Kanisa Katoliki na Tsh Bilioni 19

Kanisa Katoliki na Tsh Bilioni 19

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
18,253
Reaction score
26,641
Kanisa Katoliki na Tsh Bilioni 19

Kanisa Katoliki ni taasisi tajiri sana duniani, shirika lao moja tu la Opus dei lipo kwenye orodha ya taasisi 10 za kidini tajiri duniani.

Ukichukua utajiri wa Mo Dewj wa $1bilion ambaye ndiye tajiri mkubwa kwa utajiri hapa East Afrika na kati + na utajiri wa Azam haufikii shirika la Opus Dei.

Mali za kanisa katoliki zinamgawanyo wa kitaasisi na mashiriki. Wana mashirika mengi na taasisi nyingi duniani yakifanya kazi kwa uhuru. Lakini yote yakiwa na mahusiano ya karibu na Ukulu wa Roma (Roman see). Vatican ambayo nayo ipo chini ya ukulu wa Roma nayo ina utajiri sana ingawa utajiri wake haujawekwa wazi kwasababu wanazoona wenyewe. Kando ya mashirika ya Katoliki kuna makanisa ya kitaifa kama lilivyo kanisa Katoliki Tanzania. Yakijiendesha kwa uhuru kwa kumiliki mali na utaratibu wa kifedha.

Mfano utajiri wa kanisa Katoliki la Ujeruman, makadirio ya utajiri wake ni US$ 265.62 bilioni sawa na pesa za Kitanzania Tsh 665.5 Trilioni. Hapo ni sawa na GDP ya nchi 8 zinazounda East Afrika kasoro $47 B. Wakati GDP ya Tanzania ni USD 87 bilioni. Sasa ukikusanya utajiri wa kanisa zima la katoliki na mashirika yake unafikiri watakuwa na utajiri wa kiasi gani?

Kanisa Katoliki limekuwepo Tanganyika kabla haijakuwa Tanganyika.Mapema sana, makuu ya Kanisa Katoliki yalifika katika maeneo ya Zanzibar na pwani ya Bahari ya Hindi mwaka 1860-1863.

Kwa mfano, shirika la waamini Katoliki (mission) la kwanza lilianzishwa Zanzibar mwaka 1863 na kutoka hapo likapanuka kwenda kwenye pwani na kanda za ndani ya Tanganyika (leo Tanzania)

Majengo ya Kanisa Katoliki yaliopo Dar es Salaam, kama St Joseph's Cathedral Dar es Salaam, yalijengwa kati ya 1897 na 1902 na kuadhimishwa rasmi mwaka 1905.

Idadi yao nchini

Makadirio ya idadi ya Wakristo Wakatholiki nchini Tanzania ni karibu 18,076,000 (hadi Desemba 31, 2021) ambao wanawakilisha takriban 30.4% ya idadi ya watu wote nchini.

Taarifa nyingine inaonesha “zaidi ya waumini 23 milioni” kwamba ni karibu theluthi moja ya idadi ya watu nchini.

Hivyo ni salama kusema kuwa Kanisa Katoliki lina waumini wengi, takriban kati ya 18-23 milioni nchini Tanzania.

Hao tu ni mtaji wa kutosha wa kanisa. Kama kila mmoja akitoa sadaka ya tsh 100 kwa kila misa ya jumapili tu, watakuwa wameingiza Tsh 2,300,000,000 bilioni.

Hali ya utajiri na mali

Kuna makala zinazosema kwamba Kanisa Katoliki ina rasilimali nyingi nchini, hasa kupitia vituo vya elimu (shule za msingi, sekondari), taasisi za afya, vikundi vya kijamii na mali zisizo za kibiashara.

Kwa upande wa Tanzania Episcopal Conference (TEC) ya Catholic Church in Tanzania, namba zinazopatikana za taasisi za elimu zinazoendeshwa na Kanisa Katoliki ni kama ifuatavyo:

Shule za msingi: 147

Shule za sekondari na minor seminars: 245.

Vituo vya mafunzo ya ufundi (Vocational Training Centres): 110.

Vyuo vya walimu (Teachers Training Colleges – TTC): 13.

Vyuo vikuu au vyuo vya juu: 4

Hivyo kwa uwiano wa asilimia kwa upande shule za msingi na secondary kwa Katoliki na seikali ni kati ya 25% kwa 75%.

Vituo vya afya

Kanisa Katoliki lina jumla ya vituo vya afya 494 nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na hospitali, vituo vya afya, dispensari, n.k.

