Freyzem
JF-Expert Member
- Jun 29, 2013
- 10,113
- 24,642
Kanisa takatifu la Galilee ambapo Yesu Kristu aliwalisha watu 5000 kwa mikate mitano na samaki wawili
Misa maalum imefanyika kufungua rasmi kanisa Katoliki Kaskazini mwa Israel ambalo liliteketezwa na Wayahudi wenye itikadi kali mwaka wa 2015.
Kanisa hilo lililoko eneo la Tabgha kando mwa ziwa la Galilee linaaminika na Wakristo kama eneo takatifu ambapo Yesu Kristo alifanya muujiza wa kuwalisha watu 5000 kwa mikate mitano na samaki wawili pekee.
Ukarabati wa kanisa hilo ulichukua miezi minane na kugharimu kima cha dola milioni moja.
Kanisa hilo huwavutia mahujaji wengi Wakristo kila mwaka
Licha ya Wayahudi watatu wenye itikadi kali kupatikana na makosa ya kuchoma kanisa hilo hata hivyo hawakuhukumiwa.
Uvamizi huo uliharibu maktaba ya kanisa na jengo nzima.
Hata hivyo sakafu yake iliyotengenezwa karne ya tano ilinusurika uharibifu huo.
Kanisa hilo lilifunguliwa rasmi kwa misa Jumapili.
Ujumbe ulioandikwa kwa Kiebrania wa kulaani kuabudiwa kwa sanamu ulipatikana ukiwa umeandikwa kwa rangi nyekundu ukutani baada ya shambulio.