Hoja za Lula-Maridhiano ya Zanzibar yatokane na kanuni


MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2009
Messages
741
Likes
47
Points
45
MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2009
741 47 45
Huyu mwandishi kasomea uandishi au basi ni mwana maskani aliepewa kalamu na kuanza kudumaza akili za jamii?

Kwa waandishi kama hawa kazi tunayo kweli kweli...:confused:

Maridhiano ya Zanzibar yatokane na kanuni

Lula wa Ndali-Mwananzela
Januari 27, 2010


KWANZA sina budi kushukuru barua pepe nyingi ambazo nimezipata kutoka kwa Wazanzibari wengi. Karibu barua zote nilizopata madai makubwa matatu yanatolewa; niache Wazanzibari wazungumzie mambo yao "wenyewe" (kwamba mambo ya Wazanzibari hayawahusu Watanganyika); Natumiwa na watu wasiopenda Wazanzibari wapatane (wengine wamedai nafurahia Wazanzibari wanapovurugana, na kwamba historia ya Zanzibar haijulikani kwa mtu mwingine yoyote isipokuwa Mzanzibari (mmoja kadai Mzanzibari anazaliwa na historia ndani ya damu yake!).

Katika makala hii nilitaka niendelee na hoja za kisiasa zaidi na kujibu hoja alizotoa Seif Shariff Hamad kwenye hotuba yake ile kuhusu Maridhiano na Mustakabali wa Zanzibar.

Lakini kutokana na mwitikio nilioupata na jinsi gani watu wengi wameguswa na makala iliyopita na hasa zaidi mwelekeo wa kisiasa Visiwani imenilazimu niliangalie suala hili kwa namna tofauti kidogo. Lakini kwanza niwajibu kwa mkupuo wale walioniandikia wakitoa hoja hizo hapo juu.

Kwanza, kwa wale ambao wanaona kuwa nimeingilia mambo ya "Wazanzibari" na kuwa tuyaache mambo hayo mikononi mwao peke yao na kuwa hata kuyajadili hairuhusiwi hawa nina jibu moja kwao; Mambo ya Zanzibar hayawahusu Wazanzibar tu na watake wasitaka yamefungamana kabisa na mambo yanayohusu Bara, eneo zima la Afrika ya Mashariki na kiukweli yanahusu dunia yetu hii. Kutokana na ukweli huu basi hakuna mtu yeyote katika sayari hii anayeweza kumuamulia mwingine azungumzie nini au asizungumzie nini.

Tabia hii ya kumuamuru mtu mwingine afanye au asifanye inatokana na hisia ya ubwana! Kwamba unamdharau mtu mwingine kiasi kwamba hata mawazo haya hayapaswi kutolewa kisa na mkasa kwa sababu hukubaliani naye! Hakuna mtu yeyote (awe Mzanzibari, mtu wa Bara au anayetoka peponi) ambaye anaweza kuniamulia mimi niseme nini, namna gani na kwa nini. Hivyo, kwa karidi ya kwamba Zanzibar bado ipo na ina masuala yenye kugusa jamii yake na jamii pana, kila Mtanzania anayo haki ya kuzungumzia mambo hayo bila ya kuomba kibali wala kuomba samahani.

Kama kuna watu ambao hawataki mambo ya Zanzibar yazungumzwe na watu wengine basi wao na wale wanaowaunga mkono wajikusanye pamoja na kukibeba kisiwa kizima na kukipeleka Zebaki au Zuhura ili watu wa sayari hii tusizungumzie!

Pili, hakuna mwanadamu yeyote mwenye akili timamu na ambaye anajali haki za watu au misingi ya haki za binadamu atafurahia machafuko mahali popote duniani. Kinyume na watu wengine ambao wanachagua wapi wakemee uovu sisi wengine tunapinga uovu kama utokee Pemba, Mwembechai, Tarime au mahali pengine popote.

