Wakotoriki nawaomba msome UFUNUO WA YOHANA na mpate mtu wa kufunulia au nendeni hata Google ili iwasaidie kama mimi ilivyonisaidia. Ninawaambia haya ili mpate kujua juu ya Imani, mimi nilikuwa Mkatoriki wapendwa na nikapata Komunio ktk kanisa la Mbagala Zakhem na nina vyeti nilivyopewa na Roman ila kwa sasa NIMEOKOKA maana nimeijua kweli ya Mungu. Mungu halijui Dhehebu wala Dini ila anachojua ni WOKOVU ili watu wapate kuokoka wapendwa. Madhehebu na Dini zilikuwa tangu enzi za Yesu kama Mafarisayo na Masadukayo ila Wokovu umekuja na Bwana Yesu Jamani. Wale waliokoka nadhani wananielewa kwa mapana sana. Pentekoste sio dhehebu wala dini ila ni siku ambayo Roho Mtakatifu alianza kazi ndani ya Kanisa lilioamini ktk Yesu 'Matendo ya Mitume sura pili(2) utakuelewesha vema juu ya hili' na ndio maana waliokoka huwa wanaujazo wa Roho Mtakatifu. Wapendwa ukitaka kujua Mambo ya Rohoni na Mungu ajifunue kwako OKOKA ili upate kumtambua Bwana Yesu sawasawa. Si kwa Katoriki tu, hata kwa Walutherani, Wasabato, Anglikana na n.k. Kama nimewakwaza Naomba mnisame ijapokuwa imenilazimu nifanye hv ili Mpate KUOKOKA. M'barikiwe