Mbise Alex
New Member
- Apr 1, 2017
- 1
- 3
Somo: KANUNI ZA MJASIRIAMALI:
Mwl. Mbise, AJ
E: mbisealex@gmail.com
M: 0762730157
Wasalaam;
Leo tuendelee na somo letu ambapo tunajifunza Kanuni za mjasirimali. Utakubaliana nami kuwa kila kitu kina kanuni zake na ili uweze kufanya jambo kwa ukamilifu na kuona mafanikio yake ni lazima ufuate kanuni za jambo husika. Watu wengi wamekuwa wakifanya mambo bila kufuata taratibu na kanuni hali ambayo imesababisha watu wengi kutofikia malengo yao. Ukisoma maandiko matakatifu ya Biblia kuna sehemu imeandikwa “afanyaye kazi kwa ulegevu hatafanikiwa”, hii inatufundisha kuwa kwa lolote tunalofanya inatupasa kuweka bidii lakini pia kufuata kanuni za mambo tunayoyafanya ili tufike pale tunapotaka.
Nitaeleza kwa kifupi sana juu ya kanuni za mjasiriamali ila naamini zitakufanya na kukuonyesha namna ambayo unatakiwa kufanya endapo umeamua kwa dhati kuwa mjasiriamali. Zifuatazo ni baadhi ya kanuni za mjasiriamali miongoni mwa nyingine nyingi:
*Dhamira*: Dhamira ni kanuni ya kwanza na muhimu katika jambo lolote na siyo kwa ujasiriamali pekee. Mtu yeyote naweza kujiita mjasiriamali lakini kiukweli mafanikio yanahitaji uelewa wa kutosha,kufanya kazi kwa kujitoa huku ukiwa umeweka mbele lengo au dhamira. Lengo au dhamira ni motisha tosha itakaoyo kupa msukumo mpaka kufikia mafanikio. Dhamira ya kweli inahijajika kabla hujaingia katika biashara au mradi fulani.
*Uthubutu*: Baada ya kutambua pasina shaka dhamira yako unahitaji uthubutu. Hapa nazungumzia uwezo na utayari wa kufanya uamuzi mgumu wa kuingia katika biashara au mradi fulani huku ukiwa umeondoa nidhamu ya woga. Watu wengi ni waoga wa kuchukua hatua au kuthubutu kuingia katika biashara. Wengi wanaogopa kupata hasara, kuanguka mtaji au kufilisika. Mjasiriamali bora ni
lazima awe na uwezo wa kuthubutu kufanya mambo makubwa lakini uthubutu huo uendane na utafiti wa kina. Usiwekeze sehemu ambayo hujafanya utafiti wa kutosha.
*Nidhamu*:Nidhamu ni muhimu sana katika ujasiriamali, matumizi ya pesa, muda, nidhamu kwa wateja na kila kitu kinachohusu shughuli zako zinazokuingizia kipato. Nidhamu ni chanzo cha mafanikio na hivyo vema kuwa na nidhamu ya hali ya juu.
*Uvumilivu*: Watu wengi hasa vijana wamekuwa wakishindwa kuendelea katika ujasiriamali kwa sababu ya kukosa uvumilivu kwa kutaka mafanikio ya haraka kitu ambacho kinawapelekea kukata tamaa na kuishia kutofikia malengo. Unapoamua kuwa mjasiriamali inakubidi ujifunze kuvulimilia ili kufikia malengo yako.
*Umakini*: Wale waliofanikiwa siyo tu walikuwa tayari kufanya kazi bali waliweka umakini mkubwa katika kazi walizokuwa wakifanya. Mjasiriamali anatakiwa kuwa mwangalifu kwa kila jambo, anatakiwa kujua soko linaendaje na pia ni lazima awe na uelewa wa kutambua mabadiliko yanayojitokeza katika soko, uzalishaji na uendeshaji kwa jumla.
*Uaminifu*: Uaminifu ni silaha kubwa itakayokulinda mjasiriamali na kuwafanya watu wengi wapende kufanya kazi na wewe. Jifunze kulipa madeni hata kama ni madogo unapodaiwa, wauzie wateja wako huduma au bidhaa kwa bei halali, lipia kodi na vibali vyote muhimu. Kamwe usiwauzie watu bidhaa zilizokwisha muda wake, zenye ubora hafifu au mbovu kwani kwa kufanya hivyo, wateja watakukimbia na huo ndiyo utakuwa mwisho wako.
*Bidii*: Kama nilivyosema awali ili ufanikiwe katika kazi yoyote, lazima uwe na moyo wa kujituma na uipende kazi unayoifanya. Usisubiri kusukumwa kwa sababu hakuna atakayefanya kazi hiyo. Jifunze kuwahi kuamka asubuhi ili uendane na kasi ya soko, jitume kufanya mambo yatakayoiboresha biashara yako bila kuchoka na fanya kazi kwa moyo wako wote.
Tutaendelea wakati mwingine…!