Karata ya kufunga Strait of Hormuz na kuishiwa Interceptors za ulinzi wa anga vyamtisha Trump na kutaka ceasefire.

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
16,817
Reaction score
62,027
Kwanza nataka nikiri kuwa wazungu ni wajanja. Wao huwa wanaact kwa mtindo wa good cop vs bad cop. Safari hii Marekani na Israel walikuwa bad cops huku Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zikijifanya kama ziko mbali lakini behind the scenes wako pamoja.

Leo Trump ametangaza ceasefire kati ya Israel na Iran, lakini kuna mambo yamechangia kufikia hapo.

1. Mosi hofu ya Iran kufunga strait of Hormuz kiukweli kabisa ndiyo iliyokuwa game changer. Hii ingeumiza uchumi wa Marekani, dunia, na lawama ya dunia nzima ingeenda kwa Marekani

2. Pili Interceptors za Israel kuzuia makombora ya Iran zilikuwa zimeanza kuisha, maana yake ni kwamba Miji ya Israel ingeendelea kupondwa na missiles za Iran

3. Camp ya MAGA kule Marekani, ambayo ilimchagua Trump kwa hoja ya kutoiingiza marekani ktk vita huko middle east ilikuwa imeanza kuchachamaa, Wananchi wa Marekani walianza kumiminika mitaani kupinga vita.

4. Lakini pia huenda ilikuwa ktk plan za kivita za Israel na Marekani kuwa wakishamaliza kulipua vinu vya Nyukilia na kupiga targets kadhaa za kijeshi ndani ya Iran basi waanze de-escalation process. Yaani waanze sasa diplomasia na Iran kwa sababu baada ya kulipuliwa vinu vyake, Iran haitokuwa na bargsining power ya kutosha.

Kiufupi: Iran imejitahidi sana kwenye hii vita, ilishtukizwa, ikauliwa makamanda wake, ikafanikiwa kuficha Uranium yake na baadhi ya mitambo muhimu ya kuenrich Uranium. Ikajiorganise, Ikaanza counter attacks ambazo nazo zimeiumiza Israel kwelikweli.

Israel ilizoea kupeleka kichapo kwa wengine, Leo na yenyewe imeshuhudia miji yake ikichakazwa, nadhani sasa itajifunza kuwa Vita vina consequences.
 
Vema sana
 
USA muongo muongo, unaweza kuta hapo kuna kitu anavizia aje amtwage Iran
 
Iran asikubali huu ujinga israel haijawahi kuheshimu makubaliano yoyote angalia hisbullah na hamasi mtu mwene historia kama hii unaanzaje kukaa naye mezani .. kesho anakushambulia halafu west wanakuja kumlinda israel has right of self defence
 
Iran asikubali huu ujinga israel haijawahi kuheshimu makubaliano yoyote angalia hisbullah na hamasi mtu mwene historia kama hii unaanzaje kukaa naye mezani .. kesho anakushambulia halafu west wanakuja kumlinda israel has right of self defence
Iran analijua hilo,ndio maana akasema kuwa Israel aki act yeye ata react baada ya kushambulia Beersheba usiku kuamkia leo.
 
Iran asikubali huu ujinga israel haijawahi kuheshimu makubaliano yoyote angalia hisbullah na hamasi mtu mwene historia kama hii unaanzaje kukaa naye mezani .. kesho anakushambulia halafu west wanakuja kumlinda israel has right of self defence

Umeongea ukweli. Ukiona Israel inaomba ceasefire, basi ujue hiyo ni tactical retreat ili wafanye assesments wajipange upya warudi tena.
 
Iran inabidi aendelee kusukuma moto tu
 
Nilikuwa najua hii ngoma zinapigwa hadi Ayatollah anang'olewa sasa kama habari ndiyo hizo mambo yatakuwa ni yaleyale tu.
Wanaipa tena Iran muda wa kujipanga na kuendelea na mambo yake ya kufadhili magaidi na kuandaa nyuklia.
Wataanza na kushughulikia mifumo ya ulinzi kwa kushirikiana na Russia .
Iran wanatakiwa wampindue Ayatollah na kubadiri mfumo wa uongozi na waachane na habari ya kuwatetea wapalestina kwani dunia nzima imewaacha, wao wafanye mambo yao
 
So unadhani ni rahisi ??
 
Kwanini iwaache Wapalestina?.
 
Huu ndio ukweli
 
Umechambua vizuri sana! Yote uliyoandikwa yamekuwa yakijadiliwa katika media mbali mbali za kimataifa.
Lakini kubwa ni hilo la Israel kuishiwa air interceptors! Vinginevyo kwa jeuri ya Israel ingeendelea kuiponda Iran.
 
Kwanini iwaache Wapalestina?.
Kuitetea palestina kutaigharimu Sana Iran.
uingereza, marekani, ujerumani, ufaransa na mataifa mengi ya ulaya wanaiunga mkono Israel sasa kama waarabu wengi wameiacha palestina kwanini Iran aumie kwa ajili ya palestina?
 
Kuitetea palestina kutaigharimu Sana Iran.
uingereza, marekani, ujerumani, ufaransa na mataifa mengi ya ulaya wanaiunga mkono Israel sasa kama waarabu wengi wameiacha palestina kwanini Iran aumie kwa ajili ya palestina?
Hio ndio tofauti sasa ya Iran na West+USA.
 
Yaani hapa Israel ameishapata ugumu na hatoweza tema kuja kuivamia Iran kwa sababu, Iran itajipanga zaidi ya hapa. Kwa mfano, Putin alitaka kumpa Iran ulinzi wa anga mapema kabisa lakini Iran alitakaa, kwahiyo safari hii lazima watajiimarisha na washirika wake!
 
IRAN aikuwa na chaguo zaid kusitisha Vita pale Iran kwanzia kesho kutwa kuna shughuli ya kidini kubwa sana yani Muraham ndio unaanza 26/06 Israel na Marekani walipanga mipango yao kwa Akili sana..

Iran kipindi ichi inapokea Waumini wengi sana kutoka nchi mbalimbali za Dunia ivyo nayo Iran kipindi ichi inapata pesa nyingi sana kwaiyo wamechagua Aman ili pia Shughuli yao ya Dini iyendelee kwa Aman.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…