jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 36,155
- 29,677
Kanisa la Anglikana Tanzania limepongeza na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais wa Tanzania Dkt.John Magufuli katika kupambana na ufisadi huku katika Dayosisi yake ya Ruvuma likiwa limejipanga kufufua mashamba yake ya miwa na kiwanda cha sukari huko lundo Nyasa mkoani Ruvuma ili kupunguza uhaba wa sukari nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Askofu mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Mhashamu Askofu Jacob Chimeledya huko Liuli Wilayani nyasa mkoani Ruvuma wakati wa kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu wa kanisa hilo Dayosisi ya Ruvuma Askofu Raphael Haule anayekuwa Askofu wa nne wa Dayosisi hiyo anayechukua nafasi ya Askofu mstaafu Martenus Kapinga.
Kwa upande wake Naibu waziri wa elimu,Sayansi na Teknoloji Mheshimiwa Stela Manyanya aliyeiwakilisha serikali katika shughuli hiyo amewataka viongozi wa dini kusimamia malezi ya jamii na maadili kwa kuwa maadili mema na mila na desturi za kitanzania zinapita katika wakati mgumu na hatua zisipochukuliwa hali itakuwa mbaya zaidi.
Nao waumini wa kanisa hilo dayosisi ya Ruvuma wamemshauri Askofu wa Dayosisi ya Ruvuma Askofu Jacob Chimeledya kuwaendeleza kielimu wachungaji wa kanisa hilo.
My Take:Zile Sala Zetu ndio hizi
Source ITV
:: Kanisa La Anglikana Lamuunga Mkono Rais Magaufuli Katika Mapambano Ya Ufisadi