Kanuni mpya za fedha: Dr Mpango

Kanuni mpya za fedha: Dr Mpango

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
16,818
Reaction score
62,032
KANUNI mpya za kudhibiti utakatishaji fedha, zinatarajiwa kubana zaidi wanaofanya miamala kwa njia za kielektroniki ikiwamo benki na simu za mkononi.

Kwa mujibu wa kanuni hizo zilizosainiwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, Mei 7, mwaka huu na kuchapishwa kwa umma Mei 24, zinataka taarifa za mtu anayefanya muamala wa fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 10,000 (zaidi ya Sh mil. 20) au zaidi, kutoa taarifa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU).

Kanuni hizo pia zinabana wanaochezesha michezo ya kubahatisha kwa njia mbalimbali ambao nao wanatakiwa kutoa taarifa zao FIU.

Kwa mujibu wa kanuni hizo, kiasi hicho kinachotakiwa kutolewa taarifa ni kile kilichofika thamani hiyo ya fedha kwa muamala uliofanyika kwa wakati mmoja.

Katika kanuni hizo, uhamishaji fedha umetafsiriwa kuwa unajumuisha “shughuli yoyote ya fedha inayohusisha amana, utoaji, kubadilisha, malipo au kupokea fedha kwa shilingi za Tanzania au sarafu yoyote ya kigeni.”

Kanuni ya tano inasema, “mtu anayepaswa kutoa taarifa, atapaswa kutoa taarifa zifuatazo katika Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) (a) ubadilishaji wa fedha zinazohusisha shilingi za Tanzania au sarafu yoyote ya kigeni ambayo thamani yake ni sawa na dola 10,000 za Marekani au zaidi kwa mara moja.

“(b) Kuhamisha fedha kwa mtandao, unaohusisha shilingi za Tanzania au sarafu yoyote ya kigeni sawa na Dola 1,000 za Marekani au zaidi kwa mkupuo.

“(4) Katika kutambua thamani ya fedha za kigeni sawa na Dola za Marekani 10,000 kwa madhumuni ya taarifa ya fedha au dola 1,000 kwa lengo la kutoa taarifa za uhamisho wa fedha za kwa njia ya kielektroniki, muhusika anatakiwa kutumia viwango vilivyowekwa na Benki Kuu ya Tanzania vinavyotumika kwa wakati huo.”

Akizungumzia kanuni hizo, Msemaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ben Mwaipaja, alisema; “kanuni zinasema mtu yeyote anayefanya muhamala wa fedha kwa njia ya mtandao ama anayesafirisha fedha kwa njia ya mtandao, atoe taarifa kwamba ‘nataka kusafirisha kiasi fulani kwa sababu fulani’.

“Kama unatuma fedha Japan kwa ajili ya kununua gari ama umepokea fedha kutoka nje, au unataka kumtumia mtu fedha zinazofika kiasi kilichotajwa kwenye kanuni, lazima utoe taarifa, hii ni kwa benki ama simu kwa sababu zote hizo ni njia za kielektroniki.

“Utaona dhumuni hapa ni kupambana na fedha haramu ama ndiyo maana ukienda kwenye mambo ya ‘cash’ kuna sheria inabana ipo kwenye viwanja vya ndege na mipaka, kwamba mtu anaweza kusafirisha kiasi gani cha fedha na azitolee taarifa.

“Kwa hiyo inahusu watu wote kama ni nje ama ndani ndiyo maana inasema ndani au nje ya nchi,” alisema.

Alisema kanuni hizo zinabana hata wale wanaochezesha michezo ya kubahatisha ambao kama wanataka kutoa fedha kama zawadi ambazo zinafika kiwango kilichotajwa na kanuni wanatakiwa kutoa taarifa hizo.

“Kwa hiyo hizi kanuni zinakubana kama unataka kutumia njia za kielektroniki kutuma fedha ama kuchukua fedha huko,” alisema.