Wakati wengine wanafikiria kuwa haki za Mpemba au Muunguja ni kubwa zaidi kuliko za mtu wa Mafia au Ileje, sisi wengine tunasimamia kanuni kuwa kila Mtanzania ana haki sawa na wakati wowote haki ya Mtanzania inatishiwa ni jukumu letu kuzisimamia bila kuangalia huyo mtu anatoka wapi.

Kama Watanzania ni maslahi yetu kuhakikisha kuwa yale yaliyotokea Zanzibar huko nyuma hayarudiwi tena na kwamba hatimaye siasa za Zanzibar zinakuwa za tofauti ya kiitikadi na hoja za kisiasa, sera na mwelekeo kuliko za kisasi, chuki na kuumizana. Mtanzania ambaye anaona kuwa ya Zanzibar hayamhusu hatendi haki kwa taifa lake.

Tatu, Wazanzibari hawana uhodhi wa historia yao. Ni kinyume na hoja za kimantiki kudai kuwa kwa vile mtu si Mzanzibari basi hawezi kujua historia ya Zanzibar kwa sababu wenye kuijua ni wachache waliojaliwa kuwa Wazanzibari tu. Barua zote nilizopokea wiki iliyopita zina maudhui hayo hayo: Nitoe mifano michache hapa (msisitizo ni wa kwangu):

Nashukuru kwenye makala yako umeweza kuonyesha chuki za kitwana dhidi ya Zanzibar na kujaribu kuitwika kila uongo wa dhahiri au shahiri kuikinga hoja yako hiyo Hongera, lakini kwa Mzanzibari umechelewa. Historia ya Zanzibar imo ndani ya mioyo ya Wazanzibari na kamwe si kwenye vitabu- Mkombe S.

Mimi nadhani Mr. Lula, wewe hasa ndio mpotoshaji wa historia kwa sababu mbali ya kushindwa kusikiliza na kuifahamu vizuri hotuba ya Maalim Seif lakini umeishia kuja juu na ubishi uliojikita katika akili yako ambao umekufanya kushindwa kuelewa facts na kukimbilia kupinga kabla hujaelewa. - – Mussa M.

Nimesoma makala yako kaka ila nimestushwa na kusikitishwa sana na maoni yako hasa kuhusu utukufu wa Historia ya Zanzibar,tatizo liko wapi? – Mohammed M.

Unapowalaumu wana CCM wa Zanzibar kwa kukubali kushirikiana na Upinzani mimi nikiwa miongoni mwa wana CCM kutoka Zanzibar na pia nikiwa kiongozi wa UVCCM katika chuo kimoja kilichopo Bara sijafahamu mantiki ya weye kama msomi kuandika makala ya uchochezi kama ile – Mohammed A.

Sikukuelewa kwamba wewe ni mwana historia au ni mwana CCM mwenye chuki na husda dhidi ya Wazanzibari, ninyi ndio mnaotaka Wazanzibari siku zote wawe wanaishi kwa kutesana na kuuana kwa visingizio vya siasa zisizokuwa za kiungwana, ninyi ndio mnaojaribu kupandikiza chuki dhidi ya Wanzanzibari wenyewe kwa wenyewe huku mkifurahia nyinyi mkishi kwa amani na Tanganyika yenu. – Moxamed M.

Naendelea kukaribisha maoni motomoto kama hayo. Hata hivyo, kama nilivyosema hapo juu historia ya Zanzibar haiwahusu Wazanzibari tu na sisi wengine kuwa watazamaji walio nje (tunaangalia). Wale ambao wangependa sana wengine wasiguse, kusoma, kutafakari au kutoa maoni juu ya historia ya Zanzibar hawajitendei haki wao wenyewe na hawawatendei haki watu wengine. Kama leo hii tunawafundisha watoto wetu historia ya Ulaya, historia ya Afrika na ya Dunia kwa ujumla tuna woga gani wa kujifunza historia ya Zanzibar kwa sababu tu baadhi ya watu hawapendi?

Wazanzibari wasiogope mtu mwingine kuangalia historia yao. Na mimi kama Mtanzania historia ya Zanzibari ni historia ya Taifa langu na ya watu wangu (Nilipoangalia mara ya mwisho Wazanzibari ni Watanzania!). Nikikubali (kwa woga au vinginevyo) kuwa mambo ya Wazanzibari hayanihusu nitakuwa na haki gani ya kufuatilia mambo ya Wameru kule Arusha na yale ya Wakurya kule Tarime?

Nikikubali kutozungumzia mambo ya Zanzibar ninakuwa na haki gani ya kuzungumzia mambo ya Morogoro, Mbeya, Bagamoyo na Tanga? Zanzibar ni sehemu ya Tanzania na kwa hilo peke yake linanipa haki ya kuzungumzia historia yao kama vile wao walivyo na haki ya kutolea maoni historia ya Mafia au Kilwa kwani nayo imefungamana na historia ya Zanzibar!

Naomba nirudi kwenye maridhiano.

Hakuna maridhiano ya kweli yenye kuleta mustakabali bora kwa Zanzibar ambayo yanaweza kutokana na hali ilivyo sasa. Maridhiano ya kweli hayawezi kupatikana bila kutambua misingi na kanuni muhimu ambazo juu yake ndio maridhiano hayo huweza kujengwa. Lakini kubwa zaidi ni kuwa kinachohitajika Zanzibar si maridhiano (msingi wa neno hili ni kuridhisha) bali ni mapatano (ambayo msingi wake ni kupatana).

Kama Wazanzibari na Watanzania wengine wataona kuwa ni bora kuridhishana kuliko kupatana basi wajue wanachofanya ni kuahirisha tu matatizo yaliyokuwapo. Watu wawili waliotofautiana wanaweza kukubaliana kuridhishana bila kushughulikia tofauti zao na hivyo kupatana.

Kwa mfano, mtu ambaye amekuibia punda wako na wewe ukaenda ukachukua mkokoteni wake na ukazuka ugomvi, basi mtajikuta mnatakiwa kuchukua uamuzi. Aidha kila mmoja atang'ang'ania kilicho mikononi mwake na kukihalalisha kwa hoja mbalimbali au mtaamua kukaa chini na kuamua jinsi gani mtasuluhisha tofauti zenu.

Mwaweza kurudishiana mlivyochukuliana na kila mmoja akaenda njia yake (mmeridhishana hapo) au mwaweza kuamua kurudishiana mlivyochukuliana na kuulizana kwanini mlichukuliana vitu hivyo ili huko mbele yasije kutokea tena na katika kufanya hivyo mkaamua kujenga mahusiano mema hata kwa kuazimana na kubadilishana vitu vingine kama ujirani mwema (huku ni kupatana).

Wazanzibari wanataka kuridhishana; Serikali ya Muungano wanataka Zanzibar waridhishane; binafsi naamini tunapoteza nafasi kubwa ya kihistoria ya kuleta mapatano Zanzibar. Mapatano ambayo yataangalia historia ya Zanzibar na matukio yote ya kheri na shari na kutoka kwayo kuweza kuona ni jinsi gani Zanzibar mpya yaweza kujengwa na jinsi gani Muungano utadumishwa pasipo kuendeleza machungu, hisia ya kuonewa na kukandamizwa na jinsi gani majaribu tunayopitia leo kama taifa yaweza kabisa kuwa ni chachu ya mafanikio makubwa zaidi ya Taifa letu katika bara la Afrika.

Ndugu zangu Watanzania! Kwenye machungu haiwezekani kuwa na mapatano. Mnaweza kuwa na maridhiano lakini yanakuwa ni maridhiano ambayo yamefunika tu manung'uniko. Kwa Zanzibar kuna mambo muhimu na ya msingi ambayo bila hayo kuwa sehemu ya mazungumzo ya mapatano basi juhudi zote za maridhiano zinatupia kizazi kijacho matatizo.

Naam! Kama kweli Wazanzibari na Watanzania wanataka kuwe na siasa za umoja na upatano Visiwani humo basi ni lazima kwanza kabisa tuwe tayari kuzungumza ambayo ni mwiko; tuwe tayari kujadili yaliyopigwa marufuku; na tuwe tayari kuukabili ukweli hata kama kwa kufanya hivyo tutatokwa na machozi.

Marekani, Taifa kubwa lenye nguvu zaidi duniani limechimbwa toka kwenye kingo na historia na kuundwa kutoka katika machozi na historia chafu na mbaya, lakini vile vile historia ya fahari na kheri na leo linasimama duniani kama jaribio kubwa zaidi la wananchi kujenga taifa lao wao wenyewe kwa kanuni zao wenyewe na kukabili changamoto zao kwa pamoja.

Marekani ni muungano; hata hivyo tangu zamani wanasema ni Muungano usiyo mkamilifu. Kwa karibu karne mbili na nusu, Wamarekani wamekuwa wakijitahidi kuuboresha Muungano wao na kuulinda. Leo hii Rais wa Marekani ambaye ana asili ya Afrika Barack Obama, anasimama kwa mara ya kwanza kutoa hotuba yake ya "Hali ya Muungano" kwa Bunge zima la Marekani na kwa wananchi.

Kuna watu kwenye taifa hilo hilo la Wamarekani bado hawaamini kuwa watu Weusi wana haki kama watu Weupe; kuna watu ambao hawaamini kabisa kuwa Obama ni Rais halali (wanahoji kuzaliwa kwake); wapo ambao wanaona kabisa kuwa Rais Obama anaingilia sana maisha yao na hivyo hata kumtambua hawataki kumtambua kama vile wengine walivyofanya hivyo kwa Rais George W. Bush baada ya uchaguzi wake wa kwanza. Na leo hii bado mahakama za Marekani zinahangaika kila kukicha kuamua kati ya mambo yanayohusu serikali kuu na serikali za majimbo. Lakini Wamarekani hawataki kuvunja Muungano wao.

Wapo Watanzania wa Zanzibar na Watanzania wa Bara ambao wanaamini kabisa kuwa "ni bora tu tuvunje huu Muungano yaishe"; watu hawa ambao wamekosa maono ya kiuongozi wanapenda kukwepa matatizo kuliko kuyashughulikia; ni hawa ambao kwao ni bora kusalimu amri kuliko kupigana kwa sababu wanaogopa kuchukua msimamo.

Wapo wengine ambao kutokana na vidonda vya machungu na huzuni hawataki kabisa kuona Muungano huu unafanikiwa. Naam! Wapo ambao wanasimama leo kufuata mkumbo wa kisiasa wakiamini kabisa kuwa hatima yao iko mikononi mwa watu wawili tu yaani Maalim Seif na Rais Amani Karume.

Kwa hawa nina ujumbe mmoja kwao; Muungano wetu upo na utadumu; Muungano wetu utakabiliwa na changamoto zaidi kuliko hizi za kisiasa na kihistoria; Muungano wetu katika yote unapaswa kulindwa na kutetewa kwani japo kuuvunja kwaweza kuwanufaisha wachache lakini kuuimarisha kutanufaisha vizazi vingi vijavyo.

Kama Abraham Lincoln asingeamua kupigana na ndugu zake wa Kusini waliotaka kujitenga na Shirikisho la Marekani leo hii Marekani isingekuwa jinsi ilivyo. Kama wasingetokea Wamarekani kutoka maeneo ya Kaskazini ambao walienda kupigania haki ya watu Weusi na kushirikiana nao katika harakati miaka ya hamsini na sitini, yawezekana hali ya kihistoria ingeandikwa tofauti.

Walikuwapo watu wa Kusini ambao walidai bila ya shaka kuwa "Mambo ya Kusini waachiwe watu wa Kusini wenyewe" na wapo viongozi ambao waliwakilisha hisia na mawazo ya watu wa Kusini ambao kwa muda mrefu wameona kuwa wanaonewa na watu wa Kaskazini. Lakini katika yote Wamarekani wameweza kutambua kuwa wamefungwa pamoja katika historia na mafanikio ya Kaskazini ni mafanikio ya Kusini na matatizo ya kusini ni matatizo ya Kaskazini. Na kwa sababu hiyo kwa pamoja wanashughulikia matatizo yao na kwa kufanya hivyo wanaimarisha Muungano wao.

Ni kutokana na hilo basi naamini ili tuweze kuondoka katika kiza hiki cha wasiwasi wa Muungano na hofu ya nini kitatokea Zanzibar ni lazima tujenge kanuni za mapatano ambazo kimsingi zitaleta kuridhishana kwa kweli na mustakabali wa kudumu wa Zanzibar na Tanzania nzima. Ni lazima tutambue kanuni za msingi ambazo zinaweza kuongoza mazungumzo ya mapatano hayo.

Binafsi ninayo mapendekezo ya kanuni kadhaa na misingi kadhaa ya nini chapaswa kufanyika Zanzibar ili kuleta mapatano ya kweli. Nidokeze tu hapa kwamba sikubaliani kabisa na hoja za kupiga kura ya maoni kujua kama wananchi wa Zanzibar wanataka serikali ya umoja wa kitaifa.

Tukikubali kuwa kura ya maoni iwe na nguvu ya kuamua nini kifanyike kisiasa Zanzibar kiasi cha kubadilisha mfumo wa serikali ni kitu gani kitazuia wanasiasa wengine kupendekeza huko mbele kura ya maoni ipigwe kuamua kama Zanzibar inataka kuwa sehemu ya Muungano au itoke?

Nitaendelea na wazo hili na hoja zangu za Kanuni na misingi ya mapatano na maridhiano ya kweli Zanzibar katika makala ijayo, inshallah.
 
Wacha1

Wacha1

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2009
Messages
12,765
Likes
1,031
Points
280
Wacha1

Wacha1

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2009
12,765 1,031 280
Huyu mwandishi kasomea uandishi au basi ni mwana maskani aliepewa kalamu na kuanza kudumaza akili za jamii?

Kwa waandishi kama hawa kazi tunayo kweli kweli...:confused:
Naona kakudumaza akili kazi kweli kweli.
 
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2008
Messages
14,745
Likes
2,035
Points
280
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2008
14,745 2,035 280
Tujifunze kuheshimu demokrasia ambayo ina enzi kila mtu kutoa mawazo yake bila kuvunja sheria.
Mimi sina shaka kwamba litakalotokea Zanzibar litawaacha wale wanaotaka uongozi kwa njia zisizo sahihi za kuonyesha kama vile wanatawaliwa kwa ukoloni na Tanganyika wakae midomo wazi,huku historia ikiwashuhudia wazi ubaya wa kutafuta njia za mkato kwenye maswali magumu.
 
MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2009
Messages
741
Likes
47
Points
45
MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2009
741 47 45
Tukikubali kuwa kura ya maoni iwe na nguvu ya kuamua nini kifanyike kisiasa Zanzibar kiasi cha kubadilisha mfumo wa serikali ni kitu gani kitazuia wanasiasa wengine kupendekeza huko mbele kura ya maoni ipigwe kuamua kama Zanzibar inataka kuwa sehemu ya Muungano au itoke?
Unajua amenifurahisha sana hapo, maana amenifanya nitoe kicheko cha kweli kweli.CCM na agizo lao la Butiama, sisi wazanzibari tulivyopiga kelele kusiwe na kura ya maoni.Walituona hatuna akili, wazenji hao kila siku kelele.

Sasa naona kibao kinagewageukia wao, wazenji wanasema leteni masuala mazito yote kwa wananchi tuamue.Na mimi ni mmoja nilianzisha thread humu JF ikiwa na kichwa cha habari "Masuala mazito yote tuletewe wananchi".

Basi sisi Zanzibar tunaendelea kuenzi agizo la Butiama :D
 
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined
May 19, 2009
Messages
13,211
Likes
385
Points
180
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined May 19, 2009
13,211 385 180
Kweli hivi visiwa viondoke kwenye uso wa dunia vipelekwe kusikojulikana ili tusiviongelee! Vikiwa kwenye sayari ya Pluto bado tutajua viko wapi, tutaviongelea kama tunavyoongelea Sayari yenyewe ya Pluto! Alternatively, watafute namna ya kuziba vinywa vyetu, masikio yetu na macho yetu (sijui ni kwa namna gani) ili tuwe bubu-viziwi-vipofu! Otherwise, tutaona, tutasikia na tutaongea, kwa kuwa ni uhuru wetu wa Kikatiba!
 
Monsignor

Monsignor

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
523
Likes
2
Points
0
Monsignor

Monsignor

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
523 2 0
Huyu mwandishi kasomea uandishi au basi ni mwana maskani aliepewa kalamu na kuanza kudumaza akili za jamii?

Kwa waandishi kama hawa kazi tunayo kweli kweli...:confused:
Huu wa kwako ndio mchele!!!!!!!????:rolleyes:
 
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2006
Messages
11,505
Likes
238
Points
160
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined May 5, 2006
11,505 238 160
MrFroasty,
Mimi namzimia Lula wa Ndali. Na aliyosema kuhusu Zanzibar na Seif ni ukweli mtupu. Ingekuwa vizuri zaidi kama ungeweza kupinga hoja zake hapa kwa kujenga hoja zako.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,898
Likes
8,105
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,898 8,105 280
Hakuna maridhiano ya kweli yenye kuleta mustakabali bora kwa Zanzibar ambayo yanaweza kutokana na hali ilivyo sasa. Maridhiano ya kweli hayawezi kupatikana bila kutambua misingi na kanuni muhimu ambazo juu yake ndio maridhiano hayo huweza kujengwa. Lakini kubwa zaidi ni kuwa kinachohitajika Zanzibar si maridhiano (msingi wa neno hili ni kuridhisha) bali ni mapatano (ambayo msingi wake ni kupatana).
miye nimeipenda hii hiyo..!!
 
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Messages
3,158
Likes
11
Points
0
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2009
3,158 11 0
Kweli hivi visiwa viondoke kwenye uso wa dunia vipelekwe kusikojulikana ili tusiviongelee! Vikiwa kwenye sayari ya Pluto bado tutajua viko wapi, tutaviongelea kama tunavyoongelea Sayari yenyewe ya Pluto! Alternatively, watafute namna ya kuziba vinywa vyetu, masikio yetu na macho yetu (sijui ni kwa namna gani) ili tuwe bubu-viziwi-vipofu! Otherwise, tutaona, tutasikia na tutaongea, kwa kuwa ni uhuru wetu wa Kikatiba!
soon mtaongea kwa adabu kubwa..siyo kikoloni koloni
 
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined
May 19, 2009
Messages
13,211
Likes
385
Points
180
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined May 19, 2009
13,211 385 180
Huu wa kwako ndio mchele!!!!!!!????:rolleyes:
Huyu MrFroasty ameifanya bara ni "kitambaa chake cha kupengea kamasi" kila zinapokuwepo puani! Wazenj walipoamua kupitia BLW kuwa Karume asiongezewe muda na kuwa maazimio ya Butiama yazingatiwe, bado ameona kama maamuzi yale ni ya Wabara eti kwa kuwa wametoa vitisho! Kwa lugha nyingine ni kulidhalilisha BLW na kulifanya kuwa si lolote na halina maamuzi yoyote ya kwake! Watu wa namna hii ni wa hatari sana na wanastahili kuogopwa kama ukoma!
 
MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2009
Messages
741
Likes
47
Points
45
MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2009
741 47 45
Huyu MrFroasty ameifanya bara ni "kitambaa chake cha kupengea kamasi" kila zinapokuwepo puani! Wazenj walipoamua kupitia BLW kuwa Karume asiongezewe muda na kuwa maazimio ya Butiama yazingatiwe, bado ameona kama maamuzi yale ni ya Wabara eti kwa kuwa wametoa vitisho! Kwa lugha nyingine ni kulidhalilisha BLW na kulifanya kuwa si lolote na halina maamuzi yoyote ya kwake! Watu wa namna hii ni wa hatari sana na wanastahili kuogopwa kama ukoma!
Is this Nyereres ghost?Mie aliponimaliza huyu bwana ni pale anapokuwa bizzi na Zanzibar wakati wenzake wanazama maji huko Kilosa.

Haya ongeleeni kuhusu karafuu zetu hadi mushibe harufu yake...sisi tunaenda kwenye kura ya maoni, kama tulivyoagizwa na Msekwa && Makamba.

Ujumbe huo kwenye attachment...

 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,898
Likes
8,105
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,898 8,105 280
MrFroasty.. wewe Zanzibar unataka kuwa na nini? Maridhiano au mapatano?
 
MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2009
Messages
741
Likes
47
Points
45
MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2009
741 47 45
MrFroasty.. wewe Zanzibar unataka kuwa na nini? Maridhiano au mapatano?
Mimi tena.....whats the difference?...I think Maridhiano is just fine with me...but I don't really know the difference, it seems to be almost the same thing with different color on it.After all I am not a swahili expert :rolleyes:

Yet i don't really get the point of Lula standing btwn these efforts...he is just another looser, just like everyone who will oppose this work.

Its whether you join the attempt made by Karume && Seif or we will just see you as another enemy of Zanzibar's peace...thats the theory we are going to use to succeed on this one.

So its up to you...remember this issue has been passed in the house of Reps with 100%!

Just to show you how serious this issue is, any puppets standing on our path will just be blown away :D
 
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined
May 19, 2009
Messages
13,211
Likes
385
Points
180
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined May 19, 2009
13,211 385 180
Is this Nyereres ghost?Mie aliponimaliza huyu bwana ni pale anapokuwa bizzi na Zanzibar wakati wenzake wanazama maji huko Kilosa.

Haya ongeleeni kuhusu karafuu zetu hadi mushibe harufu yake...sisi tunaenda kwenye kura ya maoni, kama tulivyoagizwa na Msekwa && Makamba.
Wewe wakati unaleta hoja hapa JF ulitaka nani aijadili? Au ulitaka Seif Shariff Hamad, Juma Duni, Prof Issa Shivji, Prof Ibrahim Haruna Lipumba, etc, etc, ndio wajadili? Kama hutaki mijadala basi hakuna haja ya kuileta hapa, otherwise acha mawazo tofauti ya-prevail na ndiyo demokrasia! Hiyo kura ya maoni unayodai ni maagizo ya Makamba na Msekwa ni kufilisika kimawazo na kulifanya BLW kuwa si lolote! Anyway, ni notion yako ya "kutupa kila uchafu" Bara ambako uchafu haujai, hata kama huo uchafu haujafanywa na Wabara! Endelea kumwaga uchafu kwenye "dampo!"
 
MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2009
Messages
741
Likes
47
Points
45
MrFroasty

MrFroasty

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2009
741 47 45
Hiyo kura ya maoni unayodai ni maagizo ya Makamba na Msekwa ni kufilisika kimawazo na kulifanya BLW kuwa si lolote!
Hapo sio kama napeperusha propaganda, nazungumza ukweli wa mambo.Hata huyo ndugu Lula ameonya juu ya hiyo kura ya maoni.Ni wazi hili ni wazo na agizo kutoka Butiama.

Huwezi kuficha makucha na uchafu huo wa kuwa kura ya maoni ni wazo limeanzishwa na CCM Bara.Kabla ya kujadiliwa hiyo hoja Msekwa alifanya kikao maalum na Karume, na hapo walicho kifanya CUF ni kupita mule mule.

Sema naona kama Msekwa na Makamba pamoja na vizee vya CCM havina macho makali kama ya Lula na niliyonayo mimi.Hii kura ya maoni itakutokeeni puani...maana ndio munafungua milango ya kuwa kila kero ya muungano pamoja na muungano wenyewe utaamuliwa kwa kura ya maoni.

