Uchaguzi 2020 Kanuni mpya CCM: Tumaini la pekee la Makonda, Mtulia, Mtolea, Nassari, Mwakyembe na Mwanri ni Kamati Kuu ya CCM chini ya Rais Magufuli

Ndugu yangu Peter upo kwenye jukwaa hili la siasa muda mrefu kwelii wewe wakusema "KANUNI MPYA" wakati hata 2010,2015 zilikuwepo, na mifano hai ipo wakina Kigwangala.
Mkuu, wakati ule majina matatu ya kupigiwa kura yalitokea Kamati Kuu halafu yakapigiwa kura na kurejea huko. Kwasasa, wote waliotia nia wamepigiwa kura kwanza kabla ya kupelekwa Kamati Kuu kwa maamuzi. Huo ndiyo upya. Tena, wakati ule wanachama wote wa CCM jimboni walipiga kura. Kwasasa ni Kamati ya Jimbo tu ndiyo iliyopiga kura. Kanuni zimebadilika.
 
Nadhani kilichobadilika ni utaratibu tuu namna na upigaji kura lakini KANUNI YA KAMATI kuu kuwa mwamuzi wa Mwisho imebaki palepale.
 
Zako zinasemaje? Kwamba kura za maoni ndiyo mwisho?
Ndo mana nikakwambia acha uongo..hii kanuni sio ivo weeh ulivyoutafsiri ilihusu zaidi kama mgombea hakupatikana kwa misingi ya haki...its means labda kwa mipango ya Rushwa au vitisho ndo akamaanisha kutakua na panga la mwsh..asa unaleta uzi wa uongo tukuangalie tuu
 
Nakuunga mkono
 
Sidhani Kama kamati kuu lengo lake Ni kuonesha "ubabe" wao kwa kuchagua yeyote wanayemtaka.Wenye "tumaini" kwa kamati Ni wale ambao pengine mchakato wa kupata mshindi wa kura za maoni uligubikwa na makandokando mengi au mshindi kuwa walakini.Amini,kwa Mambo yalivyokwenda,asilimia kubwa ya walioongoza Katika mchakato wa awali ndio watakaopitishwa.
 
Nadhani kilichobadilika ni utaratibu tuu namna na upigaji kura lakini KANUNI YA KAMATI kuu kuwa mwamuzi wa Mwisho imebaki palepale.
Ili kutokuleta mgawanyiko, makonda apitishwe kugombea Buchosa, Dr tizeba aende sumve, na shigongo aende Kibamba. Mwanry apelekwe Kawe
 
Mkuu, nasikitika kukuambia kuwa hujui chochote kuhusu jambo hili nililolizungumzia. Tafuta Kanuni na uzifahamu. Usilazimishe kubisha wakati huna hoja ya maana.
 
Ili kutokuleta mgawanyiko, makonda apitishwe kugombea Buchosa, Dr tizeba aende sumve, na shigongo aende Kibamba. Mwanry apelekwe Kawe
Ili iweje sasa??CCM hawafanyi mambo ya hovyo to that extent, ulipogombea ndipo unanafasi ya kurudishwa na sio kuhamishwa ukagombee sehemu nyingine huko unapoenda kwengine utaenda kumuomba kura mwanaCCM gani wakati hawakutambui?
 
Tusifanye Mambo kwa mazoea, mgombea akipewa bendera anakuwa wa chama ndio kitakacho mnadi, Sasa hivi kinachoendelea nimapendekezo tu
 
Kwenye hili la kamati kuu kupitisha wagombea watakaosimama kwenye majimbo, kuna watu watalia na kusaga meno

Inategemea nimeamkaje
 
Tusifanye Mambo kwa mazoea, mgombea akipewa bendera anakuwa wa chama ndio kitakacho mnadi, Sasa hivi kinachoendelea nimapendekezo tu
sasa utampeleka sehemu ambayo hakubaliki braza vipi??hajagombea hilo eneo kwasababu anajua hana ushawishi eneo husika.
 
Well said uko vizuri mkuu
 
Kuna kipengele kimeongezwa kinasema "maamuzi ya nani atakua mgombea kupitia ccm yatategemea pia jinsi mwenyekiti wa chama taifa alivyoamka siku hiyo ya maamuzi"
Atakavyoamka siku hiyo hajasema kuwa atahamisha mtu kutoka kusini akagombee kaskazini. Na kanuni za chama zipo wazi kuwa majina matatu ndio yataenda kamati kuu kujadiliwa, washindi watatu wa mwanzo.
 
Watu mnakuwa wa ajabu,Magu angetaka apite angepita Kigamboni,huko kapigwa chini na kamati itampiga chini
Kigamboni angempitishaje wakati kila mjumbe anapiga kura ya siri? Una maana wajumbe karibia 400,angawalazimiza wampigie makonda kura?!! Huko kwenye kamati kuu inakuwa rahisi kama ataamua, kwakuwa atakuwa ndio kiongozi, na kule hawapigi kura, wanatumia vigezo vyao tu, kumbeba mgombea kulingana na matakwa yao! Na akilazimisha sana ndipo hutokea jimbo kupotea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…