya baadaye ambayo hakuna mwenye uhakika nayo. Tafiti zinaonesha kwamba mtu mmoja mmjoa anaweza asiweze kubashiri matukio ya baadaye vizuri zaidi kuliko watu wengi wakiwa pamoja, katika mfumo ambao unazawadia wanaosaidia kubashiri vizuri na kuwawajibisha wanaushindwa kufanya hivyo. (The Wisdom of Crowds - Wikipedia, the free encyclopedia - http://en.wikipedia.org/wiki/The_Wisdom_of_Crowds )

Kujifurahisha inaweza ikawa sababu moja wapo ya mtu kushiriki, na kunasababu nyingine kadhaa mtu angependa kushiriki.

Lakini lengo la msingi ni kujaribu kukusanya maoni ya watu na kupata picha ya wastani kuhusu matukio ya baadaye.

Kwa mfano kama bei ya hisa za tukio fulani ipo juu, inaweza ikawa ni kidokezo kwamba washiriki wa soko wanaamini kwamba tukio hilo linauwezekano mkubwa wa kutokea. Na kama ipo chini ...

Kwa hiyo nisisitize kwamba lengo la msingi sio kumnufaisha mtu. Lengo la msingi ni kubashiri yajayo. Halafu sasa wale wanaobashiri vizuri ndio tunawazawadia kwa sababu ndio wanaotusaidia zaidi kufikia lengo letu kwa kutengeneza mazingira mazuri ya soko.

Na baadaye jinsi soko letu linayokuwa, kutakuwa na aina nyingine za Tuzo. Kwa mfano kwa aliyetengeneza faida nyingi zaidi ndani ya wiki, mwezi, au mwaka, e.t.c. ili mradi tu wabashiri wetu wazuri wanafaidika.

Kwa hiyo zawadi zitakuwepo kwa wanobashiri vizuri zaidi kuliko wengine.

Exchange Rate & "Cashing out"

Kuhusu exchange rate ya currency yetu ya U kwenda kwenye currency nyingine ni kwamba jinsi ya "ku-cash out" ni kwa kushiriki kwenye minada ya zawadi. Kwa hiyo kama tumeweka simu ya 300,000TZS, kwa mfano, madau ya washiriki wa mnada wa simu hiyo ndio watakao determine U ngapi ni sawa na simu hiyo ya 300,000TZS kwa kuweka madau yao. Kama atakayechukua zawadi hiyo atakuwa ametoa 300,000U, basi tutasema kwa wakati huo 1U = 1TZS . Ndio free market inavyofanya kazi mwanawane.

Kwa mfano sasa hivi kuna zawadi ya 100,000TZS cash. Ingekuwa sio free-market tungesema tunaiuza hiyo zawadi kwa kiasi fulani cha U. Kwa hiyo tungekuwa tume-fix exchange rate. Lakini kwa sababu ni free market, wewe ndio utaamua U ngapi ni sawa na hizo 100,000TZS kwa kuweka dau lako la juu ambalo hakuna mtu mwingine anayeweza kulifikia, ama hakuna mtu mwingine anayedhani thamani ya hiyo zawadi inazidi dau lako la U uliloweka wewe.
 
Nimekuelewa.

Sasa ni vipi mtaweza kuthibiti manipulation ya ubashiri? Wasiwasi wangu ni kama mshiriki au baadhi ya washiriki watafanya usanii katika ubashiri ili kujiingiza kwenye draw ya minada ya zawadi.

Mfano, Mheshimiwa Waziri Mkuchika ni memba kwenye UtuExhange: kwenye list ya madai kuna: "Ndio, kufungiwa kwa MwanaHALISI kutatenguliwa;" Na ubashiri wa "Ndio" unazaa faida kubwa (ambako yeye amebashiri hivyo pia). Mh. Mkuchika anahamua kufanya usanii kwa kulifungulia Mwanahalisi katika muda uliowekwa kwenye dai. Matokeo yake anafaidika mno.

Au

Baadhi ya washiriki wanapata "inside information" kuhusu matokeo ya ishu ambayo iko kwenye list. Mfano, dai ni "Simba itashinda mechi ya kesho dhidi ya Yanga kwa bao 2-0." Na kuna washiriki ambao wanajihusisha na club hizo mbili kwa karibu sana, ambao wanapata dondoo kuwa wachezaji wa Yanga wamehongwa ili wapoteze huo mchezo kwa idadi hiyo ya magoli. Matokeo yake wanabashiri hivyo na kujimbikizia mafaida kibao.

Je mnathibiti/mtathibiti vipi kuhusu usanii kama huu?
 
Hahahaha,

Hapo nadhani ToS itabidi ziwe applied... Yani watu flani kwenye swali flani wasiruhusiwe kushiriki kwa sababu maalumu. Mkuu UtuExchange, hapo inabidi utueleze itakuwaje!?

Binafsi nasubiri maelezo yako! QM hapo umenifurahisha kweli!
 
Kaka unaona mbali.

Kwa la kwanza
Hilo hatuna jinsi ya kulizuia.
Kwa maoni yangu binafsi, nadhani kama uamuzi huo umechukuliwa na mtu tu ili ashinde UtuExchange, itabidi wanaohusika na uhakiki au usimamizi wa swala hilo ndio wenye mpira.

Kwa mfano, kama mchezaji wa Simba akijifunga goli ili ashinde UtuExchange, nadhani makocha wake na washabiki ndio wakumhukumu. Sisi hatumo kwa kweli.

Sisi tunaangalia tu: limetokea au halijatokea?

Kwa la pili
Nadhani tungependa sana litokee. Na moja ya effect inzuri ya mchezo kama huu ni kuwafanya hao wenye inside information wazitumie kwenye soko letu na hivyo kusaidia ubashiri wetu. Kumbuka cha msingi ni ubashiri sahihi.

Kwa hiyo kama kuna mtu au kikundi cha watu wanajua matokeo, hawa watu watakuwa tayari kununua kwa bei za juu. Demand itakwenda juu na hivyo bei ya hisa za dai hilo zitapanda, ambayo inamaanisha kwamba uwezekano wa hicho kitu kitokea umeongezeka. Kitu ambacho ndio kweli, ama?

Kwa hiyo insiders tunawataka, na ndio watusaidia kujua ukweli, na tunachotaka sis ni kujua ukweli kuhusu yajayo. Na ukweli ni kwamba michezo kama hii inasaidia saa nyingine kuchokonoa hayo yaliyofichwa. Ambacho ni kitu kizuri, au? Ambao hatuna inside information tunaula wa chuya kwa sababu tunajifanya tunajua wakati atujui ... :)

Kujua mambo
Huu ni kama mchezo wa bahati nasibu, lakini unahitaji ustadi, na kujua vitu. Jinsi ambavyo unajua undani wa swala linalozungumziwa ndio utakuwa mzuri wa kubashiri katika swala hilo. Kama ukidhani unajua halafu ikatokea hukuwa unajua, unapata hasara.

Mfumo huo unasaidia kulazimisha watu kuweka pembeni ushabiki, na kufanya maamuzi kuendana na wanayoyajua kuhusu hilo swala. Insiders wana advantage, na vivyo hivyo watu wanaojua.

Kwa mfano, kwa kesi ya Zombe. Mtua ambaye ameifuatilia kwa karibu hiyo ishu, na anajua sheria angalau kidogo atakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kubashiri sawasawa kama Zombe atakutwa na hatia ama la, kuliko ambaye haifuatilii kiasi hicho, ama haielewi sheria kiasi hicho. Na kama matokeo ya kesi hiyo yashapangwa, mtu mwenye inside information ndio tunamtaka kwa sababu sisi wengine hatuujui ukweli na kunauwezekano mkubwa tukabashiri visivyo.

Kwa hiyo jinsi ambavyo unajua kuhusu ishu hiyo ndivyo jinsi ambavyo unaweza kubashiri sahihi, na wewe ndio inabidi tukuzawadie. Ukiingia kichwa-kichwa unakula hasara.

Manipulation kwa ujumla
Manipulation zinaweza kutokea kama zinavyotokea kwenye masoko ya mitaji.

Kwa mfano mtu mwenye hisa nyingi anaweza ku-force bei ya hisa ya dai fulani kwenda chini kupita kiasi kwa kuuza hisa zake nyingi kwa bei ya chini mno. Au mwenye U nyingi anaweza ku-force bei ya hisa kwenda juu kuita kiasi kwa kununu kila hisa inayouzwa chini ya bei anayotaka yeye.

Lakini tafiti na uzoefu katika masoko ya namna hii zinaonyesha kwamba manipulation kama hizo huwa zinakuwa short term tu, na baada ya mda bei inarudi kwenye equilibrium.

Kwa mfano kwenye uchaguzi wa marekani wa 2004, kwenye soko moja la aina hii (nadhani ni News Future, sikumbuki vizuri), kuna watu walifanikiwa kushusha bei ya "... Bush will win ..." mpaka karibia na sifuri, kutu kinachomaanisha kwamba watu hawaamini kwamba Bush atashinda, kitu amabacho hakikuwa kweli, ila tu ni kwa sababu ya manipulation. Lakini bei zilirudi to equilibrium ndani ya mda si mrefu.

Kunasababu za kichumi (hasa kunapokuwa na free market) na ki-saikolojia kwa nini inakuwa hivyo.

Kwa soko letu changa, manipulation itakuwa inawezekana zaidi mapaka pale watu watakapokuwa wengi.
 
Hahahaha,

Hapo nadhani ToS itabidi ziwe applied... Yani watu flani kwenye swali flani wasiruhusiwe kushiriki kwa sababu maalumu. Mkuu UtuExchange, hapo inabidi utueleze itakuwaje!?

Binafsi nasubiri maelezo yako! QM hapo umenifurahisha kweli!

Hehehe.

Kama nilivyosema, kwa hilo mpira haupo kwetu. Na tukifika huko ... du! ... kweli itakuwa soo ... imagine unamkuta Mkuchika busy kwenye screen yake ndani ya UtuExchange ... anajinunulia hisa ... yuko late kama 5 mins hivi huku waandishi wahabari aliowaita wanamsubiri atoe tamko lingine ... :) Soo ...

Kwa ukweli kwa sasa ni ruksa mtu yeyote kushiriki. Na kama nilivyosema insiders ndio tunawataka mno yani :)
 
........Kwa soko letu changa, manipulation itakuwa inawezekana zaidi mapaka pale watu watakapokuwa wengi.

Maelezo yanajitosheleza.

Labda kaswali kengine kadogooo ka nyongeza: Humu jamvini (JF) kuna tatizo moja sugu sana la memba kutumia majina lukuki. Jina mmoja la pointi, jina lingine la shari, na kadhalika.... Je mnathibiti vipi washiriki wa UtuExchange kuregister more than once? Au na hii ni rukhsa? lol

Ni vipi pale mshiriki mmoja anapotumia majina kedekede kupindisha matokeo ya dai?

Shukhrani.
 
Jamaa anajieleza hadi maswali mtu unakosa!

Mkuu unaua... Una hakika na hili au ni sawa na mdau mmoja humu huwa anaweza kumwita Mwanakijiji kuwa Kuhani na hata Ole kumwita mswahili huku akidai yeye anamjua fika! Niseme ukweli wengi wanaodai haya hawana proof ya uhakika, na ni members wachache ambao wana tabia hii, si rahisi ku-manage majina zaidi ya mawili hasa JF!
 
lol

Watukutu hawakoselani kwenye jamii yoyoye ile.

Haitaruhusiwa kuwa na akaunti zaidi ya moja. Kadri tunavyokua tutakuza technolojia yetu kuboresha game, na pia ku-deal na tabia ambazo si nzuri.

Lakini uzuri wa hii gemu bro utakuja kuuona baadaye. Influence ya watukutu itakuwa inajichuja naturally. Unajua kufanya manipulations na kutengeneza faida ni kazi, inbidi uwe in the know kweli. Pia manipulation inahitaji uwe na salio la maana. Na mara nyingi manipulation zinakusababishia hasara. Hasara itasababisha salio lako kushuka. Na salio lako likishuka uwezo wako wa kufanya manipulation nao unashuka pia.
 
Jamaa anajieleza hadi maswali mtu unakosa!

Mkuu unaua... Una hakika na hili au ni sawa na mdau mmoja humu huwa anaweza kumwita Mwanakijiji kuwa Kuhani na hata Ole kumwita mswahili huku akidai yeye anamjua fika! Niseme ukweli wengi wanaodai haya hawana proof ya uhakika, na ni members wachache ambao wana tabia hii, si rahisi ku-manage majina zaidi ya mawili hasa JF!

