Hiyo namba kumi na moja,mwaka fulani tulienda kikazi Mkoa X nyanda za juu kusini tulikuwa Mimi na mshkaji wangu wa ofisini,tukafikia lodge moja kama kawaida yetu. Baadae ya wiki mbili tukawa wennyeji pale lodge jamaa akajiopolea manzi fulani mtaa wa pili kutoka pale akawa anajipigia,kumbe siku za mwanzo kabisa jamaa alipita na cashier wa pub mule lodge.
Baadae jamaa ndio kupata huyo demu wa nje ambae alikuwa kisu kweli,sasa yule cashier akaanzisha bifu la chini chini na jamaa yangu,siku moja jumamosi tukaamka mapema tukaanza kupiga gambe pale Pub muda ya saa9 nikamwambia jamaa Mimi nachomoka hapa naenda club fulani kupata mdudu na kuendeleza gambe,jamaa kwa kuwa alikuwa na demu wake na washawaka akasema anaenda kumpuzika then ataamka aendelee nikasema pia. Nikachomoka zangu,mida ya saa4 usiku nikarudi ile kufika mlango mkubwa wa lodge naona watu wanakimbiana kutoka ndani,nikszama nikakuta jamaa anapambana na masela fulani pamoja na security guard wa ile lodge.
Wala sikuuliza shida nini,moja kwa moja nikadaka kiti cha mbao piga sana wale wajinga nikamchomoa jamaa,baada ya hapo tukaanza kuwatembezea kichapo cha mbwa mwizi,gonga sana pamoja na yule cashier,wakakimbia nje mule ndani lodge yote tukabaki wawili tuu. Wakatufungia geti kwa nje tukawasikia wanaita polisi jamaa akaniambia mwana twende fasta vyumbani tukakusanye vitu vyetu ndani ya dakika kumi tuwe tushasepa hapa,kama Polisi tutaenda wenyewe kesho. Kweli ndani ya dakika saba kusanya kila kitu tukaruka ukuta kwa nyuma hao tukaenda mbali kidogo kwenye lodge nyingine,hapa tulikubaliana kila mtu kwa kipindi Hili akae lodge yake ila za karibu kwa usalama wetu ili likitikea lakutokea tusife kama nyumbu.
Baadae namuuliza jamaa shida nini,akasema kuwa yule cashier alimpanga ex wa yule demu wa nje aje amfanyie fujo jamaa kama fumanizi hivi,ndio timbwili likaanza na jamaa yangu sio mnyonge mikono anaiweza.
Baadae yule demu akatuambia Polisi wala hawakuja,asubuhi akatuambia kuwa tuu alikuja Mkuu wa ile kampuni ya ulinzi pamoja na mmiliki wa lodge akachukua maelezo pale na yule demu akaongea yote ilivyokuwa,cashier akawa kikaangoni kutoka kwa Bosi wake, Bosi wake akapiga simu na kutuomba msamaha na kuomba turudi pale eti amepata hasara sisi kuondoka pale maana tulikuwa tukae miezi mitatu pale na tulikuwa tunamuungisha sana vinywaji tukagoma kurudi,cashier akapigwa chini. Baadae katika harakati za clubs tukakutana na yule ex wa demu tukiwa na yule demu,tukamfuata tukamwambia leo tunakuua, baadae atukumuona tena mule ndani,kesho yake nakutana nae sehemu anaomba msamaha oh yule cashier ndio alimpanga na kumpa bia na hela akitegemea eti sisi wageni eti tutasanda.