Kulingana na TEC tovuti, Kanisa lina:

328 dispensari,

52 health centres,

14 “designated district hospitals” (DDH),

29 voluntary agency hospitals (VA)

Ingawa hakuna ukadirio kamili au mali yote ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania iliyo hadharani kuchapishwa, ni wazi kwamba ni moja ya taasisi za dini zenye uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu na afya.

Hivyo basi raia wengi wa Tanzania na hata viongozi tulionao wamepitia katika mikono ya elimu ya kanisa hili. Na zaidi ndugu, jamaa wa kitanzania ni wafaidika wa huduma za kielimu na afya kutoka kwenye kanisa hili. Hivyo hawa ni wadau wakubwa kwa serikali. Hivyo kufanya vita nao ni kufanya vita na jamii. Kuchoma vituo vyao vya kielimu na afya ni kuangusha 30% ya nguvu ya taifa.

Usifikirie

Kanisa la Katoliki Tanzania linaishia Tanzania bali ni kipande kidogo sana ambacho kinaungana na ukulu wa Roma (Roman see) ambayo ipo chini ya ukulu wa papa (Holy see) ambao una nguvu ya kiulimwengu. Maana holy see inauhusiano wa kidiplomasia na zaidi ya nchi 180 duniani kote pamoja na taasisi kubwa duniani kama UN, Umoja wa Ulaya nk. Hivyo kupambana na Katoliki ni kupambana na jumuia za kimataifa. Na daima hakuna taifa hapa duniani ambalo lilifanikiwa kupambana nao na kushinda. Wapo waliojaribu lakini mwisho kanisa la Roma likaibuka kidedea. Hivyo kwa aina ya wale wakosoaji niliowaona sidhani hata kanisa la Roma litapoteza muda kuwajibu.

Pia kama bilioni 19 ndio hoja kuu ya taasisi ya wahadhiri wa kislamu ya kulitetemesha kanisa la Roma basi wajue hiyo kwa kanisa hilo ni pesa ya nyanya kwao. Kama jimbo tu la Bagamoyo limekusanya mavuno ya bilioni 1.2, vipi kuhusu kanisa zima la Tanzania?. Na zaidi ni uzushi, kanisa la Roma halilipwi hizo pesa na serikali kama wanavyodai.

Makala ijayo ni kuhusu MoU (Memorundum of understanding) ni nini?

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika
 
Nimeishia hapo uliposema mo ni tajiri East Africa na kati !

Vyanzo vyako vinakudanganya !

Catholic? It's true wako vizuri kiuchumi
 
Kanisa Ni Tajiri
Nakumbuka Yule Askofu Wa Kilimanjaro Wakati Wa Jiwe Alimwambia Kanisa Halitishwi Na Mtu Yoyote. Askofu Wa KKKT
 
Halafu masheikh ubwabwa wanataka wajibiwe na TEC😂

TEC hawana uwezo wa kuwajibu masheikh sababu, Wana upeo mdogo sana wa Elimu na kujenga hoja.

Kwa ufupi ni watu wazandiki, wanafiki na wachochezi.

Suala la utajiri ni vitu au umakini ni vitu viwili tofauti.
 
Nimeishia hapo uliposema mo ni tajiri East Africa na kati !

Vyanzo vyako vinakudanganya !

Catholic? It's true wako vizuri kiuchumi
Tuambie wewe ni nani tajiri zaidi hapa Afrika mashariki na kati?
na vyanzo vyako ni vipi?
 
Tuambie wewe ni nani tajiri zaidi hapa Afrika mashariki na kati?
na vyanzo vyako ni vipi?
Hata kama siwajui matajiri wote wa East Africa, lakini MoDewji hata kwa Tanzania hayuko kwenye top 5.

Modewji ni mbabaishaji na mjanjamjanja tu. Angekuwa na hela angekuwa ameshaweka ile Tsh 20 Bilioni kwenye Club ya Simba
 
Ukiacha utajiri wa kanisa Katoliki, pia ni kanisa lenye mifumo dhabiti ya kiuongozi, kutoka ngazi ya jumuia hadi jimbo, na hutasikia migogoro yoyote ya kimasilahi.
 
Hapo kwa kanisa la ujeruman umenena vyema

Ndo kanisa tajiri zaid ulimwenguni
 
Umesahau ardhi,,kanisa katoliki lina maheka ya ardhi wanamiliki Tanzania..
 
Back
Top Bottom