Kwanza nakupa pole kwa kuzama humu ndani.Ili uishi kwa amani humu jela inahitajika sana nguvu yaani uwe umetuna kifua au unapiga sana karate na Kung fu maana humu ndani sikufichi kuna mwamba na miamba we umekuja leo sasa utakutana na wenzako wako miaka na miaka. Tena kuna mamafia kichizi acha mchezo kabisa.
Yaan ukiingia leo tu utatamani utoke hata kesho.utakuja na pingu ukifikishwa utashangaa huoni kingine zaidi ya ukuta mkubwa na mawingu.ndani ya jela hutamkuta bishoo kila mtu sura ya kibandidu.kiufupi utaomba kwa MUNGU wako ardhi ipasuke na haitapasuka hata ukisali usiku kucha Hadi pakuche asubuhi. Jamaa yangu maisha ya jela ni ya kibabe mixer kuchezea vitasa na kumwagika supu(damu).Ndo hivo tena ushaingia ndani nakusihi tu mwombe MUNGU utoke salama maana huku sio mwisho wa maisha. Karibu jela.
Ndani utawakuta machizi wamepinda kama ile dawa ya mbu ya kuchoma ile ya kijani na ukizingua tu ma Port askari jela wanagawa sana marungu.Usionyeshe sura ya upole sana kaza sura mzee baba ukishangaa shangaa hata msosi hupati maana msosi ni wa foleni na yule mbabe ndo wa kwanza anaanza kula.
Nimeshakwambia ukiishi kinyonge imekula kwako maana polisi hawana cha mswalia mtume wala kristo wamebeba tu ma AK 47 kiufupi huwezi ku-escape, ukijaribu unakula pisto.Ukiingia umeingia hutoki kesho wala kesho kutwa kama una lengo kichwani hilo lengo futa hutoki
Mwisho kabisa acha kulialia hata kama umebambikiwa kesi maana MAJI YAKISHAMWAGIKA HUWA HAYAZOLEKI.
KARIBU JELA