Ha ha haa.... mimi nimeandika yanayopigiwa kelele humu ndani na baadhi ya memba....hasa memba mmoja maarufu sana humu huwa haishi kubatiza watu majina ya wengine. Pengine niseme kuwa kuna malalamiko ya kuwa baadhi ya memba wanatumia jina zaida ya moja.....
 
Labda ka-tip kwa wanaojiunga na UtuExchange.

Ukishajiunga unapewa mtaji wa 2,000U. Mtaji huu unaongezeka kigodogo kidogo kila dakika mpaka utakapofika mtaji wa 25,000U.

Usipoutumia mtaji wako, utakwamba kwenye 25,000U. Ukiutumia unaongezwa tena mpaka 25,000U.

Usiuonee mtaji wako aibu. Jinsi unavoutumia ndivyo jinsi unavyopewa.

Ukinunua hisa 5, kwa mfano, mapato ya juu kabisa utapata ni 500U tu. Lakini ukinunua hisa 200, mapato unayoweza kupata ni mitaa ya 20,000U.

Habari ni kwamba kuondoa umasikini, tumia mtaji wako kwa nguvu.
 
Sasa hizo hisa ndio nanunuaje?

Mzee/Bibie hisa zinapatikana kwa njia mbili

Moja: Wakati wa IPO
Wakati wa IPO (Initial Public Offering) ndio hisa zinatolewa kwa mara ya kwanza. Dai likiwa kwenye IPO, unapewa nafasi ya kuweka dau lako (namba ya hisa unazotaka na bei ambayo upo tayari kununulia). Kila mtu mwenye salio la kutosha anaruhusiwa kushiriki kwenye IPO.

Sasa, IPO itakapofungwa, hisa zitagawiwa kwa nusu ya washiriki. Hawa ni wale walioweka madau ya juu kuliko wengine.

Jibu
Kushiriki kwenye IPO:
- Nenda kwenye main page (http://www.utuexchange.com/). Kwenye Kibox cha "Latest IPO's" chagua IPO unayotaka kushiriki. Ukipew list ya madai, chagua dai ambalo unaamini ndio litakalotokea. Kisha utapewa kurasa ya IPO ambayo itakuruhusu kuweka dau lako kwenye IPO hiyo.

-Au nenda kwenye kurasa ya madai (http://www.utuexchange.com/static/Trading.htm), chagua dai linalokuvutia (au kukukera). Ukipewa list ya madai, chagua dai unalofikiri lina ukweli, halafu weka dau lako kwa kuingiza namba ya hisa unazotaka na bei unayotaka kununulia.

IPO ikifungwa, utatumiwa ujumbe kama umefanikiwa ama la.

Mbili: Baada Ya IPO

Baada ya IPO hisa zinakuwa zimeshagawiwa kwa washika dau walioshinda kwenye IPO. Sasa hawa washika dau ndio wanoamua kama wanataka kuziuza hizo hisa kwa wengine ama wanataka kukaa nazo wasubiri faida ya mwisho.

Ukienda ukurasa wa dai ambalo sasa hivi lipo wazi utakuta kuna list mbili
- Hisa Zinazouzwa
- Hisa Zinazohitajika

Hiza zinazouzwa ni hisa ambazo wamiliki wake wapo tayari kuziuza katika bei itakayoonyeshwa. Kama hii list haina kitu basi hakuna anayetaka kuuza.

Hisa zinazohitajika ni hisa ambazo watu wapo tayari kununua katika bei hizo zilizoonyeshwa. Kama list hii haina kitu, basi hakuna anayetaka kununua.

Jibu
Ukitaka kununua hisa, ingiza order yako ya hisa upande wa Hisa zinazohitajika. Hata kama kunaanayeuza katika bei uliyoweka, basi biashara itafanyika automatically, na utapata hisa, yeye atachukua U zako. Kama hakuna, basi oder yako itasubiri mpaka mtu huyo atokee ama wewe uifute.

