Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Yapata miaka miwili imepita tangu mke wangu alipogundulika ana saratani ya matiti, tulianza dozi ya CHEMOTHERAPY pale GOOD SAMARITAN CANCER HOSPITAL Ifakara, tulipatiwa jumla ya mizunguko 8 ya CHEMO, hali ilionekana kuwa nzuri ila ndani ya muda mfupi sana uvimbe ulianza tena.

Baada ya kuona uvimbe umeanza upya tulihamia Dodoma BENJAMIN MKAPA napo tulipatiwa chemo 4 kisha ukafanyika upasuaji ili kuondoa titi lililoathirika na saratani, upasuaji amefanya mwezi wa 4 mwaka huu.

Baada ya upasuaji hali ilionekana kama ipo vizuri, ila baada ya miezi ipatayo mi3 mgonjwa ameanza kusumbuliwa tena.

Anasumbuliwa na; MAUMIVU MAKALI SANA MAHALA ALIPOFANYIWA UPASUAJI
KIDONDA KISICHOPONA (kilianza kidogo sana, kama kiji upele, hatimae kikakua. Hakionyeshi dalili ya kupona.

Najua yote ni mipango ya Mungu, ila sina matumaini kama mke wangu anaweza kupona kwa sasa.

KUNA MTU ASHAWAHI KUUGUZA MGONJWA WA SARATANI naomba ushuhuda ambao unaweza nisaidia cha kufanya.

KAMA KUNA DAWA ZA TIBA MBADALA ULITUMIA ZIKASAIDIA, NAOMBA MSAADA PIA.

Kwa sasa mgonjwa yupo tu nyumbani tunasubiri neema ya Mungu

Ushauri wowote pia napokea.
Mkuu
Chukua mmea wa cactus chukua na kilo tatu ya unga wa mbegu za parachichi chemsha maji lita tano kisha chuja yapoe kidogo anywe nusu lita ahsubuhi na jioni. Hakikisha anatumia mwezi mzima kisha tuletee matokeo kama anaanza kujisikia vyema.

Rudia zoezi kwa miezi mitatu naamini utaanza kuona matokeo. Akipata nafuu okoa maisha ya wengine kuwaambia ukweli. Usilipie huu ushauri
 
GOOD SAMARITAN CANCER HOSPITAL, hospital maalumu kwa ajili ya kansa ipo ifakara.

Benjamin mkapa napo clinic ya kansa ipo

Sijui sio sehem sahhihi kwa maana gan?
Kabla ya kumpa chemo. walitakiwa waanze na radiotherapy
 
Mkuu
Chukua mmea wa cactus chukua na kilo tatu ya unga wa mbegu za parachichi chemsha maji lita tano kisha chuja yapoe kidogo anywe nusu lita ahsubuhi na jioni. Hakikisha anatumia mwezi mzima kisha tuletee matokeo kama anaanza kujisikia vyema.

Rudia zoezi kwa miezi mitatu naamini utaanza kuona matokeo. Akipata nafuu okoa maisha ya wengine kuwaambia ukweli. Usilipie huu ushauri
Ahsante sana mkuu
 
Kwanza kabisa pole sana mkuu...... am going through the same issue

Hapo jambo la msingi ni ipo stage gani?
Kuna stage ikifika basi ni miujiza tu inatakiwa kwa Chemo na mionzi

Tiba mbadala zinatumika sana lakini so far hakuna ushahidi wowote kwamba zimewahi kumtibu mtu akapona.....
Unaweza kujaribu lakini kuna matapeli wengi sana na utatumia hela nyingi sana pia ila hakuna uhakika

Mtafute memba anaitwa Mzizikmavu anadai anajua tiba yake
 
Daaah! hii dunia acheni tu!
MGONJWA WANGU MARA ANAKUA KATIKA HALI YA KULETA MATUMAINI, MARA GHAFLA LINAIBUKA TATIZO JINGINE !

SASA MOYO UMEANZA KUMSUMBUA, MAPIGO YANAENDA KASI ISIVYO KAWAIDA

PIA DAMU INAPUNGUA SANA.

MARA NYINGINE ANAPATA CHANGAMOTO YA UPUMUJI.

Sijui ndo side effects za CHEMOTHERAPY
Pole kwa unayopitia ndugu. Mungu akufanyie wepesi kwa kweli
 
Kwanza kabisa pole sana mkuu...... am going through the same issue

Hapo jambo la msingi ni ipo stage gani?
Kuna stage ikifika basi ni miujiza tu inatakiwa kwa Chemo na mionzi

Tiba mbadala zinatumika sana lakini so far hakuna ushahidi wowote kwamba zimewahi kumtibu mtu akapona.....
Unaweza kujaribu lakini kuna matapeli wengi sana na utatumia hela nyingi sana pia ila hakuna uhakika

Mtafute memba anaitwa Mzizikmavu anadai anajua tiba yake
Kuna namna ya kujua stage? Wakati tunaigundua kwa mara ya kwanza, mwanzo mwa mwaka 2022 walisema ni stage 2 or 3
 
Kuna namna ya kujua stage? Wakati tunaigundua kwa mara ya kwanza, mwanzo mwa mwaka 2022 walisema ni stage 2 or 3
Ndio mkuu kuna namna wanapima kujua ipo stage gani
Kuna stage 0 hadi stage 4

Stage zinatokana na namna ugonjwa ulivyo sambaa kutoka kwenye uvimbe katika nyonyo na kwenda kwenye sehemu zingine za mwili

Kadiri stage inavyozidi kuwa kubwa maana yake kansa imesambaa zaidi
Na kadiri stage inavyokua kubwa ndio ugumu wa matibabu unaongezeka

Stage 4 is almost haitibiki maana inakua imesambaa sana hadi kwenye organs hatari
 
Aisee

Kwa sasa tunasubiri miujiza tu
 
Back
Top Bottom