Kapuya aburuzwa polisi

Kapuya aburuzwa polisi

palalisote

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2010
Posts
8,335
Reaction score
1,462
  • Binti anayedaiwa kubakwa ahojiwa siku mbili

HATIMAYE binti anayedaiwa kubakwa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), amefungua jalada Polisi dhidi ya mbunge huyo.

Habari za kipolisi ambazo gazeti hili limezipata, zinasema kuwa binti huyo ambaye anadai kubakwa na kisha kutishiwa kuuawa na Profesa Kapuya, amefungua jalada namba OB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Harakati za kufungua jalada hilo zilianza juzi jioni na kuendelea hadi jana ambapo polisi walitumia zaidi ya saa 12 kumhoji binti huyo anayedaiwa kubakwa ili kupata ukweli wa sakata hilo.
Akiwa kituoni hapo, binti huyo alikutana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi ya Oysterbay (OCD) na OC-CID wake na kutoa maelezo ya awali kabla ya viongozi hao kumruhusu ayaweke malalamiko yake katika maandishi kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alikiri polisi kufungua jalada hilo na kuongeza kwamba hivi sasa wanafanya uchunguzi kubaini kama ujumbe ulio katika simu ya binti anayedai kubakwa na kutishiwa maisha unatoka katika simu ya mbunge huyo.
“Tumefungua jalada, lipo kwa ajili ya uchunguzi na tukibaini kuwa ni nani anahusika na tuhuma hizo tutamsaka na kumkamata popote alipo,” alisema Wambura.
Habari zaidi zinasema polisi wamechukua namba ya Kapuya inayodaiwa kutumika mara kwa mara kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa binti huyo, akitishiwa kuuawa.



http://www.freemedia.co.tz/daima/kapuya-aburuzwa-polisi/
 
Ngoja tuone kama katika hili Polisi wata react!
Speed hii ya utendaji kama ingelitumika kwa wananchi wote basi Ng. Lwakatare asingelipata mateso yote aliyopata. Ni mawazo tu.
 
Hii wameanza na kuchunguza kama kweli ujumbe umetumwa kweli ila wengine ni ndani kwanza halafu source ya Habari za nani aliweka YOUTUBE baadae. Loh!!!
 
"Tumefungua jalada, lipo kwa ajili ya uchunguzi na tukibaini kuwa ni nani anahusika na tuhuma hizo tutamsaka na kumkamata popote alipo," alisema Wambura.

He, mbona kauli yenyewe ni kama tayari inasema mhusika sio KP!!!
 
ngoja niangalie kinachoendelea
 
Uchungzi huu huenda ukachukua muda mrefu sana mpaka prof.KP atakapoteuliwa kuwa PM basi, na uchunguzi unaishia hapo.
 
hapa hutapata wachangiaji kwani Lumumba timu haipendi kabisa uzi kama huu , sasa hivi wanahangaika na puppet wao Zito.
 
Kama binti ameweza kuhojiwa kwa muda wa masaa 12 basi kesi ikifika mahakamani itachukua zaidi ya miaka 3.
 
Habari ya mujini ni zitto and his end in politics, mambo ya wapendanao wasubiri valentine
 
Jamani haya hamuachi kuyajadili mumwache kapuya apumue tuhamie kuyajadil ya zito na kitila mkumbo
 
Kama binti ameweza kuhojiwa kwa muda wa masaa 12 basi kesi ikifika mahakamani itachukua zaidi ya miaka 3.

Mkuu hii ndiyo tz!! Mlalamikaji kawekwa NDANI kwa mahojiano kwa zaidi ya saa 12! Na mwisho polisi wakaishia KUKAMATA namba za simu ya mtuhumiwa!! Mtuhumiwa mwenyewe bado tunamnyemelea ageuke pembeni tumdake!! Huyo binti ana hakika hapo alipoenda kufungulia file ni polisi?? Isijekuwa post traumatic stress disorder zimempelekea kuingia kilabu cha mbege na kudhani ni polisi central,wauza mbege nao siku hizi wanavaaga makofia flani hivi.
 
Back
Top Bottom