Kapombe asaini azam fc miaka mitatu

Kapombe asaini azam fc miaka mitatu

cnjona

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2014
Posts
1,027
Reaction score
239
http://2.bp.blogspot.com/-jreaL3HN9X4/U4dom--E6fI/AAAAAAAA-sw/mE5nub2ds_I/s1600/bocco+na+kapombe.jpg
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
HATIMAYE klabu ya Azam FC imefanikiwa kumsajili, beki anayeweza kucheza nafasi za kiungo pia, Shomary Salum Kapombe baada ya jana kumsainisha Mkataba wa miaka mitatu.
Katibu wa Azam FC, Nassor Idrissa Mohammed ‘Father’ ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, wamefuata taratibu zote kabla ya kumsainisha mchezaji huyo, na kufanikiwa kumalizana na klabu yake, AS Cannes ya Ufaransa.
“Kama inavyofahamika, mchezaji huyu alihamishwa kutoka Simba SC kwenda AS Cannes mwaka jana, kwa hivyo nasi tumemsajili kutoka timu hiyo, lakini asilimia fulani ya fedha, ambazo tutawalipa Simba SC,”amesema Nassor.
Maisha mapya; Shomary Kapombe kulia sasa ni mchezaji wa Azam FC

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema; “Hatuna tatizo na Kapombe, awaambie Azam FC walete asilimia 40 yetu katika fedha walizotoa kumnunua huko Cannes, na sisi tutanunua wachezaji wengine wazuri tu hata wawili kwa hiyo fedha,”.
Tayari Kapombe alikuwa amekwishajiunga na Azam FC tangu Machi mwaka huu baada ya kugoma kurejea Ufaransa tangu Novemba mwaka jana aliporejea kuichezea timu ya taifa, Taifa Stars mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe.
Kapombe aliyezaliwa Januari 28, mwaka 1992 aliibukia katika timu ya vijana ya Polisi Morogoro kabla ya kusajiliwa na Simba mwaka 2011, ambako alicheza hadi Agosti mwaka jana alipojiunga na Cannes.
Tupeni Chetu; Hans Poppe anataka Simba SC ipewe mgawo wake isajili wakali wengine

Simba SC ilimtoa mchezaji huyo bure AS Cannes kwa makubaliano akiuzwa klabu nyingine, itapata mgawo mzuri.
Hata hivyo, baada ya kugoma kuendelea kuchezea klabu hiyo ya Daraja la Nne, Simba SC ilitakiwa kulipa Euro 33, 000 ambazo sawa na Sh. Milioni 66 ili kurejeshewa mchezaji wake huyo.
Kapombe anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na mabingwa hao wapya wa Ligi Kuu, baada ya beki Abdallah Kheri kutoka Zimamoto ya Zanzibar kiungo Frank Domayo na washambuliaji Mrundi Didier Kavumbangu kutoka Yanga na Ismaila Diarra kutoka Mali.
 
Kila siku tunasema tatizo la wachezaji wa bongo ni kutojitambua ukichangiwa na upeo wao wa kielimu kuwa mdogo,hivyo kushindwa kuwa na watu makini wa kuwashauri,we kwa mtu aliyomakini unaacha fulsa ya kucheza ufaransa hata kama ni timu ya daraja la nne,we unakuwa na akili yako kichwani kuwa hiyo ni njia tu,unarudi kucheza huu mpira wa bongo uliojaa mizengwe na fitina ambazo ktk maisha yako ya mbeleni hayana faida yoyote!!!usiwaone hao wachezaji wa Africa magharibi wanacheza virabu vikubwa ulaya ukipata historia zao utajua walikuwa wanamalengo gani,mtu anakuwa analipwa hela ya chakula tu na nyumba anajitolea kwa moyo wake wote.Hata sasa wakenya wameanza kutuacha hawa waki bongo wanataka watoke hapa wakacheze man utd,chelsea,barca!!!!mtasubiri sana.Na ndio maana wachezaji wanakuwa na japo washauri kama sio mameneja waliosomea fani husika,wanaokuwa mbele kumtafutia timu na kumshauri mchezaji pindi fulsa ikitokea,Ndio yale yale ya mrisho Ngasa kipindi kile wasudan wanamtaka.we mshauri wako awe mZee akili mali kuna nini hapo??ndio maana mnakuja na mambo ya kufikitika ohhoo jina la Taifa stars sio zuri eti halimtishi mpinzani linatakiwa jina kama indomitable lion,simba wa teranga!!Kote huku ni kutapatapa tu hata timu muuite MAJI TULIVU!!kama wachezaji wapo itakuwa ina shinda tu.Kifupi wachezaji wa tz hawajitambui,na hawataki kukiri hilo,hata Mbwana samata yupo pale kuna mtu anayejitambua ndio amemfikisha pale.
 
Kwa wachezaji hawa nadhan azam fc watachukua vikombe vingi.

