Kabisa mkuu, na ndio maana anasema mtu anapojaribiwa asiseme anajaribiwa na Mungu, maana mtu hujaribiwa kwa tamaa zake mwenyewe. Kwa kiasi fulani sisi wenyewe ndiyo chanzo cha kupata matatizo tunayoyapata, japo yapo pia ambayo huja kwa njia iliyo nje yetu mfano kwa Ayubu.
Ni swali rahisi lakini gumu kwa akili za binadamu.....
Ata kifo Sio kz ya MUNGU! Ni matokeo ya kz ya Dhambi!
Kwahiyo tupotezapo wapendwa wetu tusiseme kz ya MUNGU/Mola ktk mauti!
Sidhani kama nitajibu ikutoshe kuridhisha curiosity yako lakini Mungu kamuumba binadamu perfectly na pia kaumba laws zinazo govern our unirvese kwahiyo kila anayopitia binadamu ni stahili katika path yake. Hakuna linalotokea ukashindwa ku overcome the mechanisms are there mbali ya yote wewe si mwili tu ukiwa unakuwa spiritually yote yatafunuka.Nisaidie kujibu mkuu
Hii hapa mkuuWakuu mkisoma kitabu CHA Yohana Wa kwanza 4:1-21 mtakuta maneno mazito sn juu ya UPENDO.
KM kuna mtu anaweza kuileta Hiyo sura Hapa kiurahisi ITAKUA Vzr sn tukayapitia HAYO maneno ya MUNGU!
Mimi naomba mkuu Ntuzu, Eiyer na Samaritan mpitie thread hii hapa chini iliwekwa hapa jamvini mwaka 2009 na Bazazi. Thread hiyo imechambua kwa ufupi lakini kwa umakinifu ni nini maana ya neno UPENDO.
Ukisoma huko utaona kuwa neno UPENDO lina tafrisi nne tofauti kulingana na mtenda anataka kusababisha nini kwa mtendwa.
Nini maana hasa ya neno Upendo
Hivi neno UPENDO linamaanisha nini hasa? Maana yake ni nini hasa ukizingatia kuwa imesemwa/inasemwa/itasemwa kwamba upendo ndio uhitaji mkubwa zaidi wa Wanadamu. Tangu wanapozaliwa hadi kufa, watu hutamani kupendwa, wanaishi kwa furaha wanapopendwa na hata wanadhoofika na kufa wasipopendwa. Bila shaka, watu huongea sana kuhusu Upendo. Hata hivyo, jambo la kushangaza ni kuwa sio rahisi kuelezea maana ya Upendo. Baadhi ya wachambuzi wamefikia kukata kauli kuwa Upendo unaweza kuonyeshwa tu kupitia matendo.
Kulingana na Biblia, kuna aina nne za upendo. Mosi, ni shauku changamfu, ya kibinafsi kumwelekea mtu fulani; aina ya upendo ulioko kati ya marafiki wa karibu (Yoh 11:3). Pili, Upendo ulioko kati ya washiriki wa kifamilia (Rum 12:10). Tatu, Upendo wa kimahaba ambao mtu anaweza kuwa nao kumwelekea mtu mwingine wa jinsi tofauti (Mith 5:15-20). Mwishowe ni upendo ulio na maana zaidi kuliko hizo aina nyingine tatu. Huo ni upendo mkubwa zaidi kwani huongozwa na kanuni; kanuni zinazofaa-zinazopatikana katika neno la MUNGU (Zab 119:105). Upendo huo, ni kufikiri kusiko na ubinafsi wa kuwafanyia wengine lililo sawa na jema kutokana na maoni ya MUNGU, iwe mwenye kupokea anastahili au la! Zaidi ya yote Upendo huo hauna ubinafsi.