Kanuni ya 11 inasema miamala miwili au zaidi ikifanywa ndani ya saa 24 na kufikia dola 10,000 za Marekani au zaidi, itachukuliwa kuwa ni muamala mmoja na hivyo itatakiwa kutolewa taarifa.

Kwa mujibu wa kanuni hizo, ripoti za uhamisho wa fedha kielektroniki au ripoti zote za fedha zitapelekwa FIU kabla ya kumalizika kwa siku tano za kazi baada ya siku ya uhamishaji.

“Zitapelekwa kwa njia ya kielektroniki au vinginevyo inavyohitajika na FIU, kila operesheni ya shughuli za michezo ya kubahatisha atahitajika kutoa ripoti ya fedha kwa fedha zilizopatikana kutoka kwa mteja,” inasema sehemu ya kanuni hizo.

Kanuni hizo pia zimeweka adhabu mbalimbali kwa watakaoshindwa kufuata matakwa yake ikiwa ni pamoja na faini na kifungo.

Zinasema FIU au mdhibiti akiridhika kwamba mtoa ripoti ameshindwa kutoa ripoti ya fedha au uhamisho wa fedha zilizohamishwa kielektroniki au kimataifa, kitengo hicho kinaweza kutoa onyo au tahadhari ya kurudia mwenendo uliosababisha kutotii.

Mtu atakayefanya kosa hilo pia anaweza kusimamishwa kufanya shughuli yake ama biashara, kutozwa faini isiyozidi Sh milioni tano na isiyopungua Sh milioni moja kwa siku ambayo kasoro ilijitokeza.

Adhabu nyingine ni kusimamisha leseni ya biashara au kusimamishwa au kuondolewa kutoka ofisi ya mfanyakazi ambaye alisababisha kasoro hiyo.
 
Hadi vidola 1000 navyo mnavimaindi, hivi hii.mentality ya kimasikimasikini nani aliwapandikizia hawa watu?

Huwezi kubanabana flow ya pesa hata hizi ndogo ndogo kisha ukadhani unasaidia flow ya mitaji na business kwa watu wa kipato kidogo na cha kati

Umeiona vizuri au mi nimeona elfu kumi WWE umeo elfu moja kweli?
 
Daaaaah
Aisee, huu ni umasikini uliokithiri. Tatizo watu waliokulia kwenye mazingira hatarishi hawawezi kuwaza nje ya makuzi yao.
Hivi unaanzaje kuwaza kuripot muamala wa dola 1000. Jamani hii si 2.3m? Yaani nusu ya mshahara wa DED
Kweli ukistaajabu ya firauni unaweza kufir
 
Mpango: "mtu anayefanya muamala wa fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 10,000 au zaidi, kutoa taarifa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU)"

Me on Monday: 'Muamala wa $ 7800"

Me on Tuesday: 'Muamala wa $ 9500"

hapo nani mjanja?
😉😉😉😉
 
Uchumi chini ya nahodha Dr Mpango auwezi imarika kamwe the guy just doesnt have any tricks under his sleeves.

Kila siku anatafuta namna ya kuongeza ugumu kwenye mzunguko jamaa ni shida.

Ukisikiliza clip ya Bashe unaona sehemu ambayo anaelezea tatizo lililojitokeza kwenye kubadili hela wamefuta, ni watu wanaopenda kujifariji ata wanapokosea, wamejaza wanasiasa wenye shida ndani ya chama kwa sababu ya kuwasifia ata waapofanya mambo ya ovyo halafu wanachukua muda kufanya corrective actions mpaka athari zinapokuwa kubwa.

Hili sasa lingine ambalo madhara yake linaenda ongeza shida kwenye mzunguko, seriously huyu jamaa amekuwa akishauri maraisi hadi kufikia kupewa uwaziri wa kuteuliwa mbona mtu mwenyewe sio mmbunifu kabisa.

Halafu sasa katika speech yake baada ya majigambo yote deni la taifa linahimilika mwisho wa siku anasema wazi kabisa serikari inafikiria kuomba kusamehewa madeni yake kupitia wale wasio Paris Club, the opposite of that is the London Club (in other words mabenki makubwa ya kimataifa wanaoidai nchi).

Someone needs to tell him madeni yaliyofutwa miaka ya 80 ni kwa sababu kulikuwa hakuna namna nchi maskini kwa ujumla wake zilikuwa zina accumulated debt ya zaidi ya $500-800b na kuendelea kuwalazimisha walipe ilikuwa ni kuwaumiza wananchi wakose huduma ndio sababu ya kufuta hila sharti la kuendelea kuwasaidia ilikuwa wabadili tabia za kisera.

Watu kama akina Nyerere ambao walikuwa awataki ushauri wa kubadili tabia pamoja na kuwa wanashida ndio sababu za kunyimwa mikopo wale jeuri yao mwishowe tunajua yeye mwenyewe alikubali yaishe kwa kun'gatuka.

Since then wakopaji washajifunza awatoi kama uwezi kulipa, kama ulipewa kwa tathmini na wana kufanyia assessment periodically utalipa tu; tena afadhali ata hao Paris Club maana ni mataifa pamoja na kuwa wana masharti magumu zaidi ya mikopo lakini ni mataifa ambayo yanaweza samehe hao wengine huruma yao ni kukufanyia restructuring lakini kusamehe nadra sana ni hela za wateja wa bank hizo au shareholders.
 
Hadi vidola 1000 navyo mnavimaindi, hivi hii.mentality ya kimasikimasikini nani aliwapandikizia hawa watu?

Huwezi kubanabana flow ya pesa hata hizi ndogo ndogo kisha ukadhani unasaidia flow ya mitaji na business kwa watu wa kipato kidogo na cha kati
Uchumi wa kitaahira!
 
KANUNI mpya za kudhibiti utakatishaji fedha, zinatarajiwa kubana zaidi wanaofanya miamala kwa njia za kielektroniki ikiwamo benki na simu za mkononi.

Kwa mujibu wa kanuni hizo zilizosainiwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, Mei 7, mwaka huu na kuchapishwa kwa umma Mei 24, zinataka taarifa za mtu anayefanya muamala wa fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 10,000 (zaidi ya Sh mil. 20) au zaidi, kutoa taarifa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU).

Kanuni hizo pia zinabana wanaochezesha michezo ya kubahatisha kwa njia mbalimbali ambao nao wanatakiwa kutoa taarifa zao FIU.

Kwa mujibu wa kanuni hizo, kiasi hicho kinachotakiwa kutolewa taarifa ni kile kilichofika thamani hiyo ya fedha kwa muamala uliofanyika kwa wakati mmoja.

Katika kanuni hizo, uhamishaji fedha umetafsiriwa kuwa unajumuisha “shughuli yoyote ya fedha inayohusisha amana, utoaji, kubadilisha, malipo au kupokea fedha kwa shilingi za Tanzania au sarafu yoyote ya kigeni.”

Kanuni ya tano inasema, “mtu anayepaswa kutoa taarifa, atapaswa kutoa taarifa zifuatazo katika Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) (a) ubadilishaji wa fedha zinazohusisha shilingi za Tanzania au sarafu yoyote ya kigeni ambayo thamani yake ni sawa na dola 10,000 za Marekani au zaidi kwa mara moja.

“(b) Kuhamisha fedha kwa mtandao, unaohusisha shilingi za Tanzania au sarafu yoyote ya kigeni sawa na Dola 1,000 za Marekani au zaidi kwa mkupuo.

“(4) Katika kutambua thamani ya fedha za kigeni sawa na Dola za Marekani 10,000 kwa madhumuni ya taarifa ya fedha au dola 1,000 kwa lengo la kutoa taarifa za uhamisho wa fedha za kwa njia ya kielektroniki, muhusika anatakiwa kutumia viwango vilivyowekwa na Benki Kuu ya Tanzania vinavyotumika kwa wakati huo.”

Akizungumzia kanuni hizo, Msemaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ben Mwaipaja, alisema; “kanuni zinasema mtu yeyote anayefanya muhamala wa fedha kwa njia ya mtandao ama anayesafirisha fedha kwa njia ya mtandao, atoe taarifa kwamba ‘nataka kusafirisha kiasi fulani kwa sababu fulani’.

“Kama unatuma fedha Japan kwa ajili ya kununua gari ama umepokea fedha kutoka nje, au unataka kumtumia mtu fedha zinazofika kiasi kilichotajwa kwenye kanuni, lazima utoe taarifa, hii ni kwa benki ama simu kwa sababu zote hizo ni njia za kielektroniki.

“Utaona dhumuni hapa ni kupambana na fedha haramu ama ndiyo maana ukienda kwenye mambo ya ‘cash’ kuna sheria inabana ipo kwenye viwanja vya ndege na mipaka, kwamba mtu anaweza kusafirisha kiasi gani cha fedha na azitolee taarifa.

“Kwa hiyo inahusu watu wote kama ni nje ama ndani ndiyo maana inasema ndani au nje ya nchi,” alisema.

Alisema kanuni hizo zinabana hata wale wanaochezesha michezo ya kubahatisha ambao kama wanataka kutoa fedha kama zawadi ambazo zinafika kiwango kilichotajwa na kanuni wanatakiwa kutoa taarifa hizo.

“Kwa hiyo hizi kanuni zinakubana kama unataka kutumia njia za kielektroniki kutuma fedha ama kuchukua fedha huko,” alisema.

Kanuni ya 11 inasema miamala miwili au zaidi ikifanywa ndani ya saa 24 na kufikia dola 10,000 za Marekani au zaidi, itachukuliwa kuwa ni muamala mmoja na hivyo itatakiwa kutolewa taarifa.

Kwa mujibu wa kanuni hizo, ripoti za uhamisho wa fedha kielektroniki au ripoti zote za fedha zitapelekwa FIU kabla ya kumalizika kwa siku tano za kazi baada ya siku ya uhamishaji.

“Zitapelekwa kwa njia ya kielektroniki au vinginevyo inavyohitajika na FIU, kila operesheni ya shughuli za michezo ya kubahatisha atahitajika kutoa ripoti ya fedha kwa fedha zilizopatikana kutoka kwa mteja,” inasema sehemu ya kanuni hizo.

Kanuni hizo pia zimeweka adhabu mbalimbali kwa watakaoshindwa kufuata matakwa yake ikiwa ni pamoja na faini na kifungo.

Zinasema FIU au mdhibiti akiridhika kwamba mtoa ripoti ameshindwa kutoa ripoti ya fedha au uhamisho wa fedha zilizohamishwa kielektroniki au kimataifa, kitengo hicho kinaweza kutoa onyo au tahadhari ya kurudia mwenendo uliosababisha kutotii.

Mtu atakayefanya kosa hilo pia anaweza kusimamishwa kufanya shughuli yake ama biashara, kutozwa faini isiyozidi Sh milioni tano na isiyopungua Sh milioni moja kwa siku ambayo kasoro ilijitokeza.

Adhabu nyingine ni kusimamisha leseni ya biashara au kusimamishwa au kuondolewa kutoka ofisi ya mfanyakazi ambaye alisababisha kasoro hiyo.
wanatafuta kodi na tozo humo.
 
Jiwe angempa kazi Mh Bashe kwenye maswala ya uchumi
Hii nchi haina mshauri wa uchumi
Wapo lakini ni waoga kumshauri
Mwl Nyerere alisema ukiwa mwoga kumshauri mtu,ujue mnafik‍♂️
 
Duh. This is terrible. Hii italeta shida sana. Wateja watazidi kuchelewesha malipo. Sababu ya kwanza itakuwa ni kutoa ripoti FIU. Kitakachofata ni miamala midogo midogo kila baada ya masaa 24 ili kuepusha ripoti ya FIU. Ila pia hii itaongeza mapato yanayotokana na ‘transaction fees’ kwa benki na makampuni ya simu.
 
