Kapu la Babu na baba zangu

Kapu la Babu na baba zangu

usinijibu hivyo

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2017
Posts
248
Reaction score
329
KAPU LA BABU LINA VUJA...USIJIDANGANYE.

Tulikuwa na babu yetu Wa miaka 116,wajukuu tulikiwa 52,utaona ukubwa Wa familia kijijini.

Baba alikiwa mkali Sana akiwa kama msaidizi Mkuu Wa Babu.

Alituongoza kwa namna njema sana watoto wake na vitukuu vyake.

Alitulipia shule,Matibabu maji na asubuhi chai ya Maziwa.
Lakini ilitupasa kuhudumia ng'ombe zaidi ya 1000 za babu
Kulinda Mashamba nakadhalika.

Baba alikuwa Mkalai Sana tukifanya uzembe kama vijana ama watoto.usalama wetu ulikuwa ukikosea ni kuwahi kwa babu.kutokana na umri Mara zote alitutetea"Wakikua wataacha..'baba huku akihema ameshikilia kiboko kwa hasira.

Familia ya watu 87 huko mlolanguru Tabora tuka kubaliana tukae tuwe na utaratibu huru watoto,baba,wajukuu,vitukuu na Vilembe...Kutoa maoni yetu.

Jirani yetu kulikuwa na Mzee anaeheshimika Sana JOHNSON FERDNAND Wa Huru.

Tukakubaliana kuweka kikapu nyumbani kwake tuwe tunatumbukiza karatasi za Maoni yetu na Sharti asije akamwambia baba ninani katumbukiza maoni siku ya Jumapili baada ya Kutoka Kanisani...

Basi baba zetu baadhi maana walikuwa 11 wakaanza kuitamani nafasi ya baba ya kumsaidia babu bila utaratibu wakawa wanaweka maoni yao mengi Sana.

Kwa Mamlaka ya baba na uhasibu Wa fedha za kilimo alizokuwa nazo akamwajiri kwa siri Mtoto Wa Mzee Johnson na kumlipa kila mwezi ili ajue waweka maoni Mara kwa Mara..

Tulishangaa kila kikao baba anajua njama na mipango kwa majina ya wasiounga mkono maendeleo ya Familia....
Babu alikuwa akimpa Moyo wakati wote"Hata Mungu apendwi na wote..."
Wajukuu tuliostuka tukawa makini sana na kapu la babu,tukiwaangalia kwa jicho la Makengeza baba zetu ambao kila wakiwa na jambo wanakimbilia kwenye lile kapu kuweka maoni kwa lugha ikiokuwa mbaya Sana.....Sana.

hadi kusoma hizo meseji wakati wakikao ilikuwa shida...

Nimesafiri nje kimasomo mwaka wapili sasa naambiwa kule home kapu limekuwa kubwa kiasi hadi wanakijiji wanaweka maoni yao ili yafike kwa Babu ambae ni Chief ili nae ayafikishe serikalini.kwani wanamuamini Sana.

Ila hawajuhi ile siri ya yule kijana anaelipwa na baba wakumwambia watoa maoni.
"Toeni Maoni yenu kwa busara'"
Kila Mara najishauri ni mwambie babu ama la?
Nitaaminika?
Ushahidi utakuwa nini?
Sitatukanwaa?

Lakini utajiri Wa mtoto Wa Johnson Ferdnand hauwastui tu?.(NAJIULIZA)

Naombeni mawazo.
 
Huyo mtoto juzi nilimuona akijipitisha pitisha kwenye hafla moja hivi? Lakini naamini baba ako atakuja kuchokwa tu. Halafu baba zako wengine 11 watafunguliwa kesi ya wizi wa mifugo, huenda hilo likapelekea kutengwa na ukoo.coded message
 
Hahaaaa mzee Johnson Ferdinand hawezi kuvujisha siri kwa baba kichaa. Ila ipo siku babu atamchoka baba kichaa atamcharaza bakora mbele ya watoto,wajukuu,vitukuu
 
Hukumu ya hivi karibuni kwa Mzee JOHNSON FERDNAND na kutakiwa alipe faini ni Mchezo wa Kuaminisha kama Tupo salama Kapuni.TUCHUKUA TAHADHARI KWA MAISHA YAKO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom