Kanuni mpya za fedha: Dr Mpango

R.I.P MWALIMU NYERERE
 
R.I.P MWALIMU NYERERE
 
Beberu aingize $1000 kwa MPESA? Acheni ushamba bhana.
 
Kwa hyo watumishi wanaolipwa mishahara kuanzia mil 5 pale mishahara yao inaipoingizwa kwenye a/cc zao.
Je kitengo cha kulipa mishahara kitatakiwa kutoa taarifa FIU
 
Hadi vidola 1000 navyo mnavimaindi, hivi hii.mentality ya kimasikimasikini nani aliwapandikizia hawa watu?

Huwezi kubanabana flow ya pesa hata hizi ndogo ndogo kisha ukadhani unasaidia flow ya mitaji na business kwa watu wa kipato kidogo na cha kati
JF bwana inakizazi ambacho kinaumaskini mkubwa wa kuchakata taarifa wanazopokea, jilizisheni kwanza taarifa husika na ukimbilie jukwaa kutoa maoni.
jambo jingine jifunzeni kidogo huko ulaya wanafanyaje kuhusu mambo hayo ya transaction? kwa dunia ya leo hupiti na hela zaidi ya dola elfu kumi air port mpaka uitolee taarifa, haya mambo hayajaanza kwetu bongo,yapo kitambo kwa wenzetu sema sie ndo tunaanza labda
 
Hii kubana bana hii itazidi kutupoteza hongera muheshimiwa Peter Serukamba ndiyo haya uliogusia... kuna video nimeiona Ayo tv umeongea mambo ya msingi sana.. Big Up
 
Uongo mfano ulaya na Marekani wao ni wakali mno kama unatoka na pesa kwenye nchi zao lakini kama unaingiza wala hawakuhoji wala kukusumbua.Ndio maana mapesa kibao huingizwa mabenki ya uswisi na offshore banks.Wao wanataka ziingie ndio maana hata ukisafiri nchi zao kuomba Visa unatakiwa kupeleka benki statement wajue utawaingizia pesa.Hicho ulichonacho kwenye benki statement hawahangaiki kuhoji.Beba dola zako au pound zozote nenda nazo ulaya au Marekani uone kule kama kuna atakayekuuliza.Lakini Beba hizo pesa uje nazo nchi zetu za Dunia ya tatu utakoma.Hii vita ni kitu cha vi nchi maskini ndio vinavalia njuga.Nigeria hiyo Sheria ya money laundering walikataa wakasema ni uonezi kwanza dola elfu kumi ni hela ndogo pili mbona kwao viongozi wa Nigeria wanaingiza mabilioni nchini kwao mbona hawafuatilii wala kupiga makelele.Kwenye hii vita tutaumizana bure.Mtu kama anaingiza pesa nchini kwako au benki yako usiwe mkali mno Kila kitu Ku suspect vibaya!!!! Deposit tu za benki unashtuka shituka.Kenya kiwango cha kushitukia deposit au transfer ni dola laki tano or equivalent.Sisi hapa tu milioni sijui 25 mtu ajieleze Looooo.Kampesa sijui ka tu shilingi milioni sijui mbili toa maelezo mtaua sekta ya fedha.Watu wanapoingiza fedha toka nje mara ingine fumba macho kama kufuatilia fuatilia kimya kimya kama una suspect kitu sio tu kupiga miyowe .Wenzetu wasiri viongozi wa Afrika wakiiba na kupeleka kwao kuweko mabenki yao au kununua majumba nk wameufyata kimya kama hawajaona sababu zinaenda kuchangamsha uchumi wao.Kuamasha uchumi sio lelemama kuna maeneo mengine unatakiwa kuwa msiri na unapotezea kimya kimya.Pesa za kuhangaika nazo sana ni za serikali hizo ndizo uchunge sana hizo zingine za nje ya serikali chukulia poa tu achana nazo unless una suspect kitu fulani kibaya . Private money sio za kuvalia njuga ohhh unadeposit milioni 300 umetoa wapi.Kwani kwako serikalini kumeibiwa? Labda kama ni mfanyakazi wa serikali hapo sawa kuhojiwa sababu kuna maadili ya viongozi wa serikali nk.Lakini kwa private sector na watu binafsi ambao hawako public sector serikali iwe makini huko isipende kuchungulia chungulia na kuweka vitu vya kuchokonoa chokonoa huko ooh yule mbona anaingiza nchini dola milioni Moja.Kausha.Anakuingizia pesa kwenye nchi yako kama kufuatilia iwe kimya kimya Bila yowe asije shindwa kukuletea siku ingine sababu pesa hizo aweza kuwa kacheza kamari au kapata za Biko nk huko atokako kaamua kuja kuzilia nyumbani.Viongozi wetu kuweni wasiri jamani.Hata hayo madeposit sijui na miamala sijui iwe kiasi gani mngenong'onezana vikao vya ndani na mabenki na makampuni ya simu na maafisavAirports zetu na mipakani kuwa waripoti tu kama Wana suspect kitu kibaya Basi.No suspicion wakaushe mtu aingize pesa nchini au ku deposit au ku transfer kimya kimya.Na mkimdaka mtu suspect msipige yowe kuwa tumekamata mtu anaingiza pound milioni Moja .Mumalizane kimya kimya
Hakuna haja ya kupiga tarumbeta kwenye public.Watu watasusa kuleta hela iwe kwa transfer za bank au cash.Maswala ya haya mambo ya money laundering yanataka usiri na umakini mkubwa.Ukienda papara unaua sekta ya fedha na biashara ndani ya nchi
 

Well said Yehodaya.
Hivi vinchi masikini kama cha kwetu tunabanabana watu kwa pesa mbuzi kama dola 10000.
Hakuna Taifa la Money laundering kama Marekani, Wao Dola huwa wanachapisha tu wakijisikia kwa sababu wanajua kuwa Dola yao ina demand kwa hiyo itahitajika tu na Pia yupo Saudia pale atauza wese kwa dola tu na kuipa value hata kama wataprint. Lakini sisi akina hohehahe tunajiingiza katika vita siyo ya kwetu tunaanza kumaindi hata vidola 1000 hadi 10000!. Dola 10000 ni hela ambayo Messi anaitengeneza kwa dakika halafu SISI huku akina DR MPANGO wanataka kutusumbuasumbua kujaza maripoti sijui kitu gani.
THESE PEOPLE ARE NOT SERIOUS!
 
Kitu usichokijua ni kwamba wakati unasema uongo kuhusu Ulaya na Marekani kwenye mitandao, kuna watu humu wanaishi huko. Usifikiri kuwa wote humu tuko huko Buguruni. Ulaya gani hiyo ukimtumia shangazi yako $1000 kwenye nchi hiyo hiyo inatolewa taarifa?
 
Kwa style hii wawekezaji wataishia kenya, uganda, zambia na malawi.
 
Kwa waliowahi kufika Ethiopia watakubaliana nami kuwa tunaelekea Ethiopia sasa. Kama walivyo Waethiopia, tutaanza kuikimbia nchi yetu katika hii miaka 10 ya hawa watu.
Mkuu, nishaanza kufikiria kuhamia kati ya Uganda, zambia, na malawi. Hapa bongo kutoboa ngumu sana
 
Kwahiyo wewe inakuuma nini kuona mtu kanunua magari ya kifahari? Au ni kwasababu huna uwezo? Akili za kimaskini sana hizi mkuu. Badala uwaze namna ya kutafuta pesa Unashangilia kuona tajiri anabanwa?

Tajiri mmoja anauwezo wa kuajiri watanzania wengi. Sasa ukimbana huyo tajiri unamuumiza nani? Hivi unafikiri tajiri wako akiminywa utaendelea kupokea hako kamshahara kako ka mawazo?

Uchumi wetu ndo unaenda jehanamu hivyo, hakuna mwekezaji (FDI) atawekeza Tanzania kwa sheria za namna hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…