Ukitaka kuuza hisa, ingiza order yako uande wa Hisa Zinazohitajika. Vivyo hivyo kama yupo aliyetayari kununua katika bei hiyo (au nzuri zaidi kwako), basi biashara yafanyika. Kama hakuna, order yako inasubiri mpaka atokee au uifute.

Tips
Tip: Kama watu hawataki kuuza, jaribu kuwavutia kwa kuweka bei za juu juu kidogo. Wanaweza kushawishika kuuza. Na jitahidi kushiriki kwenye IPO kwa sababu huko ndipo hisa zinatolewa kwa mara ya kwanza.

Tip: Unaweza kuweka order zako na kuja kuziangalia siku nyingine kuwapa wengine muda wa kuziona.

Tip: Kumbuka lengo lako ni kutengeneza faida nyingi kuliko wengine. Hivyo inabidi kununua kwa bei ndogo kadiri inavyowezekana na kuuza kwa bei kubwa kadiri inavyowezekana.

Tip: Kama una hisa ulizonazo ambazo unadhani dai lake halitatokea tena, jitahidi uziuze kabla hazijakudodea. Lakini hakuna mtu atakayekubali kununua hisa za dai ambalo kila mtu anajua halitatokea. Kutatua tatizo hili, fuatilia news za madai yako. Kama ukijua mapema kwa hakika kwamba dai lako halitatokea, pengine unaweza kuwauzia wengine wasiojua hata kwa bei ndogo ili kupunguza hasara yako. Na hiki ni moja ya vitu vinavyotofautisha mchezo huu na bahati nasibu. The more you are in the know the more you win.
 
je usalama wa wale wanaobashiri mambo unakuwaje na ubashiri huu huwa mnashare na watu wowote wale nje ya hapa ?
 
swali la mwisho makato ya kodi yakoje ? mimi nikishinda nalipaje kodi yangu kwa serikali kutokana na mapato hayo ?
 
je usalama wa wale wanaobashiri mambo unakuwaje na ubashiri huu huwa mnashare na watu wowote wale nje ya hapa ?

Kwanza habari za Myakati Mpya (New A..) ndugu yangu :)

Unazungumzia usalama wa aina gani hapa kaka?

Ubashiri wote nia public, hauna siri. Maana bila hivyo ingekuwa vigumu ku-justfy kwa nini flani anongoza au anapata zawadi na mwingine hapati.

Nje ya hapa unaamnisha JF ama? Wana JF na wasio wana JF wote ruksa. Sema kwa sababu hapa ndio nyumbani ndio maana tumeona ni vyema kuwapa wana JF advantage ya information.
 
swali la mwisho makato ya kodi yakoje ? mimi nikishinda nalipaje kodi yangu kwa serikali kutokana na mapato hayo ?

Inanifurahisha kwamba unaipenda nchi yako. Tunahitaji watu kama wewe ambao wanataka kulipa kodi hata kama hawajawekewa manati kichwani.

Lakin, Shy naona hapo tumekuacha kidogo.

Tafadhali, nakuomba, nipo chini ya miguu yako, rudia kusoma post za kwanza. :)

Kwa ufupi ni kwamba fedha tunayotumia pale inaitwa U. Ukiingia tunakupa mtaji wa bure wa kama 2,000U ambazo unazitumia kuanza kununulia hisa za madai unayodhani yana ukweli. Hayo madai yakitokea unatengeneza faida na salio lako linaongezeka. Yasipotokea unakula hasara na salio la U linapungua.

Sasa basi kama wewe ni mzuri wa kubashiri, maana yake salio lako litakuwa liongezeka kwa sababu utakuwa unatengeneza faida kwenye yale matukio unayopatia kubashiri.

Baada ya kutengeneza U nyingi unaweza kuamua kushiriki kwenye zawadi. Zawadi zatolewa kwa mnada. Kwa hiyo utatumia U za salio lako kuweka dau lako kwenye zwadi. Kama hakuna mtu mwingine anaweza kupiku dau lako, basi unakuwa umejichukulia zawadi.

Kwa hiyo chukulia mapato yako ndani ya UtuExchange kama points unazopata unapokuwa unabashiri sawasawa.

Sasa sina uhakika kama serikali yetu inaweza kukubali tuilipe kodi kwa kutumia U, unadhani watazipokea? :rolleyes:
 
Back
Top Bottom