Kansa kubwa inakula vyama mbadala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kansa kubwa inakula vyama mbadala

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by LUS0MYA, Oct 14, 2012.

 1. LUS0MYA

  LUS0MYA JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  1.DEMOKRASIA FINYU NDANI YA VYAMA VYENYEWE
  Vyama vya siasa mbadala vinaonekana kama mali ya watu binafsi,waasisi,wenye mvuto, ambao mawazo yao ndiyo mawazo ya vyama hivyo!Demokrasia ndani ya vyama si tu kushiriki katika chama bali chama kuweka bayana haki za kila mwanachama ndani ya chama na haki hiyo haina mbadala wala kushikwa au kuzuiwa na mtu yeyote ilimradi taratibu(regulations)za vyama zinafuatwa.Haki kubwa ya kila mwanachama ni uwezo wa kugombea nafasi yoyote na kuchagua mtu yoyote!mfano Kitendo cha ZZK kutangaza nia yake ni haki yake ndani ya chama na ichukuliwe hivyo.katika kipindi hiki ambacho watu wanataka mabadiliko ni muhimu sana watu wenye nia ya kushika madaraka makubwa kama hayo kujitokeza mapema ili waweze kupimwa na wanachama na jamii nzima kuliko kukaa hadi unapobaki muda mfupi mtu anajitokeza na hivyo kunyima fursa watu kutafakari,kuchunguza,kujadili na hatimaye kuamua!ZZK amelonga wengine wenye nia wajitokeze tuwaone kuliko kuanzisha mashambulizi dhidi ya Zitto ambayo sasa nionavyo mimi yanabomoa chama.

  2.UWAZI WA MATUMIZI YA FEDHA ZA VYAMA
  Vyama vingi mbadala hili ni tatizo kubwa ambalo hata chama tawala inalitegemea sana katika kudhoofisha vyama.Hakuna taratibu za wazi za matumizi ya fedha ya vyama na utaratibu shirikishi wa matumizi ya fedha.maana yangu ni mambo gani ya kufanya kwanza kutokana na fedha kidogo iliyopo.(Priority of expenditure).Watu gani wanaopanga bajeti za vyama na uwezo huo wamepewa na wanachama wenyewe.Mathalani vyama mbadala vimejisahau kuwa kipindin hiki ni kipindi cha mapambano ya mageuzi hivyo wanachama wenye uchungu wajitolee kutokana na nafasi zao kusaidia vyama ili fedha kidogo iliyopo itumike kujenga chama na wanachama wake.Mfano sioni mantiki ya vyama kulipa mamilioni ya fedha kwa ajili ya mawakili wanapowakilisha vyama katika kesi mbali mbali ili hali wao ni wanachama na wakati mwingine ni viongozi waandamizi au kujilipa posho kubwa kiasi kundoa imani ya wanachama kama kweli lengo ni mabadiliko ya kweli au maslahi binafsi.

  3.MAFISADI
  Vyama mbadala vimekuwa mstari wa mbele kupigana kwa nguvu zote kusemea masuala ya ufisadi katika nchi lakini nitwashangaza kidogo kuwaambia kuwa ufisadi sasa umegeuka sumu katika vyama.misimamo mikali imegeuka kuwa ya wastani na baadhi ya viongozi ndani ya vyama wameshalishwa hii sumu ndani ya vyama kiasi hawana hamu tena ya uongozi ndani ya vyama.Ifahamike wazi kuwa kamati muhimu za bunge zipo chini ya upinzani na baadhi yao zimeanza kuhusishwa na rushwa!mathalani baadhi ya wabunge wamekuwa wakitumika kupitisha mambo fulani fulani kwa maslahi ya matajiri!Wengine wamekuwa marafiki wa karibu wa wale tuliohubiriwa muda mrefu kuhusika na ufujaji na ufisadi katika nchi hii.Mwishoni kabisa baadhi ya viongozi wetu katika vyama mbadala sasa wanahodhi utajiri mkubwa ambao unatia shaka jinsi ulivyopatikana!

  4.MAGAZETI NA MITANDAO YA KIJAMII
  Magazeti na mitandao ya kijamii ni nguzo kubwa katika kueneza upepo wa mabadiliko na imekuwa chachu ya mabadiliko tunayoyaona sasa.Habari za shughuli za kisiasa na mabadilko zinauza sana magazeti na baadhi ya magazeti yanaaminika kwa wananchi kutoa taarifa sahihi zinazohusu mabadiliko na shughuli za vyama mbadala.Baadhi ya magazeti pendwa na mageuzi yamebadilika na kutoa taarifa zinazochochea migogoro katika vyama na hata mara nyingine vita vya ndani ya uongozi wa vyama inapiganiwa kwenye magazeti!Na hata mitandao ya kijamii imeingiliwa sasa.

  Mtazamo wangu hii ni kansa ambayo imo ndani ya vyama mbadala ambayo isipodhibitiwa mageuzi yatabaki kuwa ndoto na watu wataendelea kuishi katika mfumo huu uliopitwa na wakati.dawa ya kansa ni mionzi au kukata sehemu iliyoathirika na tiba ya mapema ndiyo itaokoa vyama mbadala.NAWAKILISHA
   
 2. m

  mishalejuu Senior Member

  #2
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hoja nzuri! michango iendelee ili tuachane na kushambuliana sisi kwa sisi.. mwenye uwezo wa kugombea ngazi yoyote aseme mapemaaaaa ili wanachama tutafakari nakutoa maamuzi ...sio mtushitukize kama ccm... huwa waashitukizana ndio maana kila anayeingia ni mbovu.
   
Loading...