nickname
JF-Expert Member
- Dec 20, 2009
- 544
- 151
:welcome:CITY DREAM LODGE
MAHALI ILIPO: Morogoro mjini eneo la Vibandani ukiwa unaelekea Chuo Kikuu cha SUA, karibu kabisa na 'Dolphin Inn'. Kutoka soko kuu la mjini Morogoro au benki ya NMB, haizidi kilometa moja ndani ya mji.
SIFA: Ni nyumba za kulala wageni mpya iliyoanza kazi tarehe 30 Machi 2015. Ni yenye ukimya na utulivu wa kutosha kukiwa na: Self-contained & Executive Rooms, TV, Feni, AC, Simu, Break Fast, Vinywaji, Mgahawa, Parking na Bustani. Maji ya moto ya kuoga yapo pia
MAPOKEZI: Mapokezi ni mahali ambapo mteja anaweza kupumzika na kuangalia TV akiwa anajisajili na kujiandaa kuelekea katika chumba chake.
VYUMBA: Vyumba ni vipana na vina meza ya kufanyia kazi, sehemu za kuwekea begi na viatu, na pia kuna vitanda, meza na magodoro vyenye mvuto wa kipekee. Pia vyumba vina TV, feni, simu, choo na bafu na AC kwa baadhi ya vyumba. Mteja anaweza kuomba huduma yoyote pamoja na kuagiza kinywaji chochote akiwa chumbani.
CHAI YA ASUBUHI: Huduma ya chai na vitafunwa inatolewa ‘restaurant' kila siku kuanzia saa 1 hadi saa 3 asubuhi kwa ajili ya wageni tu.
HUDUMA NYINGINE: Huduma nyingine ambazo zinatolewa kwa malipo ya kawaida ni kufua na kunyoosha nguo.
USALAMA: Lodge imezungushiwa ukuta wenye usalama wa kutosha kumuwezesha mteja kuingia na gari. Pia kuna ulinzi wa kutosha kwa masaa 24.
BOOKING: Ukihitaji kufanya booking tumia simu hizi tatu za mapokezi ambazo ni: 0759 116611 / 0657 863129 / 0789 486411. Unaweza kukilipia chumba chako kabla ya siku ya kuwasili. Tafadhali kwa maelekezo zaidi piga simu mapokezi.
MOTISHA KWA MTEJA AKAAYE MUDA MREFU: Mteja akikaa siku saba (7) mfululizo, siku ya nane atalala bila malipo yoyote – yaani ni motisha kwake. Itaendelea hivyo kwa kila baada ya siku saba saba.
BEI YA VYUMBA: Bei ya vyumba nikati ya sh. 20,000/= hadi sh 40,000/= kwa siku moja, kufuatana na aina ya chumba. Bei zinaweza kubadilika kutokana na ongezeko la gharama za uendeshaji.
KUMBUKA: CITY DREAM LOGE ni mahali pazuri kufikia penye hadhi. Watu wanaohitaji utulivu wa hali ya juu ili waweze kupumzika au kufanya kazi zinazohitaji kutafakari na kufikiri kwa undani, hapa panakidhi hali hiyo. Hivyo, naomba taarifa hii uwapatie pia maafisa/ wafanyabiashara wengine, ndugu, jamaa na marafiki.
KARIBUNI TENA Morogoro na tuwe wote hapa CITY DREAM LODGE. Asanteni sana.
Kwa maulizo yoyote yale, wasiliana na:-
Fred Sichizya
Mkurugenzi
City Dream Lodge (CDL)
Simu: +255 762650377 | +255 655524287
E- mail: fredsichizya@gmail.com