Kansa ya uongozi wa CCM aliyoisema Nyerere


N

Nikupateje

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2009
Messages
1,315
Likes
113
Points
160
N

Nikupateje

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2009
1,315 113 160
Yafuatayo ni maneno ya Julius Nyerere kwenye kitabu chake UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA:
Kwenye ukurasa wa 66 anasema hivi:

....."Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa vyama vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza nchi yetu badala CCM au ambacho kingekilazimisha Chama Cha Mapmduzi kusafisha uongozi wake kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao""......

Kitabu hiki alikitoa mwaka 1994. Lakini alipendekeza mfumo wa vyama vingi kwenye tarehe za February 1990, miezi sita kabla haja-step down uenyekiti wa CCM.

Hii ina maana gani? Maana yake ni kwamba ubovu wa uongozi wa CCM anaousema ni kabla ya tarehe alipotoa pendekezo hilo, yaani kabla a February 1990. Kwa ambao hatukumjua tunaweza kusema ni ubovu anaousema ni nyuma ya tarehe hii au hata nyuma ya December 1989.

Kumbuka wakati huo ni miezi 30 baada ya mkutano mkuu wa tatu wa CCM uliofanyika Kizota, Dodoma huku yeye akiwa Mwenyekiti wa CCM. Kwa waliomuelewa uelewa wake wanaweza kusema ni dhahiri kuwa kansa ya uongozi anayoisema si ya miezi michache hiyo tena yeye akiwa Mwenyekiti na wakati huo hata Azimio la Zanzibar halijalifuta Azimio la Arusha.

Kumbe kansa ya uongozi inaweza kuwa ni ile aliyoiona mara tu alipoacha urais yaani November 1985 na alipozunguka kuona uhai wa Chama.

Nisaidieni kutafakari yanayonitatiza udadisi wa akili yangu. Anatamka hivi huku CCM ikiwa haina miaka hata miaka saba imeonyesha uongozi imara kwa kumshughulikia Aboud Jumbe mwaka 1984. Vilevile ikiwa haizidi miaka miwili ikiwa imewashughulikia Seif Shariff Hamad na wenzake mwaka 1988.

Kwa akili kali ya Mwalimu, si rahisi kuwa alichokisema mwaka 1990 alikurupuka kwa research yake ya miaka miwili tu. Inawezekana wazo la kutaka virudi vyama vingi alikuwa nalo ikibidi mwishoni mwa miaka ya uraisi wake na kabla hata Jumbe na Seif hawajashughulikiwa.

Je, wenzangu mnaonaje? Si kwamba wale waliokuwa wanatimuliwa ni kwamba kwa namna moja walikuwa wanaelekezwa walete vuguvugu la vyama vingi ambalo kwa Nyerere ni wazo lililokuwa linatembea kichwani mwake?

Jadili.
 

Forum statistics

Threads 1,235,851
Members 474,755
Posts 29,238,473