Tunaweza kupata ufahamu wa ndani wa neno hilo kutokana na maneno ya awali (ya Kiyunani) yaliyotafsiriwa "Upendo" katika Biblia (ya Kiswahili). Neno UPENDO linatokana na kutafsiri maneno manne (ndio aina nne za upendo) ya Kigiriki cha mwanzo/awali. Maneno hayo ni;
· PHI·LE´O
· STOR·GE´
· E´ROS
· A·GA´PE
PHILEO: Kitenzi kinachomaanisha kuwa na shauku, kuthamini au kupenda (kama mtu anavyompenda rafiki wa karibu au ndugu). Hutumika mara nyingi katika Agano Jipya baada ya neno Agape.
STORGE: Upendo ulio kati ya watu wa familia moja. Huu ndio upendo ambao Paulo mtume alisema una/utakuwa haba katika siku za mwisho (2Tim 3:3).
EROS: Upendo wa kimahaba kati ya watu wa jinsi tofauti. Upendo huu hautajwi katika Agano Jipya bali katika Agano la Kale (Mith 5:15-20).
AGAPE: Upendo unaoongozwa na kanuni na unatia ndani mambo mengi; unahusisha fikira na una kusudi fulani na hauna ubinafsi. Upendo huu sio hisia tunayokuwa nayo bila kufikiri. Mara nyingi huhusisha uhusiano wa karibu wenye upendo. Agape ndilo neno linaloelezea Upendo kwa njia nzuri zaidi. Aidha kati ya maneno hayo yote kuhusu Upendo; Agape limetumika mara nyingi zaidi katika Agano Jipya.
Kwa ujumla (mara nyingi) aina zote zinastahili na zinabidi ziende pamoja. Mfano: Ni kweli upendo wa kimahaba (eros) una sehemu yenye maana sana katika ndoa zenye mafanikio; shauku yenye kina kirefu na urafiki (philia) huongezeka kati ya wanandani na huimarishwa na upendo (agape) ambao hustawishwa kumwelekea Mungu, Kristo na Jirani Yetu (Zetu).
Kwahiyo, neno hilo (Upendo) ni neno ambalo lime/lina/litatumiwa sana na wanadamu. Ni neno ambalo limeandikiwa vitabu, likatungiwa nyimbo riwaya na mashairi mengi mno. Pamoja na hayo mara/ nyakati nyingine halifafanuliwi ifaavyo/ipasavyo. Ni neno ambalo lime/lina/litatumiwa sana hivi kwamba inaonekana (limeanza) kupoteza maana yake halisi (mfano ushoga, usagaji na ukahaba).
NB: Je wajua kuwa Upendo ndio sifa kuu zaidi ya Mwenyezi Mungu?
Mimi naomba mkuu Ntuzu, Eiyer na Samaritan mpitie thread hii hapa chini iliwekwa hapa jamvini mwaka 2009 na Bazazi. Thread hiyo imechambua kwa ufupi lakini kwa umakinifu ni nini maana ya neno UPENDO.
Ukisoma huko utaona kuwa neno UPENDO lina tafrisi nne tofauti kulingana na mtenda anataka kusababisha nini kwa mtendwa.
Nini maana hasa ya neno Upendo
Hivi neno UPENDO linamaanisha nini hasa? Maana yake ni nini hasa ukizingatia kuwa imesemwa/inasemwa/itasemwa kwamba upendo ndio uhitaji mkubwa zaidi wa Wanadamu. Tangu wanapozaliwa hadi kufa, watu hutamani kupendwa, wanaishi kwa furaha wanapopendwa na hata wanadhoofika na kufa wasipopendwa. Bila shaka, watu huongea sana kuhusu Upendo. Hata hivyo, jambo la kushangaza ni kuwa sio rahisi kuelezea maana ya Upendo. Baadhi ya wachambuzi wamefikia kukata kauli kuwa Upendo unaweza kuonyeshwa tu kupitia matendo.
Kulingana na Biblia, kuna aina nne za upendo. Mosi, ni shauku changamfu, ya kibinafsi kumwelekea mtu fulani; aina ya upendo ulioko kati ya marafiki wa karibu (Yoh 11:3). Pili, Upendo ulioko kati ya washiriki wa kifamilia (Rum 12:10). Tatu, Upendo wa kimahaba ambao mtu anaweza kuwa nao kumwelekea mtu mwingine wa jinsi tofauti (Mith 5:15-20). Mwishowe ni upendo ulio na maana zaidi kuliko hizo aina nyingine tatu. Huo ni upendo mkubwa zaidi kwani huongozwa na kanuni; kanuni zinazofaa-zinazopatikana katika neno la MUNGU (Zab 119:105). Upendo huo, ni kufikiri kusiko na ubinafsi wa kuwafanyia wengine lililo sawa na jema kutokana na maoni ya MUNGU, iwe mwenye kupokea anastahili au la! Zaidi ya yote Upendo huo hauna ubinafsi.
Tunaweza kupata ufahamu wa ndani wa neno hilo kutokana na maneno ya awali (ya Kiyunani) yaliyotafsiriwa Upendo katika Biblia (ya Kiswahili). Neno UPENDO linatokana na kutafsiri maneno manne (ndio aina nne za upendo) ya Kigiriki cha mwanzo/awali. Maneno hayo ni;
· PHI·LE´O
· STOR·GE´
· E´ROS
· A·GA´PE
PHILEO: Kitenzi kinachomaanisha kuwa na shauku, kuthamini au kupenda (kama mtu anavyompenda rafiki wa karibu au ndugu). Hutumika mara nyingi katika Agano Jipya baada ya neno Agape.
STORGE: Upendo ulio kati ya watu wa familia moja. Huu ndio upendo ambao Paulo mtume alisema una/utakuwa haba katika siku za mwisho (2Tim 3:3).
EROS: Upendo wa kimahaba kati ya watu wa jinsi tofauti. Upendo huu hautajwi katika Agano Jipya bali katika Agano la Kale (Mith 5:15-20).
AGAPE: Upendo unaoongozwa na kanuni na unatia ndani mambo mengi; unahusisha fikira na una kusudi fulani na hauna ubinafsi. Upendo huu sio hisia tunayokuwa nayo bila kufikiri. Mara nyingi huhusisha uhusiano wa karibu wenye upendo. Agape ndilo neno linaloelezea Upendo kwa njia nzuri zaidi. Aidha kati ya maneno hayo yote kuhusu Upendo; Agape limetumika mara nyingi zaidi katika Agano Jipya.
Kwa ujumla (mara nyingi) aina zote zinastahili na zinabidi ziende pamoja. Mfano: Ni kweli upendo wa kimahaba (eros) una sehemu yenye maana sana katika ndoa zenye mafanikio; shauku yenye kina kirefu na urafiki (philia) huongezeka kati ya wanandani na huimarishwa na upendo (agape) ambao hustawishwa kumwelekea Mungu, Kristo na Jirani Yetu (Zetu).
Kwahiyo, neno hilo (Upendo) ni neno ambalo lime/lina/litatumiwa sana na wanadamu. Ni neno ambalo limeandikiwa vitabu, likatungiwa nyimbo riwaya na mashairi mengi mno. Pamoja na hayo mara/ nyakati nyingine halifafanuliwi ifaavyo/ipasavyo. Ni neno ambalo lime/lina/litatumiwa sana hivi kwamba inaonekana (limeanza) kupoteza maana yake halisi (mfano ushoga, usagaji na ukahaba).
NB: Je wajua kuwa Upendo ndio sifa kuu zaidi ya Mwenyezi Mungu?
[/B]
Nimeamua kuiweka baisa hapa kila mmoja aione kwa urahisi zidi na nimekuza maneno ili hata wale wenye matatizo ya kuona waisome bila tatizo!!!!!!!
Naona tulikua na wazo moja mkuu.
Kimsingi nashindwa kuutofautisha Upendo na Mungu
Hata basis za upendo tunazipata kwenye neno lake,nje ya hapo hakuna pa kuzipata
Mimi nijuavyo ni kuwa kanuni ya upendo wa Agape ndio upendo halisi,hizo aina zingine za "upendo" mi naona kama sio upendo kwakuwa upendo una kanuni na ikivunjwa kanuni moja tu hapo tayari unakuwa sio upendo
Kanuni kubwa inayoamua kipi kiwe upendo na kipi kisiwe ni kutokuwa na masharti,ukishaweka masharti au sharti unakuwa sio upendo ndio maana nikasema kuwa huo upendo mwingine ni kama sio upendo kwasababu umevunja hiyo kanuni kuu
Ukishaanza kusema nampenda fulani kwasababu ni mke wangu au rafiki huo sio upendo
Hutakiwi kuwa na sababu ya kumpenda mtu,wewe unapenda tu!!!!!!!
Huwa mara nyingi napenda kutoa maoni yangu binafsi, kutokana na uzoefu na kiwango cha maisha ambayo nimeyaishi hadi wakati huu. Kwa hiyo huenda yasiwe kwenye mfumo rasmi wa ki shule au kitaalam japo yanawakilisha nnachokiongelea kwa wakati huo.
Tukija kwenye suala la mahusiano ya kawaida, huwa mara nyingi nawaambia watu upendo ni kitu cha kufukirika na kukitengeneza wenyewe. Leo hii naweza kuwa kusema Eiyer ni rafiki yangu na nampenda kama rafiki tuchukulie mfano tunafanya nae kazi ofisi moja.
Siku ikatokea rafiki yangu Eiyer akamwambia bosi wetu watu8 tuhuma za uongo juu yangu na nikapata misuko suko kazini, huenda huo ndio ukawa mwisho wa urafiki na upendo niliokuwa nao kwa Eiyer kama sio kuleta msukosuko kwenye huo urafiki wetu kama utaendelea kuwepo.
Mfano wa pili,
Kwa wale wenye mahusiano, leo hii mtu anaweza kusema anampenda mtu mwingine kiasi cha kfikia maamuzi ya kuishi pamoja, lakini ikajatokea mmoja wao akapata taarifa ambazo hakuzijua hapo awali, kama ni taarifa nzuri, upendo huongezeka na kama ni taarifa mbaya, ule upendo hugeuka chuki. Na hapo ndio najiuliza, tunapenda mtu au tunapenda sifa za mtu? Haiwezekani leo unasema unampenda mtu kisha kesho useme humpendi baada ya kusikia kwamba aliwahi kutoa mimba.
Hitimisho langu, upendo wa agape kama alivyouelezea Bazazi ndio hasa tunaotakiwa kuutafuta na kwa mtazamo wangu, Mungu anatujalia na kutuwezesha kuwa na huo upendo.
Kwangu binafsi tangu nikiwa shule, niliamua na kuweka msimamo kwamba sitakua na mahusiano yanayopelekea zinaa na msichana yeyote niamini kwamba sitakua nampenda kwa sababu kwa wakati huo, hicho tunachokifanya kwa upande mmoja ni kumharibia mipango yake tu na kama kweli nampenda sitakubali kumharibia mtu future yake.
Aina hii ya upendo nasema ni lazima Mungu akujalie kwa sababu hauhesabu mabaya, wakati mwingine inabidi uingie hasara au gharama na wakati huohuo ujisikie vizuri na fahari kutimiza aina hiyo ya upendo. Laiti tungekua na upendo huo, matatizo mengi sana yangepungua kwenye jamii kama sio kwisha. Pasingekua na sababu ya kudhulumuana, kuuana, watoto wasio na mtaani, Chuki kwenye jamii na familia zetu, rushwa na yanayofanana na hayo.
Kwa ujumla upendo una maana nyingi kwa watu tofauti kulingana na wao wanataka au wanahitaji nini na mara nyingi umechanganywa na tamaa, uchu, hadaa na ubinafsi.
Narudia tena upendo wa aina hiyo usiolipiza baya, usiohesabu mabaya ni lazima Mungu akujalie kwa sababu Mungu ni Pendo na kwa kuwa yeye ndio chanzo na asili ya huo upendo, hauwezi kupatikana nje ya yeye.