Kanisa la RC Nyangh'wale mkoani Geita

Kanisa la RC Nyangh'wale mkoani Geita

Ph-25

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2012
Posts
1,159
Reaction score
540
Hili ni moja ya kanisa kongwe kidogo hapa wilayani na mkoani pia,kanisa hili tangu aondoke Padre mmoja aliekuwa anaitwa Bilinge, halijawahi kupata Padre ambae anaelewana na waumini.

Huyu aliepo sasa ndiyo anasababisha mitafaruku mingi sana kila leo, waumini wanatukanwa kanisani matusi mazito mazito haijalishi una umri gani nikutukanwa na padre tu.

Saizi ameanzisha utaratibu kwa waumini wote ni marufuku kwenda kwenye sherehe yeyote iwe harusi au sendof kama haujaolewa au kuoa, nimarufuku kwenda ktk msiba wa mtu ambae alikua hasali haijarishi kama ni ndugu yako wala nini.

Enyi waungwana wenye kuweza kuokoa jamii hii inayo farakanishwa na huyu padre wasaidieni hawa watu pls.
 
tulia awanyooshe. Kazi ya kuwasaidia wabongo sumbufu kwenda mbinguni inabidi uwe strikti.
 
Huku Nako watatusumbua,wameelekezwa hiki,wanafanya kile.

Hosea 9: 5
Mtafanya nini katika siku ya mkutano wa idi, na katika siku ya karamu ya Bwana?

mbona sisi hatujasumbuka nilikuwa mroman katolic nikaingia uislamu nina amani tosha
 
Lipo sehemu gani ilo kanisa nije kuwasaidia ilo tatizo Dogo
Katoro Nyankumbu Geita Town Magogo Mkoani Mwatulole Shilabela Kalangalala Bwanga Chato Kasamwa Nyantorontoro Bukoli Busanda Nyakabale Nzela Nyarugusi
 
Wote mliocoment humu Bado hamjamsaidia kitu huyu mjumbe!

Iko hivi ndugu mjumbe hapo kanisani nadhani Kuna viongozi wenu wa halmashauri walei na pia Kuna viongozi wenu wa uwaka na wawata Sasa Hawa kwa pamoja wakiungana nakuwa kitu kimoja huyo padri hatochukua Muda mrefu kwenye iyo parokia.

Ili parokia isonge mbele ni lazima kuwe na mashirikiano ya pamoja na sio mtu mmoja kujiamulia tu vile anavyojisikia.

Ombeni mkutano kutoka halmashauri viongozi wote wa jumuiya wawe na msimamo mmoja kwamba hawatotoa michango yoyote Wala kushiriki kwenye maendeleo ya parokia naamin na Jimbo nalo likipata taarifa huyo paroko hachukui muda atahamishwa na kuonywa iyo tabia yake
 
Back
Top Bottom