Kanitapikia akanilipa

dist111

JF-Expert Member
Nov 29, 2012
3,698
3,084
Mlevi kamkuta mlevi mwenzie analia nje ya baa;

KOLU: We vipi tena unalewa mpaka unalia? Au umeishiwa hela ya kunywa nikakununulie?
DOLU: Nimejitapikia, mke wangu mkorofi nikifika atanidunda sana.
KOLU: Tumia akili, chukua noti ya alfu kumi, weka kwenye mfuko wa shati, ukifika hom mwambie mkeo kuna mlevi alikutapikia akakulipa alfu kumi kaweka kwenye mfuko wa shati akiiona atakuelewa.....DOLU akakubali kisha akaelekea kwake, alipofika mkewe kumuona tu;
MKE: We mshenzi, leo umelewa mpaka umejitapikia, utanitambua.
DOLU: Subiri mke wangu kuna mlevi alinitapikia akaniomba msamaha akanilipa alfu kumi iko kwenye mfuko wa shati....MKE akaingiza mkono kwenye mfuko akakuta shilingi alfu ishirini.
MKE: We si umesema alikulipa alfu kumi mbona kuna alfu ishirini?
DOLU: Unajua kwa bahati mbaya aliniharishia pia kwa hiyo akaongeza hela
 
Ha ha ha ha ha ha haaaaaaaaaaa sirudii tena kusoma hivi vichekesho huku naendesha gari maana nimecheka hadi nusura nigonge kaHarrier mbele yangu
 
aisee dist tafadhali sana bwana uwe unaangalia hata aina ya vichekesho unavyovitoa kwa sababu inaweza ikatokea ukauwa watu kwa vicheko. kwa mfano mimi hivi sasa ninakimbizwa muhimbili kutibiwa mbavu zangu zilizofyatuka kwa kucheka kuhusu hicho kisa cha mlevi. Hiyo imetulia sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom