Kanye West ashtakiwa kwa utapeli

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Kanye-West-233x300.jpg

SHABIKI mmoja nchini Marekani, Justin Rhett, ameamua kumshtaki nyota wa muziki wa Rap, Kanye West pamoja na huduma ya muziki ya Tidal kuhusu kutolewa kwa albamu mpya ya mwanamuziki huyo, The life of Pablo.

Rhett anadai alidanganywa kutia saini na kujiunga na huduma hiyo ya moja kwa moja kwa kuwa ilikuwa njia ya pekee ya kununua albamu hiyo ya West baada ya kutia saini.

Alisema kuwa alijiunga na Tidal baada ya mwanamuziki huyo kusema albamu yake haitauzwa kwingine. Jambo hilo linaonekana kuwa la kitapeli ambapo mamilioni ya wateja wameanza kuwa na wasiwasi na huduma hiyo ya Tidal.

Inadaiwa kwamba mpango huo ungekaa sawa kwa Kanye West, angefanikiwa kupata zaidi ya dola milioni 84 kutokana na mauzo hayo.

Source: Mtanzania
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom