Karaha ya kuwadai waliokukopa

Karaha ya kuwadai waliokukopa

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,395
Reaction score
13,272
Katika biashara au maisha kukopa na kukopesha ni mambo ya kawaida. Na kwa kawaida wakopaji huwa na lugha nzuri na laini wakati wa kukopa ikiwa imesheheni ahadi tele za kulipa mapema bila usumbufu. Jambo la ajabu wengi wao wakishafanikiwa kupata mkopo hawatimizi ahadi zao na sasa kazi inakuwa kwa mkopeshaji kuanza kumtafuta mdaiwa na kudai deni. Mimi katika shughuli zangu nimekumbana na kauli za hovyo na zisizo za kistaarabu kutoka kwa wadeni wangu na sijui kwanini wakopaji huwa wakorofi na wakali wanapodaiwa. Huenda na ninyi wenzangu mmekumbana na hali hii Mfano baadhi ya kauli nilizokumbana nazo wakati nikiwadai wadeni wangu ni kama:

1. Nitalipa tu mbona hata serikali inadaiwa sembuse mimi?
2. Usinitishe na vijihela vyako uchwala kwani unafikiri ndio vinavyoniweka mjini?
3. Yaani vijisenti hivyo ndivyo vinavyokufanya uje kunigongea mlango?
4. Wangapi wanadaiwa bwana?
5. Nitakulipa nikipata!

Sasa ukiwapigia simu wengine hawajibu au watakwambia wako safarini mara Arusha ,Mwanza, Songea mara wengine wamefiwa ili mradi sasa inakuwa matanga wakati wa kukopa ilikuwa harusi. Wakopaji acheni hizo!
 
Usinilize! Kuna jamaa yangu nilimkopesha kirafiki (ni jamaa yangu tangu tukiwa Sec.), yupo mji tofauti. Amekuwa akinipiga laenda kwa simu. Kwa sasa nikipiga simu, kila mara, network operator inaniambia "you are not authorised to contact to this number, contact your customer service". Bado sijafanya hivyo.
 
Yani hii kitu mbaya sana watu hawana ustarabu ndo maana. Ni kweli mdeni anaweza kuwa na sababu ya msingi tu ya kutolipa kwa muda ila kinachomfanya awe mngwana na mstarabu ni kutoa taarifa kuwa kakwama hapo ndo wengi hushindwa kuwa waaminifu...
 
Ndugu siku hizi km unataka kuwapunguza marafiki jaribu kumkopesha hela kuanzia laki utapigwa kalenda mpaka ukome yaani kwa maisha ya leo bora umkopeshe mamayako au baba hata asipokulipa haisumbui watu wamebadilika sana.
 
Roho inaniuma nikiyazungumzia haya dahr.mara nyingi huwa na mm nakopa kwa kukwamishwa na watu niliowakopesha.
yaani kuna mtu anatakiwa akulipe akianza kukupiga kalenda anakufanya na ww unaishiwa unakopa sehemu nyingine.
hii nimeisoma nikaona kuna mzunguko mkubwa sana hapo na kama haupo kwa mzunguko huu huwezi kwenda
 
Mimi sasa nimekata shauri si mkopeshi mtu tena.Lakilaki nilizokopesha nyingi, hamsini kibao, elfu kumi ya karibu nakupa baada ya nusu saa nazo usiseme. inayoniuzi ni ya hivi karibuni, nilikuwa na akiba yangu ya kumlipia mwanangu karo ya shule. Akaja jamaa yangu tumeshibana sana akaniomba nimkopeshe laki moja kwani alikuwa na tatizo kubwa sana na angenirudishia mwisho wa mwezi. Kutokana na tatizo alilonieleza nikampatia. Mwisho wa mwezi ulifika akanambia nimvumilie mwezi huo mambo hayajakaa sawa. Baada ya hapo kimya; nimemtumia salamu ya mwaka mpya kanijibu tumemaliza na kuanza mwaka salama. Nikalazimika na mimi kwenda kukopa ili kulipa karo ya mtoto. kwa kweli huu si uungwana kwani nilimwambia toka awali kuwa hii ni akiba niweka kwa ajili ya karo ya mtoto.:angry:
 
Kweli maneno ya wahenga hayaanguki chini
' kukopa arusi kulipa matanga'

Wengi tunalizwa kwa imani zetu, mtu unamdai na jeuri juu.
 
Kweli binadamu kukopa kwao laisi but kulipa Deni sasa hapo kazi IPO kulipa
 
Jaman hiyo issue ni balaa.. nilidhani ni kwangu tu kumbe wengi yamewakuta??? Mimi nimeamua simkopeshi mtu kiasi ambacho kitaniumiza baada ya kutolipwa, maana angalia kama huyo mdau hapo juu amekopesha hela ya ada halafu jamaa halipi!!! 😱
 
Tunatofautiana sana....binafsi nikikopwa sina amani mpaka nirudishe hela ya watu...
 
Back
Top Bottom