Azaaaaaam fc hoyeeeeeeeeee
 
nishasema mara nyingi sana humu,Bongo hakuna profesionalism kwenye mpira,muacheni kapombe akacheze azam,ameamua kuwa mchezaji wa ridhaa daima.
 
http://2.bp.blogspot.com/-jreaL3HN9X4/U4dom--E6fI/AAAAAAAA-sw/mE5nub2ds_I/s1600/bocco+na+kapombe.jpg
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
HATIMAYE klabu ya Azam FC imefanikiwa kumsajili, beki anayeweza kucheza nafasi za kiungo pia, Shomary Salum Kapombe baada ya jana kumsainisha Mkataba wa miaka mitatu.
Katibu wa Azam FC, Nassor Idrissa Mohammed ‘Father’ ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, wamefuata taratibu zote kabla ya kumsainisha mchezaji huyo, na kufanikiwa kumalizana na klabu yake, AS Cannes ya Ufaransa.
“Kama inavyofahamika, mchezaji huyu alihamishwa kutoka Simba SC kwenda AS Cannes mwaka jana, kwa hivyo nasi tumemsajili kutoka timu hiyo, lakini asilimia fulani ya fedha, ambazo tutawalipa Simba SC,”amesema Nassor.
Maisha mapya; Shomary Kapombe kulia sasa ni mchezaji wa Azam FC

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema; “Hatuna tatizo na Kapombe, awaambie Azam FC walete asilimia 40 yetu katika fedha walizotoa kumnunua huko Cannes, na sisi tutanunua wachezaji wengine wazuri tu hata wawili kwa hiyo fedha,”.
Tayari Kapombe alikuwa amekwishajiunga na Azam FC tangu Machi mwaka huu baada ya kugoma kurejea Ufaransa tangu Novemba mwaka jana aliporejea kuichezea timu ya taifa, Taifa Stars mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe.
Kapombe aliyezaliwa Januari 28, mwaka 1992 aliibukia katika timu ya vijana ya Polisi Morogoro kabla ya kusajiliwa na Simba mwaka 2011, ambako alicheza hadi Agosti mwaka jana alipojiunga na Cannes.
Tupeni Chetu; Hans Poppe anataka Simba SC ipewe mgawo wake isajili wakali wengine

Simba SC ilimtoa mchezaji huyo bure AS Cannes kwa makubaliano akiuzwa klabu nyingine, itapata mgawo mzuri.
Hata hivyo, baada ya kugoma kuendelea kuchezea klabu hiyo ya Daraja la Nne, Simba SC ilitakiwa kulipa Euro 33, 000 ambazo sawa na Sh. Milioni 66 ili kurejeshewa mchezaji wake huyo.
Kapombe anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na mabingwa hao wapya wa Ligi Kuu, baada ya beki Abdallah Kheri kutoka Zimamoto ya Zanzibar kiungo Frank Domayo na washambuliaji Mrundi Didier Kavumbangu kutoka Yanga na Ismaila Diarra kutoka Mali.

Kwa kiwango cha juzi taifa nilitegemea haya.
 
Tumsubiri yule wakala sijui anaitwa nani tena dfk agent aje atupe maelezo. Ila itachukuwa miaka mingi sana kwa mchezaji aliyezaliwa bongo kwa miaka ya karibuni kucheza ligi kubwa ulaya labda wale waliozaliwa hukohuko majuu kama yule wa chelsea.tatizo la wachezaji wabongo wanataka acheze hapa nyumbani halafu ghafla bin vuu huyo barca au madrid wanakuja kumsajili. Poleni sana wachezaji wa bongo. Huyu kapombe kapoteza sana bahati miaka mtano ijayo atakuwa leaders anacheza bonanza badala ya kuweka historia kama wanyama wa kenya. Wangekuwa walau wanasoma habari za wachezaji wa west africa wanavyohangaika walau wa kwetu wangefika south africa ambapo bado ni pazuri tu.
 
Nilishasema hapa wakala hakuwa na tatizo. Tatizo ni Kapombe na wapambe wake.

Naungana tena kwa machozi mengi kuwa wachezaji wetu itachukua muda mrefu kufika wanakotaka kufika maana kila mwanga ukijitokeza, giza kubwa linafuatia badala ya kuwa vice versa.

Kilichomtoa Haruna Moshi Ulaya ni nini hadi kwenda kuishia Coastal Union? Kinachomtoa Kapombe Ufaransa ni nini hadi kwenda Chamazi? So sad, lkn atulize akili yake sasa apige kazi kuisaidia Azam anaweza kutoka tena
 
Nchi hii imeoza kila sehemu,,,, kwenye siasa taaban, michezo ndo usiseme, sijui bongo movie ni kucop na kupest, muziki wa dansi ndo umekufa,,, bongo flava kinachoimbwa hakieleweki ...
 
Nchi hii imeoza kila sehemu,,,, kwenye siasa taaban, michezo ndo usiseme, sijui bongo movie ni kucop na kupest, muziki wa dansi ndo umekufa,,, bongo flava kinachoimbwa hakieleweki ...

Tanzania majangaaa ona mjangaaa
 
Uvumilivu ni kazi sana kwa watanzania tulio wengi,Kapombe tayari amesha fell.Nakumbuka kuna mtu alishawahi kuniambia kupata kazi kwa wazungu inawezekana sana;job description ni chache kwa kutazma ila uhalisia kama ni mvivu na si wa kujifunza na uvumilivu,mwezi mmja ni mrefu sana daruga unazitundika.System imetuharibu sana na inatakiwa kuibadili haraka vinginevyo hata nchini kwetu tutashindwa kupata kazi zaa maana.period
 
R.I.P. Shomari Kapombe huko chamanzi, ujaacha pengo lolote Msimbazi.
Ahsante kwa huduma uliyotupatia.
 
Back
Top Bottom