Kanuni mpya za fedha: Dr Mpango


Bongo nyoso, bank njaa sana...
Mpaka saivi siwaelewagi wakuruhusu ufungue USD acc halafu wakukate tena 1% ukiwa unatoa pesa yako halali. Dawa ni kujificha kwenye miamala ya kielectronic tu.
 
Nimekuelewa sana mkuu.

Na imekuja muda muafaka maana 2020 uchaguzi sio mbali.
 
Wamekosa ubunifu. Akili yao imegota. Halafu wakati unafungua account hawakuelezi habari ya makato. Yanakuja baadae wakati account imekwisha funguliwa! Ni kama haturuhusiwi kutoa pesa kwenye account!
Bongo nyoso, bank njaa sana...
Mpaka saivi siwaelewagi wakuruhusu ufungue USD acc halafu wakukate tena 1% ukiwa unatoa pesa yako halali. Dawa ni kujificha kwenye miamala ya kielectronic tu.
 
The failure state inatapatapa!Hizo ndiyo njia za kufikia uchumi wa kati?
 

Mkuu, binafsi sioni ubaya serikali kupitia banks kuwa na macho ya ziada kuhusu money laundering. Hakuna mwananchi atakaye athirika, biashara na miamala itaendelea kama kawaida, kwa nini tuwe na hofu? Kwa nini tunaogopa sheria zinazolinda hela chafu dhidi ya uchumi wetu.

BTW, vilevile na support vyama vya siasa kutangaza misaada yote wanayopata kutoka nje ya nchi. Kwa nini ufiche kama haina nia mbaya? CCM ikipewa pesa kutoka China na vivyo hivyo kwa CDM au ACT? Mbona hata USA wameweka hii sheria , kwao inaonekana sawa kwa nini kwetu ionekane ukatili?
 
Wamekosa ubunifu. Akili yao imegota. Halafu wakati unafungua account hawakuelezi habari ya makato. Yanakuja baadae wakati account imekwisha funguliwa! Ni kama haturuhusiwi kutoa pesa kwenye account!

Exactly....
Kama vile hawataki tutoe pesa, ukiritimba ndani ya karne ya 21. Teknolojia inakua ni suala la muda tu bank za bongo zitatolewa kwenye ramani, ndio maana hata cashless economy tz inaongozwa na mobile money na sio walafi wa banks.
 
Mi nimekuelewa
 
Hadi vidola 1000 navyo mnavimaindi, hivi hii.mentality ya kimasikimasikini nani aliwapandikizia hawa watu?

Huwezi kubanabana flow ya pesa hata hizi ndogo ndogo kisha ukadhani unasaidia flow ya mitaji na business kwa watu wa kipato kidogo na cha kati

Wapi dola 10,000 inahusika? Wapi dola 1000 inahusika? Hii kitu ya dola 1000 sidhani kama imekaa sawa
 
Hadi vidola 1000 navyo mnavimaindi, hivi hii.mentality ya kimasikimasikini nani aliwapandikizia hawa watu?

Huwezi kubanabana flow ya pesa hata hizi ndogo ndogo kisha ukadhani unasaidia flow ya mitaji na business kwa watu wa kipato kidogo na cha kati
Yaani ukimtumia mwanao sh.2,500,000 utoe taarifa kabla ya kufanya hivyo. Mbona hutwo ni tuhela twa mboga tu!
 
Unaweza kuwabinya sana watu lakini huwa kuna threshold kufikiwa. Hiyo threshold siku ikifika, watalipuka tu. Threshold ya Sudan ilifikiwa mwaka huu. Na ya Tanzania ina siku yake....
Hizi ni preventive measures kwao, na ni shield yao ya kutokufika huko wanaamini, yani kila kunapowaka sehemu wao hukaza ili waendelee kuwepo hapo walipo kwa pesa zenu.
 
Ndio maana private sector has been crippled. Naona kama nia sio kuboresha, ila kufanya mambo yasiwezekane kabisa.
Dola 1000 ni karibu 2.5mil. Kutuma 2.5 mil nayo ni shida?
 
Hali ya mifuko ni mbaya hivyo mpaka ela yakununua harrier turipoti kwenye kitengo cha usalama wa kifedha....
tucheke tu...tukilia haisaidii
 
That is a fact...na nimelink pia kwa kuwa tunaelekea kwenye uchaguzi....20/20
Walianza na wenye nazo na kuwatoa kwenye reli kwa sababu zao, kina Rugemalila, sinfasinga, manji, kina Peter Zakaria hadi masheikh wa uamsho, viongozi wa dini, kakobe, na Juzi mliona Gwajima kaitwa tena.
Hata mambo hayafanyiki kwa kubahatisha. Ni political stratergy.
 

Hawa watu wanasikitisha sana, au labda wanajitoa akili.

Wakati Mpango anatafuta msamaha wa madeni, wenzake wanakataa misaada ambayo si mikopo. Misaada hii ipo backed na UN convention kusaidia nchi maskini.

Tanzania ni nchi miongoni mwa least developed country na ina fursa ya kupata misaada (si mikopo) ili mradi tu iwe na diplomasia nzuri na shared values na donors (mostly Western countries).

Lakini leo ukimsikiliza Waziri Kabudi na Rais Magufuli ni wazi hii misaada watapewa wengine. Waziri anatoa kauli za "mabeberu" huku Rais akisema bora China hawana masharti kuliko West. Kweli?

Waziri Mpango inabidi akimbilie kukopa kwa hao hao "mabeberu" kwenye commercial na investment banks. Kama Greece hakusamehewa madeni sisi watakuja kuchukua mbuga za wanyama. Hakuna shareholder/investor atakubali pesa ipotee kwa watu maskini na viburi.
 
Kujitoa akili ndio tafsiri sahihi yanapokuja maswala ya uchumi, si ajabu wazungu washawazoea hayo maneno yao ni siasa tu za majukwaani wakimaliza wanarudi nyuma kuomba mikopo/misaada.

Dr Mpango mwenyewe kuna vitu huwa anaongea lakini udhani kama anaviamini mfano re-base waliofanya inaonyesha sector ya habari ndio inakuwa kwa kasi labda kama wanazungumzia channel za you tube wanazosajili huko TCRA lakini hili halina ukweli wowote in relation to economic growth.

Wakipeleka habari kama hizo IMF wanarudishwa kwenye dunia ya ukweli ukuaji wako ni 4% tu hizo indicators zako zingine azieleweki na uwezo wako wakukopesheka ni kupitia taasisi zetu huna uchumi wa kuuza bond kwenye international market.

Hizo benki zinazaoikopesha serikari ni kupitia WB na IMF ndio wanao facilitate kilatu na upande wa mabenki wanachofanya wao ni kupeleka proposals tu kwenye hizo taasisi madeni yao yalipwe kupitia kwa utaratibu fulani nchi inapokwama lakini private institutions hazina historia nzuri ya kusamehe madeni; hawa ndio watu waliokuja na Brady Bonds kuakikisha hela yao aipotei kirahisi rahisi nchi ata ikiwa inapitia wakati mgumu wa kiuchumi.
 
Blablabla ndio hizi

Money Laundering ni kuharibu ushahidi wa pesa iliopatikana katika njia zisizo halali sasa mnataka kutuambia watanzania wengi wetu tuna pesa haramu au?

Kama sio wivu wa waliokosa na chuki kwa wenye nacho na usumbufu?
Tushapitisha Sasa wewe fanya Kwa jinsi ujuavyo
 
Umeongea point sana mkuu... Mpango hawez kuimarisha uchumi wa nchi hii maama hajui chanzo cha tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…