Sema sisi huwa hatuna pupa...huo ndio ustaarabu wetu visiwani.Ukiona watu hawapigi kelele usije dhani hawana uwezo wa kukucharanga makofi, huwa wanakuacha tuu hadi ukifika muda wako ndio utasikia tuu...TAA!

Sasa kuwa mkweli na usilete kasumba kama za Nyerere, hili wazo zima la kura ya moani linaitwa AGIZO LA BUTIAMA!
 
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
43,029
Likes
18,079
Points
280
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
43,029 18,079 280
Lula wa Ndali Mwananzela.

Shakespeare alisema a rose is a rose by any other name.

Wazanzibari hawataki watu wazungumze mambo yao, hawajui kwamba kwa mujibu wa muungano hata watu wa bara wakiongelea mambo yao wanagusa mambo ya Zanzibar inevitably?

Mimi leo (mtu wa bara) nikisema sitaki au nataka muungano, tayari si nishaongelea fate ya Zanzibar?

Mbona kuna watu wako naively isolationist hivi?
 
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined
May 19, 2009
Messages
13,211
Likes
385
Points
180
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined May 19, 2009
13,211 385 180
Hapo sio kama napeperusha propaganda, nazungumza ukweli wa mambo.Hata huyo ndugu Lula ameonya juu ya hiyo kura ya maoni.Ni wazi hili ni wazo na agizo kutoka Butiama.

Huwezi kuficha makucha na uchafu huo wa kuwa kura ya maoni ni wazo limeanzishwa na CCM Bara.Kabla ya kujadiliwa hiyo hoja Msekwa alifanya kikao maalum na Karume, na hapo walicho kifanya CUF ni kupita mule mule.
Sasa kuwa mkweli na usilete kasumba kama za Nyerere, hili wazo zima la kura ya moani linaitwa AGIZO LA BUTIAMA!
Ninachofahamu ni kwamba huko Butiama walikuwepo Wazanzibari vile vile (Karume, Nahodha, et al) na kama waliona hilo wazo la Wabara (kama waliolianzisha ni wabara anyway, maana hujatoa ushahidi kuhusu hili) wangelikataa! Hapa nako unawaweka Wazanzibari waliokuwepo Butiama kuwa si lolote kama ilivyokuwa kwenye BLW! Anyway, kama nilivyosema tangu mwanzo, ikitokea hitilafu mahali fulani, Wazanzibari wanawekwa pembeni, hata kama walikuwa ni wenyewe watupu kama ilivyokuwa kwenye BLW, "mzigo mzito anabebeshwa Mnyamwezi!" Sasa hivi mmekaa mkao wa lawama kuhusu kura za maoni, ikitokea Wazanzibari wakakataa Serikali ya Mseto (Umoja wa Kitaifa?) Your hypocricy (undumilakuwili, ukinyonga, etc) will come to light soon!
 
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined
May 19, 2009
Messages
13,211
Likes
385
Points
180
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined May 19, 2009
13,211 385 180
Lula wa Ndali Mwananzela.

Shakespeare alisema a rose is a rose by any other name.

Wazanzibari hawataki watu wazungumze mambo yao, hawajui kwamba kwa mujibu wa muungano hata watu wa bara wakiongelea mambo yao wanagusa mambo ya Zanzibar inevitably?

Mimi leo (mtu wa bara) nikisema sitaki au nataka muungano, tayari si nishaongelea fate ya Zanzibar?

Mbona kuna watu wako naively isolationist hivi?
Kuna watu wamekaririshwa vitu vya kuzungumza ndugu Kiranga na ukiwadodosa zaidi wanaanza kujiumauma na wanajikuta hawana hoja!
 
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined
May 19, 2009
Messages
13,211
Likes
385
Points
180
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined May 19, 2009
13,211 385 180
Kiranga, I hate your signature: "There is no god, and Kiranga is his prophet."
 

Forum statistics

Threads 1,250,530
Members 481,403
Posts 29,736,594