Kanuni mpya za fedha: Dr Mpango

Kusema ukweli hata $10,000 n ndogo kwa wafanyabiashara hata wa level ya kati.
Hiyo pesa ni dogo sana hamna mfanya biashara anae enda nje na mtaji wa $10,000 tu atumie air tiketi $1200 hotel $1000 alipie na usafiri wa mzigo pamoja na kodi.....hapo wanafanya hali kua ngumu Kenya wataendelea kutupiga bao bora nitumie badari ya Kenya na benki za Kenya kuliko za hapa mfanya biashara yoyote hapendi usumbufu tunafukunza wafanya biashara wakati na wakubwa
 
Wachumi sababu ya kufanya hivi mbali kuzuia utakatishaji wa pesa,kina faida kwa uchumi?
 

Kwenye kiwango kuna mahali umeweka 1000$ na kwingine 10,000$, kiwango ni nini?
 
TRUE. We have been there before. Now they are taking us back into the communist world. Communists are dictators. Wanaweza kumfunga mtu kwa majina haya lakini matendo yao yanaonyesha. Wameharibu uchumi. Itafika wakati watakosa hata pesa za kulipa mishahara ya wafanyakazi. Watalazimika kutaifisha nyumba na amana za watu benki ili kuendesha serikali kama alivyofanya Nyerere mwaka 1967. Why are they not learning from history? Kuna nchi gani ya kikomunisti iliyowahi kupata maendeleo ya watu ama vitu?
 
Jamaa wanaharibu uchumi kisha wanakuja kutupia lawama kwa wazungu kwa kuwaita eti mabeberu, yaani slogan zile zile za enzi za ujamaa wanazirudisha tena
 
Hadi vidola 1000 navyo mnavimaindi, hivi hii.mentality ya kimasikimasikini nani aliwapandikizia hawa watu?

Huwezi kubanabana flow ya pesa hata hizi ndogo ndogo kisha ukadhani unasaidia flow ya mitaji na business kwa watu wa kipato kidogo na cha kati
Unazijua kanuni za India na us wewe?
 
Hadi vidola 1000 navyo mnavimaindi, hivi hii.mentality ya kimasikimasikini nani aliwapandikizia hawa watu?

Huwezi kubanabana flow ya pesa hata hizi ndogo ndogo kisha ukadhani unasaidia flow ya mitaji na business kwa watu wa kipato kidogo na cha kati
Mbona hiyo n kawaida Sana nchi za wenzetu ?kwa watumiaji wazuri was benki wenye transaction kubwa hiyo kitu wanifaham ila Kama unatransaction ndogondogo utaona n kitu kipya

All in all money laundering Ina impact kubwa Sana kwenye uchumi was nchi.Hata hivyo tumechelewa Sana kuja na hi sheria
 
Hivi siku hizi madokta wanapatikanaje kwani?

Hahaha, Umenifanya nicheke kwa sauti
Kuna mtu alisema, "Mpango wa tume ya mipango na Mpango wa Wizara ya fedha na mipango ni watu wawili tofauti"
Lakini ki-ukweli, hizi ni zama tu, nazo zitapita
 


Blablabla ndio hizi

Money Laundering ni kuharibu ushahidi wa pesa iliopatikana katika njia zisizo halali sasa mnataka kutuambia watanzania wengi wetu tuna pesa haramu au?

Kama sio wivu wa waliokosa na chuki kwa wenye nacho na usumbufu?
 
Ukiwa mjinga utasapoti kila kitu - hata ujinga. Kanuni za India na US zinasemaje kuhusu miamala ya $1000? US na India unaizona kwenye ramani tu, siyo?
Unazijua kanuni za India na us wewe?
 
Ukiwa mjinga utasapoti kila kitu - hata ujinga. Kanuni za India na US zinasemaje kuhusu miamala ya $1000? US na India unaizona kwenye ramani tu, siyo?
India huwezi kutuma nje ya india dola 1,000 bila ya benki kuu kujulishwa
Tatizo lenu mnauza bucha,vingunguti to manzese muamala umekamilika
 
Hao ndio wasomi wetu bhana hiyo Wizara wamkabidhi Bashe wa Nzega au Halima Mdee watukomboe kwenyd hii deep shit.
 
Unaota wewe. Nani kakwambia India ukituma rupee kiasi kadhaa kwa shangazi yako ambaye yuko hapo hapo India inabidi utoe taarifa kama hii sheria yenu mpya ya kikomunisti inavyotaka? Hata kama una mapenzi na huu ushetani, mambo mengine ni vema kuyanyamazia tu. Nani kakwambia kwamba BOT huwa haijulishwi na mabenki ya biashara kuhusu pesa wanazotuma na kupokea kutoka nje?
India huwezi kutuma nje ya india dola 1,000 bila ya benki kuu kujulishwa
Tatizo lenu mnauza bucha,vingunguti to manzese muamala umekamilika
 
Kwa US$ 1000 kuitolea maelezo ni kusumbuana tuu...

Kwa US$ 10,000 kuzitolea maelezeo tena swala litafanyiwa kazi ndani ya siku tano, ni kuchelewesheana mishahara tuu...

Bank ifanye kazi zote za kupeleka hayo maelezo panapohusika mimi mambo yangu yaendee...

Hapo sasa itakua kama una issue zako juu ya US$10,000 unaanza kuzitoa kidogo kidogo kila siku mpaka tarehe ya jambo lako una US$10,000 mkononi...


Cc: mahondaw
 

Ukiitoa kidogo kidogo wanakata kodi, kwa hiyo utagundua kuwa sababu mojawapo ya kubanabana huenda ni ili walime kodi kwenye miala mingi utakayofanya!
Ndiyo maana hata kwenye ATM wameweka limit ya kutoa laki nne nne ili ukitoa milioni wakate gharama za kodi za miaamala minne!
 

Kwa Bank niliyopo mimi chini ya US$ 1,000 unatoa bila kukatwa chochote, juu ya hapo ndiyo wanakata asilimia moja ya kuanzia US$ 1,000 and above...


Cc: mahondaw
 
Safi sana Serikali kwa kuliona ilo, natumaini pia ni njia sahihi ya Watu wanao takatisha Pesa kukomeshwa.

Kuna wengine wananunua Magari ya Fahari wanayajaza Showroom yote hiyo kutakatisha Fedha.

Hii njia ni Bonge la Mwarobaini kwa Serikali yenye juhudi za kuweka Usawa. Pongezi Waziri Dr Mpango heshima kwako.
 
Sijaelewa maana ya hii kitu kwa kweli.
Tayari tunayo sheria na kanuni za antimoney laundering.

Kanuni hizi zinaelekeza kila bank inatakiwa kutoa taarifa ambazo kwa mihala ya aina yoyote ambayo sio ya kawaida inayofanywa na wateja wao "suspicious transactions". Mabank yamepewa nguvu za kutokufanya mihamala hiyo ikibidi. Serikali binafsi imeishatumia mamilion ya pesa kuwa train maafisa wa bank namna ya kutambua mihamala yenye mashaka, Mabank pia yamewekeza pesa nyingi sana kwenye kutrain wafanyakazi wao, yamewekeza kwa kuajiri na kuwalipa mishara mizuri sana wafanyakazi ambao ni mahusi kwa kuangalia mihala hiyo na yamewekeza pesa nyingi sana kwenye teknologia ya utambuzi wa mihala yenye mashaka.

Sasa inamaana hayo yote ni bure? au kanuni hizi zinafanya kazi kwa pamoja?
serikali inauwezo wa kuipitia mihamala yote hii au ndio inataka kuingilia private financial affairs zetu, financial surveillance ya namna hii inatia mashaka na ninaamini imetengenezwa katika misingi ya ujinga wa uongozi.

mtu yeyote anayefikiria anaweza kucontrol kila kitu ni mjinga tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…