Tumaini Makene
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 2,642
- 6,072
Kuna taarifa zisizokuwa na chembe ya ukweli ambazo zimezushwa na kusambazwa mitandaoni, ikiwa na pamoja na jukwaa hili zikijaribu kumhusisha Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe kuwa amechukua zabuni zote katika Wilaya ya Hai.
Wanaosambaza uongo huo, wamesema kuwa Mwenyekiti Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, amefanya hivyo kwa ubabe.
Ni vyema tukaweka ukweli kuhusu uzushi huo ambao umeanza kuwasumbua wanachama, wapenzi, mashabiki na wapenda mabadiliko kwa ujumla, kuwa Mwenyekiti Mbowe hana zabuni yoyote katika Wilaya ya Hai wala hajawahi na hana zabuni katika wilaya yoyote nyingine katika maisha yake yote ya uongozi na utumishi anaowajibika kwa umma.
Halmashauri ya Wilaya ya Hai kama yalivyo maeneo mengine ya halmashauri, manispaa na majiji ambayo yako chini ya uongozi wa Chadema na UKAWA kwa ujumla inajiandaa kuwa mojawapo ya maeneo ya kupigiwa mfano kwa mabadiliko yatakayofanyika kutokana na kusimamia uwajibikaji utakaotanguliza uadilifu mbele wenye dira ya maendeleo kwa ajili ya wananchi.
Hai ni halmashauri ambayo tayari imeweka rekodi kadhaa, kwanza inaongozwa na CHADEMA kwa 'full majority' kwa maana ya madiwani wanaounda baraza ambalo liko chini ya Mwenyekiti wa Halmashauri mwanamke ikiwa ni mara ya kwanza.
Makene