Karagwe FFU wanawapiga mabomu wananchi ambao wamelizingira jengo la Halmashauri hapo Kayanga. Hali ni tete sana na Wananchi hawa hawajazoea Mabomu. Taarifa za ndani ya Tume hapo Kayanga zinasema CCM na Blandes lazima watangazwe washindi kwani wanadai kuwa namzidi mgombea wa CHADEMA kwa kura 6500. Mgombea wa CHADEMA anadai kuwa wamemzidi wa CCM kwa kura 550. Hakuna anayekubali kushindwa. Polisi wameona ni heri watumie nguvu ili mradi Blandes wa CCM ashinde.