They do not think things thoroughly wao ni kukurupuka tu
 
KANUNI mpya za kudhibiti utakatishaji fedha, zinatarajiwa kubana zaidi wanaofanya miamala kwa njia za kielektroniki ikiwamo benki na simu za mkononi.

Kwa mujibu wa kanuni hizo zilizosainiwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, Mei 7, mwaka huu na kuchapishwa kwa umma Mei 24, zinataka taarifa za mtu anayefanya muamala wa fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 10,000 (zaidi ya Sh mil. 20) au zaidi, kutoa taarifa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU).

Kanuni hizo pia zinabana wanaochezesha michezo ya kubahatisha kwa njia mbalimbali ambao nao wanatakiwa kutoa taarifa zao FIU.

Kwa mujibu wa kanuni hizo, kiasi hicho kinachotakiwa kutolewa taarifa ni kile kilichofika thamani hiyo ya fedha kwa muamala uliofanyika kwa wakati mmoja.

Katika kanuni hizo, uhamishaji fedha umetafsiriwa kuwa unajumuisha “shughuli yoyote ya fedha inayohusisha amana, utoaji, kubadilisha, malipo au kupokea fedha kwa shilingi za Tanzania au sarafu yoyote ya kigeni.”

Kanuni ya tano inasema, “mtu anayepaswa kutoa taarifa, atapaswa kutoa taarifa zifuatazo katika Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) (a) ubadilishaji wa fedha zinazohusisha shilingi za Tanzania au sarafu yoyote ya kigeni ambayo thamani yake ni sawa na dola 10,000 za Marekani au zaidi kwa mara moja.

“(b) Kuhamisha fedha kwa mtandao, unaohusisha shilingi za Tanzania au sarafu yoyote ya kigeni sawa na Dola 1,000 za Marekani au zaidi kwa mkupuo.
Hivi siku hizi madokta wanapatikanaje kwani?
 
Hawakurupuki, wao wanaogopa pesa ya mabeberu isiingie nchini kinyamela. Nchi zinazopata misuko suko huwa kuna donor somewhere anaingiza nguvu ya pesa, wao hapo wamebana. Vyama vya siasa wamepewa mashart magumu kuliko yenu, wao kiasi chochote wanachopewa wanahitaji kuriport serikalini, na balozi zote zimepewa masharti ya jinsi na namna ya kusaidia vyama vya siasa na NGOs, lengo lao ni kuhakikisha hakuna anayepata pesa nje serikali isifahamu, huo ndio udhibiti walioweka. Ubalozi au shirika lolote la nje likitaka kukisaidia chama cha siasa kwanza serikali inapewa taarifa za kiasi na malengo ya msaada, na ndio maana uliona ulifanyika uhakiki wa NGOs zote na kuweka masharti ya kutoa taarifa za mipango kazi yao mara kwa mara serikalini.
Walengwa siyo nyie wananchi wakawaida, nyie mmekumbwa na mtego wa panya. Kulinda madaraka siyo kazi rahisi, lazima yatengenezwe mazingira magumu kwa kila mtu ili ionekane ni kawaida, na siku wakibinywa waseme hii siyo kwao tu bali ni nchi nzima.
Hivyo msimlaumu Dr. Mpango, yeye ni mtekelezaji wa mipango iliyo kwisha ratibiwa serikalini. hata akifahamu hasara ya sera Fulani leo, hawezi kubadirisha kama imeamriwa hivyo. Nyie mnadhani Bashe anaakili sana kuliko Dr.mpango, ni kwasababu mpango hutekeleza mipoango iliyopo hatengenezi sera yeye.
 
Back
Top Bottom